Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI kuna wapendao KUONGOZWA au kuamuliwa tu mambo na kuna WAPENDAO KUONGOZA hata wasiyoyajua MAMBO!:-(

>> Tuesday, February 01, 2011

Labda kuna wakati  hata mie huwa NAHAMU ya kuambiwa nini la KUFANYA jambo,....
.... kitu ambacho chaweza kurahisisha mambo na hata kufanya WAKULAUMIWA isiwe ni mimi!:-(

Ndio,...
.....labda kuna ulaini wa KUTOJIAMULIA  na matokeo yake  kufuata ya wengine mambo,...
.... hasa kwa kuwa   matokeo ya KUAMUA KITU yanamchezo wa kuathiri na watu wengine ambao taka usitake kwa kuwa tuko katika JAMII MOJA - ya mmoja kinamna yatamgusa tu na mwingine hata kama sio mimi!:-(

Na labda moja ya ugumu wa KUONGOZA jambo na sio kufuata jambo,....
.... ni jinsi  aongozaye  maamuzi yake yanavyoathiri wengine ingawa chakusikitisha KUNA VIONGOZI ambao siku hizi hawajali waathirivyo wengine ukiniuliza mimi.:-(

Swali:
  • Hivi ukiangalia  yanayotokea kwa mfano Ivory COAST, Zimbabwe ,MISRI  hata kimakusudi nikiruka kutaja nchi nyingine hasa za  AFRIKA unafikiri viongozi wake wanajali ya wengine wanao waongoza?

Ndio,...
..... dunia ina UMIMI sana,...
.... na kufuata ya wengine ,..
.....kama tu KUFUATWA na wengine vyote vinaweza kuwa VINAUMIMI kwa kuwa ya wengine labda  HATUJALI kuliko yale tuyatafsirio kama YETU!:-(



Naendelea KUWAZA.....



Hebu tumsikilize kiongozi wa wengine mwaka 1994 alikuwa anasema nini...



Tujikumbushe tena....




Au tu The special warudie-GHOST TOWN

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP