Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

``(TUSI la nguoni!) ´´-kwa aliyeanzisha kuhusisha UTAPELI na neno `` USANII´´ Bongo!

>> Monday, February 07, 2011

Kuna kipindi Tanzania  sanaa , Wasanii  na USANII,...

....viliheshimika!

SIKU hizi ukisikia mtu ni MSANII,...
... cha kwanza kinachokujia akilini ni kuwa labda jamaa TAPELI au  kuna kitu tu anauhusiano nacho ambacho kimemfanya afudhu kutoheshimika!:-(

Swali:
  • AU?

Ila,...
... taka usitake,...
... SANAA na USANII ni vitu MUHIMU sana katika JAMII yoyote ile,....
... na kitendo cha kuoanisha USANII , WASANII ,SANAA na UTAPELI au mambo mabaya  nchini TANZANIA,....
.... inaweza kuwa inaua moja ya KIOO cha JAMII ambacho ni SANAA za wananchi katika JAMII!




Swali:
Na kama unachangia  katika kupaka KIOO cha JAMII matope,.....
.... unafikiri JAMII itaonaje?


Na kama USANII na UTAPELI kwako vinalinganalingana TANZANIA,...
.... unafikiri JAMII ya TANZANIA iko katika hali gani?



Nilitaka  kusema ningependa WOTE walinganishao USANII na UTAPELI watoke usaha kwenye vishimo vyao vyote vya mwili,...
.... lakini ngojea niendelee kuwaza kwanza hili swala KIUNDANI ,...
.... kabla sijatukana zaidi ya NYOKO mtu!:-(



NAWAZA tu kwa SAUTI HAPA Mheshimiwa!:-(



Hebu Mbaraka Mwinshehe arudie-Matusi Ya Nini?


Au tu Mbaraka Mwinshehe amalizie tu na -Ushamba Umekutoka

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 4:44 pm  

Hapo Dogo ume ongea,Neno Usanii kuhusiswa na utapeli.Nimewahi kumuuliza mwandishi mmoja maarufu, katika blog yake aligusia neno hil la usanii kam a utapeli, kwa kweli sikupata jibu alikuwa na maana gani jinsi alivyo litumia kwenye maandiko yake.tusikie wengine wana semaje. nihayo tu,kaka s.

Simon Kitururu 5:15 pm  

@Kakak S: Mie nimechoka na jinsi USANII na WASANII wanavyodharauliwa BONGO ! Na siku hizi na BONGO FLEVA basi ndio kabisa USANII unaonekana kama vile ni vitu fulani tu ambavyo.....


NAAACHA lakini naamini KAKA S unanielewa!

Halafu asante kwa kunitembelea hapa! Kwakuwa sijawahi kuona KOMMENTI yako kijiweni kwangu! Karibu sana KAKA S!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP