Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA kuna mambo mengi TU ambayo ni STAREHE TU kwa wasio HUSIKA!:-(

>> Monday, February 07, 2011

Kuna mambo ni apigaye chabo kwa pembeni ,...
... ndiye mwenye cha KUCHEKELEA,...
... ndio maana kuna ambao  labda mpaka waonjewe MKE,....
..... ndio watastukia machungu ya aumiaye roho kwa kuwa anaonjewa MUME na  mdada wa nyumba ya jirani!:-(


Na labda kabla MTU hajasikia njaa wakati  hana uwezo wa kupata CHAKULA labda stori za huruma  kwa  waokotao MAKOMBO majalalani bado ni stori tu za aliye kwenye kitu  PEMBENI,...
..... kwa kuwa ni mpaka afikie kuona  jalalani  kunukako KIMAVIMAVI kuna bonge la msosi ufaaokuliwa ndipo  kisawasa tu anaweza kuelewa hata ya ambaye hajaenda majalalani bado YULE  mwenye NJAA na  mla MAKOMBO ya jirani.:-(

Swali:

  • Si inasemekana   ni rahisi kuhudhuria misiba ya wengine ambako  kirahisi UKACHEKELEA KITU ingawa wahusika WANALILIA mambo au tu kuangalia wafao kwenye TV kuliko mtu kufiwa yeye mwenyewe na swala liko katika ya YA MTU na sio pembeni?



Ndio,...
.... kuna mambo  wewe mwenyewe ukiwa ndio MUHUSIKA,...
.... ndio utajua KISAWASAWA  ni  nini JOTO LA JIWE,...
.... hata kama  KUNA watu hukazia KWA KAWAIDA matamu ya kuwa MUHUSIKA kwa kuwa  ni MUHUSIKA pia NDIYE isemekanaye  NDIYE ajuaye vizuri tamutamu HATA ya KINUKA MKOJO   hata kwenye ngono pia ,...
... NA KUFANYA wasiohusika  wafikiriaye  KWA KUWA ANANUKA KIMKOJOMKOJO harufu ya mkojo na UTAMU  DHAIFU  vinauhusiano  KUWA  katika MTIHANI wamepata ZERO kinamna,...
....kwa kuwa  kwenye ndoa yenye baraka za SHEKHE  yenye ANUKIAYE PAFYUMU mpaka kwenye kipengele kitumikacho KUKOJOLEA bado inaweza ikawa sio moja ya siri ya  maeneoyake ni HARUFU NZURI aka utuli katika UTAMU!:-(


Swali:
  • SI unajua  si kila mtu achukiaye hata  harufu ya MKOJO uliovunda?

NI WAZO tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu tumpate DIEYNA katika -Bes bi sa bessa




Au tu DIEYNA aweke kiwanjani na -Jaapalé

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 1:36 pm  

Kampyuta zetu (yaani ubongo) hazifanani kabisa Bw Kitururu. Hata hiyohiyo kampyuta moja inaweza ikashughulika na APPLICATION fulani asubuhi, na INPUT zikafaa kabisa. Leta hizohizo INPUT jioni wakati APPLICATION imebadilika na unaambiwa kampyuta yako imeathirika na virusi (VIRUSES).


Wewe ukitaka kuniwudhi mimi niambie nifumbe macho na huku uniletee yai uliepika kisirisiri au uniletee CHEESE na kuniambia ninuse. Nitakwambia 'mchezo wako mbaya [umemjambia]'.

Lakini ninapofumbua macho na kuona kwamba 'kinachonuka' nichakula, NITAKUSHUKURU SANA NA PAPOHAPO kuanza kuutwanga ugali kwa mboga hiyo ambao sekunde chache niliekuwa nadai INANUKA!!

Sasa hainuki tena; bali INANUKIA!!!

Simon Kitururu 2:31 pm  

@Mkuu Goodma: DUH! Yani weye mpaka uone ndio uhakikishe kuwa yai ni YAI?

Yasinta Ngonyani 3:18 pm  

Kaaazi kwelikweli:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP