Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tujifunze kupiga MWIZI! -SOMO LA KWANZA

>> Wednesday, February 02, 2011

KILA kitu  ni shule,...
.... na ndugu wananchi labda leo tujifunze kutoka katika kitendo maarufu mtaani  cha KUPIGA MWIZI!



 Au nianze hivi:




Moja ya kitu kirahisishiacho watu kufanya vitu  mpaka hata KUUA,....
.... ni kuviita jina jingine,...
... na KISAIKOLOJIA  kujiandaa kwa kujiaminisha KITENDO wafanyacho hakikufanywa kwa nia  mbaya hata kama moja ya matokeo yake yanajulikana yanaweza KUUA  mtu.:-(

Ndio,...
.... kuna mpaka wajisikiao  kukiri kirahisi kuwa WAMECHINJA kuku na WATASITA  kuita kitendo HICHO  cha uchinjaji huo  ni KUUA,...
..... hata kama ni KUKU kwa kuwa tu  neno KUUA  halina ladha nzuri kwa wastaarabu kutokana tu na lihusianishwavyo na unyama na sio ule UTU.:-(

NDIO,...
.... binadamu  kwenye kundi ukiwapa sababu kuwa wampigaye ni MWIZI au tu ADUI wanaweza kirahisi KUUA,...
..... halafu wakaenda nyumbani na kulala SHWARI KABISA kisa kitendo chao KISAIKOLOJIA wamesha kijengea mlainisho kuwa walichokuwa wanakifanya ilikuwa ni KUMUADHIBU  MWIZI  TU na sio KUUA  mtu na kama KAFA wakawa na sababu nyingine yakutojisikia vibaya kwa kujiaminisha  kwanza MWIZI  alijitakia mwenyewe kwa kuiba na kwa hilo MAREHEMU alikuwa hana UTU.:-(



Swali:
  • AU?

Ndio,...
... karibu kitu chochote KINACHOKUTISHA ukijiandaa nacho KISAIKOLOJIA ,...
... yasemekana utafanikiwa KUKIONDOA MTISHO kwa staili hii hii   WATU WAITUMIAYO kujilinda kisaikolojia wakati WANAMPIGA MWIZI ,...
....cha KIFIKIRA kubadili tafsiri ya KITENDO wanachofanya ,...


... kwa hiyo unaweza :

  •  Kama ni MUISLAMU  uko baa -  ukaita nyama ya NGURUWE kitimoto ili uigide vizuri bila kujisikia ulacho ni HARAMU kwa kuwa  wakati unailenga KUING'ATA  ukaruka kufikiria huyo ni NGURUWE na kwa tafsiri  YA KISAIKOLOJIA  YA AKILI vilevile hiyo sio  nyama ya nguruwe kwa kuwa ni bonge la kitimoto   kwa kachumbari na ndizi za kuchoma pembeni ya BIA na sio pombe!

  • Unaweza kumkabili  ADUI yako  kwa kumfananisha na mtu unayemjua  ambaye umeshawahi kumsuta na kutafsiri KITENDO unachofanya kama sio kukabili mtu  labda  kwa kukifanya kiwe tu  ni chakutaka kujua  `` HIVI kwa nini UNANICHUKIA BILA SABABU?´´ hata  kama washuhudiao waonacho ni mipasho na  usemacho ni ``NIKOME BABU wee MIE SILI KWAKO!´´



  • Kumuweka kona BOSI wako unayemtamani kimapenzi  AMBAYE KWA KAWAIDA  unamuogopa  -kwa kumfananisha  kimuandao na MALAYA wako - na  unaweza kujikuta  umemtongoza hata kwa nguvu ya gia yako  uliyoizoea  uiitayo `` KIUTANITANI TU!´´ kwa kuwa wewe mara nyingi kwa wale uwaogopao utumiacho  kulainisha kuongea nao huwa ni UTANI. Kitu kifanyacho kumuingia bosi wako siku hiyo ya mashambulizi ya kauli unamgeuza kuwa huyo ni MTANI na wala sio BOSI wako kwa hiyo unafanya kama utani kuandaa A B C za aisee nakupenda ! INGAWA BADO  kuna uwezekano  ukishindwa mashambulizi waweza kujikuta umefukuzwa kazi kwa KUMKOSEA HESHIMA BOSI wako.:-(.

Swali:
  • SI  moja ya kitu ambacho tunaweza kujifunza pia  kutoka APIGWAVYO MWIZI  ni kuwa kila mtu ana bahati yake - kwa kuwa kuna MWIZI  mwingine  mdundo kidogo anakufa halafu mwingine anabwengwa kisawasawa na kuchomwa mpaka na matairi ya gari lakini  bado tu anadunda na labda kutokana na hali ngumu ya maisha yake ATAIBA TENA TU  akishapona?



Ndio,...
... wote tunajua  katika nchi zetu hasa za AFRIKA waibao kidogo ndio chamoto wanakiona zaidi kwa kuwa,..
... kinamna labda wale WEZI wakubwa  bado kwa WAIBIAO walivyoiba vyachangia kuwatafsiri kwa wanyonge kama WAHESHIMIWA  katika JAMII,...


....lakini labda moja ya DAWA  tujifunzayo kutoka katika kupiga VIBAKA WADOGO WADOGO,...


...moja wapo ni jinsi tunavyowatafsiri katika JAMII,..
.... kwa kuanza kwa kuwaona HAWASTAHILI HESHIMA na sio WAHESHIMIWA na  kwa kuwa wameiba hao HAWANA utu,...


.... kitu kifanyacho  BONGO mwizi mdogomdogo akipigwa mpaka akauawa ,...
.... wengi wa watu hawaoni TATIZO hapo,...


..... ingawa ukitukana  mwizi mkubwa FISADI kwa kuwa anaweza kuwa kitafsiri  za watu bado watu huyo kwao ni MUHESHIMIWA,...
... hata KUMSONYA aka ukimfyonza tu hadharani kuna mpaka WAZEE WA MJI watakao kuombea   ULAANIWE kwa  utovu wa nidhamu kwa kumfyonza MHESHIMIWA!:-(


MWISHO wa SOMO!

Swali:
  •  Hivi unafikiri ni mangapi TANZANIA yangekuwa bomba sasa hivi kama kitafsiri na juhudi ingewezekana kuwafanya watu wapende kuyafanya kama wafanyavyo kwa bidii ngono?
  • Lakini hufikirii moja ya sababu ni vigumu kukabiliana na mengi tu akumbananayo BINADAMU hutokana na ni nini tu BINADAMU  anakitafsiri  kitendo cha kukabili kitu, kitu kiwezacho kufanya  baadhi ya watu waliosoma KIINGEREZA wakashindwa KUMGAMBIRA INAFU  MUINGEREZA kisa wanafikiri  kusema ``HAPANA  aka NO au tu IMETOSHA ´´  katika hatua za kukabili wanafikiria ni MPAKA ujue kuongea KIINGEREZA?

Ndio,...
.....tafsiri MUKICHWA ya kitendo ufanyacho,...
.... inaweza PIA  ikawa ndio sababu UNAUMIA KWELI KAZINI   ila umeridhika na kazi  kwa kuwa hicho wewe umekitafsiri ni ``KUFANYA KAZI kwa BIDII!´´ .:-(

NI WAZO tu hili MHESHIMIWA!:-(

Na hebu Aurelio Martinez aingizie staili ya muziki ya aina ya GARIFUNA katika - Tio Sam




Aurelio Martinez aendelee kwa - Lubara Wanwa




Au tu Ballet Garifuna watukumbushe kuwa UAFRIKA haujakufa HONDURAS ambako mkuu AURELIO ndio anatokea katika :

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 12:46 pm  

WAZO JEMA MKUU,...NAWAZA TU, Hivi kweli kama wizi ungelikuwa kupigwa kama adhabu kama tuwafanyavyo vibaka, wakituibia simu zetu, kuna mtu angelibakia hai hapa Tanzania!
Nakumbuka mmoa wa mabosi wangu kwenye kampuni niliyowahi kufanyia kazi alisema, amegundua kuwa Watanzania wengi ni wezi, kwani mshahara wanaopata hawawezi kuishi...ni mdogo sana, je inakuwaje mtu atumie laki tano kwa mwezi wakati mshahara wake ni lakini mbili na nusu, hela nyingine kapatia wapi?
Sasa ina maana sote tungechomwa moto, sote tungepigwa kipigo cha kibaka...
Kihaulalai hata mimi ninayeoba muda wa ofisi kuosma maili zako mkuu ninastahili kupata kipigo cha kibaka...naiba muda wa ofisi
Ni tafakari ya wazo lako mkuu!

Goodman Manyanya Phiri 1:18 pm  

Sisi kwetu Afrika Kusini ni aibu kumla nyani. Lakini watu kadhaa wanakula tu.


Sasa kwakuwa nyani ni "IMFENE" kwa Kiswahili cha kwetu kikubwa (Kizulu), basi mlaji atatupilia mbali neno "IMFENE" nakusema [mimi nakula [mnandapolile]/"COOL-THE-DISH-DOWN-BEFORE-INGESTION"].

Hata Wazungu wanaokula nyama ya binadamu hawakubali wamemla mtu, bali [wamekula 'nguruwe mrefu'/ LONG PIG]. Na miaka kama mitano iliyepita hapa kwetu alikamatwa mswahili-mwenzetu huko Kwazulu-Natal aliyempika na kumla mwana-mama mmoja mlevi. Mpaka leo bado yuko jela lakini sidhani anaelewa kosa lake haswa ndio nini... je, ni kosa kula nyama????

MAANA YAKE YOTE NINI?

Jamii za binadamu kote haziko katika ukweli wa mambo halisi; bali zimejengwa juu ya fikra tu za sisi binadamu, kukujibu, MWALIMU KITURURU MWENYE-SOMO-KUUWA-MWIZI

Rachel Siwa 4:25 pm  

mmmhh hii kiboko,Kwakweli asilimia kubwa hao wanaompiga kibaka nao wezi kwanamna moja au nyingine!!!@emu-three tukianza kuchomana moto nawe umo kwa kuiibia ofisi hahhahaaa.Naunga mkono hapo kwakufanya kazi ngumu au ya mateso lakini kujiona mchapa kazi au kazi kwa bidii!@kaka Kitururu umewaza sana hapo!.

Christian Bwaya 4:45 pm  

Hii elimu sikuitegemea. Nashukuru kuipata bila malipo.

Simon Kitururu 5:35 pm  

@M3: Nahisi angebakia yule wa mwisho kabisa kupiga mtu!:-)

Ni kweli ,..
... rafiki yangu alisema BONGO ndio nchi ambayo unaweza kukuta mtu ana si mu ya ghali na bili ya simu ghali kuliko uwezo wa mshahara wake na bado anakula analipa kodi na katika kitimoto yumo na KANISANI/msikiti nako yumo!

BONGO kiboko!

@Mkuu GOODMAN: Si ndio hapooo! BINADAMU mambo zake wee acha wee.

Na utashangaa kuwa hata maswala ya KINYAA na MIIKO ni yakujifunza tu ndio maana unaweza kukuta ukichunguza kuanzia PAKA, nyoka , na kila kitu watu wakiweka mawazo kimkao fulani wanakula tu!

Ila wanao enda mpaka kwenye LONG PIG nao DUH!:-(

By the way nilibahatika kuonja nyama ya NYANI kutoka kwa marafiki zangu wa KIKONGO na nafikiri kilichokuwa kinanisitisha kidogo kumgida kisawasawa kama wao ilikuwa ni KASUMBA tu za niliyokua nayo kwa kuwa kusema ukweli nyama yake ilikuwa inalika vyema tu ingawa tunajua maswala mengine ya chakula kinogeacho mtu utundu wake anao MPISHI!:-(

@Dada Rachel:

Kweli kabisa mambo mengine ni jinsi tunavyoyatafsiri kichwani ndio siri ya jinsi tuwezavyo kuyavumilia hata kwenye ndoa, au hata URAFIKI.

@Mkuu BWAYA:

Pamoja sana MKUU!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP