Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BINADAMU HARIDHIKI - na akifanikisha HIKI ataanzisha KILE!

>> Wednesday, February 16, 2011

Na labda moja ya kifanyacho MAISHA ya mtu yalete maana,...
... ni kwa MTU kila wakati MAISHANI  kuwa katika mchakamchaka wa kiana ya kuhangaikia tu kitu FULANI!:

Na ndio maana ,....
.... utakuta aliyetaka mke mzuri AKIPATA mke mzuri LABDA  ataanza kufikiria labda ingekuwa bomba zaidi angekuwa na MKE mwenye MIAKILI kedekede  hata kama  kwa mitazamo ya wahukumuo mionekano ya watu MKE HUYO ATAKUWA  ana sura kama sehemu za nyuma za KINYEO CHA  nguruwe ambazo wanaamini hazina sura nzuri  katika CHATI ZAO fulani.:-(

Na ndio maana,...
...... kuna wasomeao UDAKTARI kwa nia ya kutibu wagonjwa na wakishakuwa MADAKTARI  hustukia hawaridhishwi na wito huo na kuamua afadhali wawe WABUNGE  wa majimbo FULANI.:-(

Kwa ujumla  LABDA ndio MAANA,...
....MTU akihangaikia kitu  - muhangaiko huo ni moja ya KIJAZAYO ya mahitaji ya BINADAMU kujisikia kuna kitu kinajaza UTUPU uwezao kuwepo MAISHANI - kitu ambacho akifanikisha hicho inabidi aanzishe kitu kingine ili asijae UTUPU MAISHANI - na ndio labda kifanyacho kuna watu wakishapata MUME fulani  maisha huanza kuboa na inabidi  waibie na pembeni  kwa WAUME wengine hata wa SHOGA WA NYUMBA YA JIRANI ili tu angalau kujazia MATUPU hata wasiyoyajua ni yapi KWA UHAKIKA  yaletwayo na KUOLEWA na limtu ambalo wameshalizoea SASA  na kujua ni lao lotelote  ambalo kwa kitendo cha KUOLEWA NALO maishani kimepungua baadhi ya meno KIKUNA KIPELE  na kusababisha kuwashwa kusiishe kabisa  kama mkunaji ni YULEYULE mwenye YALEYALE yatabirikayo katika matibabu ya KUWASHWA kwa KIPELE fulani:-(

Swali:
  • Unafikiri kama MBINGUNI ni mahali fulani na BINADAMU akiachiwa kiroho papo kama alichonacho DUNIANI  - hakuna ambao hawatapaona MBINGUNI kunaboa ikizingatiwa  inasemekana mengi wapendayo na kuridhika nayo BINADAMU duniani huhusianishwa na ya SHETANI kwa hiyo labda SHETANI ndio mjanja wakunogesha wanadamu?
  • Mkuu hivi umewahi KURIDHIKA na baada ya kuridhika  na kitu ilikuchukua muda gani kujikuta unahangaika na kitu kingine ambacho labda hakikuwa na umuhimu wakati unahangaika na na ulichofanikiwa tu KURIDHIKA nacho muda sio mrefu?

Ndio,...
... labda BINADAMU haridhiki,...
... ndio maana  kila siku ni MCHAKAMCHAKA na  ukimpa chipsi mayai anaweza kulalamika mbona CHIPSI DUME hakuna ile yenye KACHUMBARI,...
... na ukimlisha WALI  anaweza kudai  kwanini analishwa vyakula vya NDEGE na sio UGALI aka NGUNA ya NGUVU ambayo rijali hudai akipiga hilo KWA SAMAKI SAFI wa NGURUKA halafu akaingia kazini,...
.....mtu atapata tu mimba siku hiyo.:-(NIMEACHA!
Na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu tu tubaki hapahapa Afrika KUSINI ili  BLACK COFFEE aingilie kati kwa-Even ThoughAu tu BLACK COFFEE amalizie tu kwa -Come to Me


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 2:24 pm  

Hapo umenena kabisa!

Na ndio maana yapo matatizo makubwa kufikiria "Mbinguni" kama "sehemu fulani katika Jiografia".


Mimi, Mkuu, nafikiri "Mbinguni" ni hali tu yenye kuridhika kiroho mtu akiwa hai au akiwa amekwishakufa maana yake roho ya mtu sidhani inakufa.Kuja basi katika swali lako barabara.

Nimekuwa mwandishi tangu utotoni, bado naridhika na nafurahia kwandika hadi leo hii na ndio maana nimejiunga na Blogi ya Mkuu Kitururu.

Wakati huohuo ningali mtoto, nilikuwa pia mwimbaji mzuri wa kwaya shuleni, kanisani kotekote.


Lakini sauti yangu iliharibika hapo baadaye nilipofika umri wa miaka 15 na nikaacha kuimba. Shangwe na makofi kupigiwa na wasichana kwa wavulana vikaadimika.


Nafikiri nilipojiunga na jeshi mwaka huohuo ilikuwa basi ndiyo namna yangu ya kuokoa mishangilio kwangu kama zamani. Mpaka leo sijuti hata kamwe tendo lakuingia jeshini, pamoja na mateso yake yote kwa maisha yangu binafsi.


Pamoja na hayo yote niliyekuwa nayakimbiza na kuyafanikisha maishani mwangu, nilikuwa (muda mzima wa miaka 35)bado nakumbuka enzi za utoto wangu nilipokuwa katika mambo ya muziki.

Kwahiyo, wakati watu hapo juzi walipokuwa wanafurahia VALENTINE'S DAY mke wangu yeye alinivumilia kupata mafunzo yangu ya kwanza kupiga GUITAR.

Siku iliyefuata nilijinunulia 'WASHBURN' yangu binafsi ya kwanza (mwaka juzi nilimnunulia Binti Phiri[17] na kumpelekea huko Iringa).

Lakini leo, kama ninavyoandika hapa: najisikia niko mbinguni kabisa kwani mwalimu wangu wa GUITAR keshaichunguza hiyo 'WASHBURN' na anasema sikupoteza kabisa hiyo laki moja na nusu (kwa kiwango cha Tsh.)Bwana Kitururu, kama huko kujiona au kuota mzee kama mimi[50] nitakuwa mpiga-GUITAR maarufu baada tu ya miaka mitatu "NDIO ISHARA BINADAMU HARIDHIKI" sidhani.

Mimi nafikiri ni ishara kwamba hata nikizeeka kimwili, sitaki kuzeesha akili yangu sambamba na huo mwili.

Naipa akili yangu CHALLENGE kila wakati.
Lakini katika suali lako, Mkuu, hukuishia hapo tu; bali uligusia hata mambo ya tamaa.

Hiyo ikiwa na maana eti 'kwakuwa mshahara wangu hautoshi basi nikaibe pesa za watu';

Ikiwa na maana 'kwakuwa eti mke wangu huyo mzuri nimekwishampata niende sasa nikaonjaonje hata huko kwa majirani zangu';

Hayo yote ni mauwaji ya akili, uchafuzi wa dhamira, pia 'uvunjaji' wa roho na huku mtu huyo akijiathili vibaya yeye mwenyewe!

Ni jela au aina yoyote ile ingine ya jehanamu, kwa maoni yangu: uma au binadamu wenzio watakuja kukushughulukia tu kwa namna moja au ingine ikiwa kumbe wewe ni mtu mwenye tamaa kama hizo! Na unastahili kwenda tu!Kwa hiyo tunapoangalia suala hilo, Mkuu, tuwe waangalifu: Iko mizani ya kupimia ndoto (AMBITIONS) nyingi za mtu na hizo ndoto ni halali kabisa.


Heshima zote kwako, Mkuu (Na asante kwa suali lako la kuvutia). Hatuwezi lakini kutumia mizani hiyohiyo ya wachapakazi ili tupimie uchu na tamaa hizo za kijingajinga kama nilivyojitahidi kuvitaja hapo juu.

SIMON KITURURU 2:50 pm  

@Mkuu Goodman: Nomekusoma na umeniwazisha sana na kipengele hiki cha maoni yako:


-``Kwa hiyo tunapoangalia suala hilo, Mkuu, tuwe waangalifu: Iko mizani ya kupimia ndoto (AMBITIONS) nyingi za mtu na hizo ndoto ni halali kabisa.


Heshima zote kwako, Mkuu (Na asante kwa suali lako la kuvutia). Hatuwezi lakini kutumia mizani hiyohiyo ya wachapakazi ili tupimie uchu na tamaa hizo za kijingajinga kama nilivyojitahidi kuvitaja hapo juu.´´-Mwisho wa nukuuu.

Naendelea kuwaza!:-(

Swahili na Waswahili 6:17 pm  

Usiwaze @kaka Kituru hatua moja ndiyo mwanzo wa mwendo,hata mtoto anasimama dede ndiyo atembee!

lakini hiyo ya kuonja mke/mume wa mtu mmhhh huo wizi sasa!!

kunakutoridhika kwa maendeleo nakuna roho mbaya,wivu,tamaa!.

SIMON KITURURU 6:25 pm  

@Da Rachel: Ni kweli mtoto anasimama dede ndio atembee!

Lakini sijui kwanini nahisi Mtoto akisha tembea labda baada ya kuridhika anajua kutembea ndipo hapo huanzisha kujifunza kutembea kwa Maringo ili mradi ni kitu kingine kaanza ili kujazia tu kitu .

Na nakubali pia kuna roho mbaya,wivu na tamaa,..
... ingawa labda navyo ni vitu wajaziavyo tu watu UTUPU fulani MAISHANI,...
... kwa kuwa naamini kwa aliye BIZE ,...
.... hata muda wa kugundua kutendea watu vitu kiroho mbaya, KUWA na WIVU au hata kugundua cha kuonea mtu tamaa unaweza kukosekana!

Na sijui kwanini NAENDELEA kuwaza DADA yangu!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP