Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama AFRIKA ni MALAYA na bado kuna wakataliwao kugawiwa MALIGHAFI !:-(

>> Friday, February 11, 2011

[ Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]

 Kwa wale ambao wamewahi KUKATALIWA  na MALAYA asifikaye kwa kugawa kama pipi chachu wanajua:



Sifa tulizozoea, MALAYA ni mgawaji
Nalohatukuzoea,huchagua ugawaji
Kuna anaowagea, naanyimao gawaji
AFRIKA ka' malaya, wagawiwa gawaji?




Sasa hivi kuna wenye ngekewa tu ndio waponaji wakati tunasikia :



Anajulikana sana, kwa kugawa MALIGHAFI
Chakusikitisha sana, wenyeji  wala tu  GHAFI
Utajiri wake sana, wanao kina GADAFI
Viongozi  AFRIKA , na wale wa  nje  ya bara.


Na kwetu tusiogewa, ni macho tu twatolea?
Twaona anavyoliwa, na tafrija twalea?
Kama vile twagawiwa, makombo yawe mbolea?
Lakini je AFRIKA, ni MALAYA mgawaji?




Na hebu  turudie kuangalia swala tena kuhusu AFRIKA :

Kama sio mgawaji,kuna wajigawiao
Kama chungu chenye maji,kuna wajichoteao
Wenye kichotea maji,ndio kiu wakatao
Wale wenye AFRIKA,SI twasubiri mgao?


Na labda :


Mgao hautakuja, Malaya ni MCHAGUZI 
Afeva waliokuja, na nyenzo za nguvu kazi
Na tupo tunaongoja,bila kufanyiakazi
Wafikiri tutagewa, vya bure  tu bila kazi?




Mwisho wa kamanyola bila jasho!:-(



Swali:
  • Umekumbuka kuifikiria AFRIKA leo na kama unapata shea yako ya TITI LA MAMA huyu wengine wamuitao MAMA  AFRIKA?
  • SI unajua nawaza tu hapa na nasikia kuwaza saa nyingine eti husaidia kupata jibu ingawa hakuna garantii?


NI WAZO TU HILI JEMADARI na wala USINUNE BASI kama kwa zigizaga zake UMECHEUA!:-(
Cheka basi kidogo eeh MWANAKWETU hatakama hatuelewani!:-)
AU?




NA  NAWATAKIENI WOTE ,...
....Ijumaa ,...
.....na WIKIENDI njema,....
......WAHESHIMIWA!






Hebu tu turudi Afrika upande wa chini kidogo tukutane na Sipho Gumede arudishe busara kwa -When Days Are Dark, Friends Are Few






Au tu Jimmy Dludlu arudie tu na -Tote

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 3:47 pm  

Mkuu, ...kila nikiandika mtandao unagoma....!
Basi nitaandika chochote j3...wikiendi njeeeeeema!

Yasinta Ngonyani 6:13 pm  

sisemi kitu leo!

Simon Kitururu 6:15 pm  

@M3: Tuko pamoja!

@Mtoto mzuri Yasinta: Nahisi kunakitu umesema!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP