Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ile kitu ``Najua SIJUI!´´

>> Friday, February 04, 2011

MKAO wa MTU kujua HAJUI,...
..... labda ndio KUJUA huko kutakiwako.:-(

Na CHOCHOTE mtu afikiriacho ANAJUA hata kama hatuongelei hapa  BWIMBWI,...
.... siku akiamua kukiangalia UPYA kama mtu asiyejua hicho kidude,...
.... anaweza kukuta anastukia vitu vipya hata :

  • Katika ya WAZAZI wake achukuliao tu  kilaini kuwa ANAWAJUA kuna kitu hajui ambacho akijua kinaweza kumsaidia kitu hata kama sio kwanini ana bonge la matege.

  • Aweza kustukia  labda hajui sana kuhusu hata JUA na MWEZI ambavyo anaamini tu  hakuna cha zaidi cha kujua.
  • Aweza kustukia labda UGALI WA SEMBE wala haufuidafu  kwa wa DONA .
  • Ule aliokuwa anafikiri ni mwanya wa MPENZI ni pengo tu
  •   Au  aweza mpaka kustukia  MAMBO MADOGO MADOGO kama yale ya  kuwa  ni karibu  tu chupi AIPENDAYO  ILE YA SIKUKUU itaanza kuchanika na kuna umuhimu wa kununua mpya kama hataki  kutembea bila chupi mara mojamoja au kuvaa ya zamani  siku utokeapo uwezekano wa kumvulia mtu kificha nyeti huku akidadisi staili ya maringo ya uvuaji KWA KUWA KAOMBA kudeku miondoko!:-(

Swali:
  • Si unajua KUNAUWEZEKANO ukiamgalia HATA KIGANJA CHAKO ufikiriacho unakijua unaweza kustukia kinamistari  au tu kitu ambacho HUKUWAHI KUSTUKIA kwa kuwa tu unadhani KIGANJA CHAKO UNAKIJUA kwa kuwa unaridhika na kifanyavyo kazi ya kufinyanga MATONGE  ya Ugali?

Ndio,...
... najua SIJUI!:-(

Na samahani NAWAZA tu hapa MHESHIMIWA!:-(

Hebu tulisikilize TOTO Tundu Robert MUGABE tena likimwaga sera...



Tuendelee kucheza naye....



Hebu tulisikilize na TOTO tundu Muammar Gaddafi



Hebu tuendelee naye...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP