Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati ni ya DUNIANI yadhaniwayo ndiyo BINADAMU huyajua,...

>> Wednesday, February 23, 2011

.....lakini labda ni ya MBINGUNI ya kiimani   ambayo kwa imani BINADAMU ndiyo awezayo vizuri kiimani KUYAJUA!Swali:
  • Kwani si inajulikana ni vigumu kwa BINADAMU hasa yadhaniwayo ni ya KIDUNIA yajulikanayo  kwa BINADAMU kuyajua?

  • Unauhakika unamjua hata mtu mmoja ambaye ni yote yajulikanayo ni ya KIDUNIA ambayo anayajua?


NDIO,...
.... labda kwa kuwa ya MBINGUNI huoanishwa na IMANI ,....
... labda kwa imani BINADAMU  anaweza kujua ya MBINGUNI kuliko ya DUNIANI  hasa kwa kuwa labda swala zima la KUJUA VITU kiimani lahitaji tu  KIIMANI uamini UNAJUA kitu kifanyacho WAKRISTO, wamfuatao BUDDHA mpaka WAISLAMU wote watofautiane KIIMANI kwa kuwa tu kuna kitu wote wanaamini WANAJUA.:-(


Naendelea kuwaza....:-(

Hebu SEAL aingilie kati kwa-This could be HEAVENSEAL  aendelee kwa - Lost My FaithAu tu amalizie na-Kiss From A Rose

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:46 am  

si jambo baya kuwaza:-) IMANI!!!

SIMON KITURURU 10:09 am  

@Yasinta: Kuwaza kwa sauti LAKINI labda ni kitambulisho kwa watu kunaasilimia ngapi katika kichwa cha MUWAZAJI za UJINGA!:-(

Yasinta Ngonyani 1:53 pm  

Sijawahi kusikia kama kuna watu katika dunia hii wanawaza ki-ujinga au wanawaza ki-busara. Kwani naamini katika dunia hii hakuna mjinga na hakuna mwenye busara. Pia hakuna kilichokuwa sawa na kichokuwa sawa..

SIMON KITURURU 2:55 pm  

@Yasinta: Mie nimeshawahi kusikia!


Na nasikia kuna UJINGA ndio maana kuna waaminikao ndio wenye BUSARA. Na nasikia kuna visivyo sawa na ndio kisa kuna wapendao kukosoa wenzao DUNIANI!:-(

Swahili na Waswahili 9:11 pm  

Hakuna binadamu awezaye yote na ajuaye yote,ukiona wewe unajua/unawaza hili kumbe mimi naweza nisilijue/nisiwaze hivyo!

hata imani mimi naamini Mungu yupo mwingine akaamini ni ubabaishaji tuu!

lakini ana Imani yake,anamawazo yake na ujuaji wake!

na hakuna asiye na mawazo yawe mazuri au mabaya kwa mtazamo wangu,lakini yeye anayapigia mstari!kwa sababu zake.

Nimewaza tuu na nasubiri kujifunza zaidi!

SIMON KITURURU 9:24 pm  

@Da Rachel:Mie kwa mawazo yangu naona kama wewe umemaliza kabisa kwa komenti yako.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP