NDIO, labda YULE ,wewe , kama tu MIMI ni MZURI kwa baadhi tu ya WATU!:-(
>> Tuesday, February 08, 2011
Na haki ya nani ,...
.... kwa kuwa wewe ni MBAYA kwa BAADHI tu ya watu,...
... kuna uwezekano ni katika MACHAGUZI YAKO ya vinono kama MIMI ,...
.... ndipo uwezapo kujikuta umekutana na wasiochangamshwa DAMU na UZURI wako!:-(
Swali:
- Si unajua LAKINI uzuri wa MTU na UBAYA wa SURA au SEHEMU za SIRI za mtu labda wala huwa si muhimu kama wakati huo WATU wana njaa na cha muhimu NI CHAKULA na sio watu wanavutiaje KIMUONEKANO?
- Na si tunakumbuka uzuri na UBAYA wa mtu sio uko tu katika YAONEKANAYO TU?:-(
Ndio,...
... kama wewe umeanza kufikiria hutaki kushea SINIA la BWIMBWI na mtu kwa kuwa hupendi muonekano wake kwa kuwa mchafu na ana PUA kama MATAKO ,...
... kuna uwezekano kabisa wewe umeshaanza KUSHIBA na UMUHIMU wa CHAKULA umepungua!:-(
Ndio,...
... inasemekana mwenye shida ya CHUPI hutafuta tu yoyote na ikibidi hata ile ya kufunga na kamba za migomba ili mradi ishikilie MAENO yenye mpaka matako,....... na mchaguaye chupi kwa RANGI au tu kwa kuwa haijakaa kiguniagunia KIMSIKILIZO WA NGOZI kuna uwezekano huyo hana shida sana na KIFICHA nyeti aka CHUPI au tu umuhimu wake KIFAA hicho UMEPUNGUA.:-(
NI WAZO TU HILI mkweche MHESHIMIWA na wala USIKONDE Jemadari!:-(
Hebu MANU CHAO arudie-Bongo Bong na Je ne t'aime plus
Manu CHAO aendelee kwa -Me gustas tu
Basi BWANA ngojea adinye tu na-Desaparecido
Hebu ahojiwe basi
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hivi kuna mtu `mbaya' wa sura, na ni kigezo gani cha `sura mbaya, maana watu kama marehemu Ongala, alidai mwenyewe kuwa ana sura mbaya hata kuingia mashindano ya sura mbaya, lakini mzungu waake alimuona bonge la chombo!
Ubaya wa sura ni wa mtu mwenyewe, kipenda roho hula nyama mbichi! NI WAZO TU MKUU:
`Ufuma Kiruru, kana vusangi?'
@M3: Mmmh!
@emu-three
Kama kawaida yake huyo mtoto wa Kitururu, anaongelea maswala mazito sana.
Tatizo ni kwamba wengi hatumwelewi kutokana na kwamba tunashikilia mno mifano ile anayotutolea.
Kosa lakini haliko kwake; kosa kwetu nikule kutochunguza undani zaidi wa ule mfano wachupi.... a nami nisije nikaeleweka vibaya!
Nitaacha chupi na badala yake nichukulie mfano wa “kitanda cha Mhindi” (Si unaambiwa Mhindi mmoja alitakiwa amalizie msemo waKiswahili: “Ukitaka cha uvunguni….?” naye akajibu “…inua tanda!” badala ya kusema “…sharti uiname!”
Turudie basi katika ???mjadala??? (DEBATE) ya Ndugu Kitururu hapa. Kila takwa duniani linatokana na hitaji fulani na yote, yakiwa matakwa kwa hayo mahitaji yamo yote katika mawazo ya mtu. Yote yakiwa mawazoni ya mtu amini usiamini unaweza kisayansi KUYAWEKA JUU YA MIZANI NA KUPATA UZITO WAKE!
Kwahiyo:
Wazo la "cha uvunguni" linao uzito wake tuseme kwa mfano liko upande wa kulia katika mizani yetu ya ubongo.
Wazo la "kunyanyua kitanda cha Mhindi liko kushoto ya mizani"
Na sasa ndugu yetu (Kitururu) mwenye takwa la "cha uvunguni" anatafakari "ninyanyuwe kitanda chaMhindi nisinyanyuwe?" (Mawazo kama hayo yalimfikia Jacob Zuma siku moja nyumbani mwake zamani ya kale na "cha uvunguni" ilikuwa kufanya mapenzi na bibi mmoja wakati "kunyanyuwa kitanda" kwake ilikuwa mahabarisho aliyekuwa nayo tayari kwamba 1. dada alikuwa na virusi vya ukimwi 2. hamna soksi mule ndani ya nyumba yake).
Sitaki kukaa zaidi kwaRaisi wangu; nitakung'utwa bure nikiwa peke yangu hapa Afrika Kusini. Haidhulu nirejee kwake Simon Kitururu nimwombe aniruhusu! Naye kwake wazo la kupata cha uvunguni likiwa ndilo nzito basi atanyanyuwa kitanda hicho cha Mhindi!
Lakini (labda kutokana na uvivu wake) ikiwa wazo la kunyanyuwa kitanda ndilo nzito kuliko matakwa yake juu ya cha uvunguni Bwana Kitururu atakwambia: "Kwanini nijikwanue mabega na kunyanyuwa vitanda hovyo?"
emu-three, Rafiki yangu, panapokuwa wewe unatupiga chenga ni pale pale unapodai eti [mbaya wa sura hayupo]!
Mi nakwambia Wapo Tu!!! Tena wengi sana ukizingatia kwamba hata mimi “Manyanya yaliyooza” nimo kati yao!
Haya basi: Simon Kitururu na Kitanda Chake Tena! (Nakwepa kusema "na Chupi Yake").
Kama Simon angelikuwa mvulana wa umri 16 na "cha uvunguni" ilikuwa kitabu chake cha saikolojia aliyeamuriwa namama yake "lazima kijana ukitowe pale uvunguni kabla ya saa kumi nambili jioni hii ninaporudi kazini", atakaposhindwa kukipata hicho cha uvunguni huyo Simon atashindwa kutokana na UVIVU wake wala siyo kutokana na kwamba "hamna cha uvunguni'!
Au nikuulize Rafiki yangu, emu-three: Kwanini tunapata mashindano ya warembo na hatujawahi kumwona hata mmoja mrembo [mwenye pua kama matako] anaitawala dunia?
Sijui kama nilichelewa wapi huku, kumbe nilikuwa naulizwa swali kuhusiana `ubaya wa sura' Uzuri na ubaya wa sura ni kutokana na `uonaji wa mtu, kwani hata huyu anayeambiwa kashinda ubingwa wa urembo wa dunia kuna ambao wanamkataa na kusema `kapendelewa' kwanini, kwasababu wengine hawauoni huo uzuru unaotajwa!
Na huyo unayemuona ana sura mbaya , mbona anamuoa `mrembo wa dunia' kwanini kwasababu ana uzuriu ambao mimi na wewe tunaosema ana sura mbaya hatuuoni!
Ndio hilo tu mkuu na rafiki Goodman kutoka `bondeni'
Post a Comment