Kwa kuwa MHESHIMIWA anatafuta MFANYAKAZI mzoefu wa usafi wa CHOO na kazi KIWANDANI lakini katika kutafuta MKE mwenye ya UKE anataka kuoa BIKIRA asiye MZOEFU wa kazi za NDOANI!:-(
>> Wednesday, February 23, 2011
UZOEFU ni sifa,....
.... kama tu ikitungiwa sababu za kwanini ni SIFA hasa kwa kuwa UZOEFU waweza kutafsiriwa kuwa ni UMALAYA kama VIGEZO na KITU vikioanishwa na KITU na VIGEZO vikaashiria dalili zote kwa kitambulikacho kwenye jamii kuwa MAZOEZI ya KITENDO na KUZOEA kitendo kwa asiye kwenye ndoa ni UMALAYA.
Uzoefu pia ni sifa,...
....kama kiongelewacho ni MAPISHI au ufuaji wa gwaguro kama tu udhaniwavyo umahiri wa kukata kiu kiufundi hamu ya CHAKULA SAFI cha USIKU kitolewacho na MUME kwenda kwa MKE wake katika JUHUDI za kujaribu kutomshindisha tu na njaa ya lawalawa za mchezo wa baba na mama MAMA WATOTO kutokana na MATATIZO YAWEZAYO kujitokeza - kutokana na kutopatia kitu - kutokana na kukosa uzoefu wa shughuli ambazo yajulikana kuna wengi mabingwa WA KUPATIA HILO huitwa MALAYA.:-(Na KUKOSA uzoefu ni SIFA,...
.... hasa kwenye baadhi ya jamii ambazo huamini kuna mambo ambayo mojawapo ni hamu ya kuamini USWAFI wa MTU dalili zake ni kukosa uzoefu wa kitu hasa kama mtu hataki kudhaniwa KWA KUJUA SANA sindimba ya kiuchiuchi ni MALAYA.:-(
Swali:
- AU?
Ndio ni kawaida kuulizwa UNAUZOEFU gani wa kazi kabla ya KUAJIRIWA,...
... ingawa kuna waaminio moja ya SIFA NZURI ni kutokuwa MZOEFU kama nia ni kuwa na uhakika na UCHUKUAYE wotewote ni aliyesafi KIBIKIRA na masomo umuanzishie mwenyewe ili afae kwenye yajayo faragha na KUOLEWA!:-(Na kwa kuwa twajua hata katika DARASA lisilo la FARAGHA kama la KILIMO cha GEZA ULOLE bado kuna ambao kufunza watu vizuri HAWAJABARIKIWA,...
....labda ndio maana KUNA watakaodai na kuwa na ushahidi kuwa labda BIKIRA hafai sana KUOLEWA!:-(
Na kwa hilo:
- Umegundua BINADAMU wafungwavyo na VIGEZO tu kutokana na waliyojitungia BINADAMU wenyewe?
- Na si umeshawahi kusikia BIKIRA akisifiwa ingawa kwa kuwa tu BIKIRA labda ni ushahidi yeye sio MZOEFU wa kazi nyingine wafanyazo wazoefu kabla ya KUOLEWA?
Natutoke kwenye UPUMBAVU huo hapo juu niliouandika na kuingia kwenye UJINGA:
Nia na madhumuni ya TARALILA hii ilikuwa ni kukumbushia ni kwanini swala la UZOEFU wa kitu laleta usumbufu na kama ni MWANAFUNZI unayemaliza tu MASOMO utagundua jinsi gani UZOEFU wa kazi waupavyo WAAJIRI kipaumbele kama vile wao wenyewe walikuwa WAZOEFU wa miaka MITANI mpaka KUMI katika kazi wakati wanaanza KAZI.
Na unaweza kukuta pamoja na MIAKILI YAKO DARASANI bado hiyo haitoshi kwa kuwa ni UZOEFU na UJUZI wa kazi ndio UNAHITAJIKA.
Na wakati tunaliangalia swala ki hivyo:
- Hufikirii labda hapa DUNIANI maisha ya ndoa yangekuwa bomba sana kama JAMII ingeruhusu kuwe na ndoa nyingi na ndoa ya kwanza iwe ni ya MAZOEZI tu ili kupata uzoefu ?
- Hivi mkuu bado unanisoma tu mpaka hapa wakati nishatoa tetesi labda huu ni UJINGA bin UPUMBAVU?:-(
Ndio,...
.... labda kila kitu HUTEGEMEA tu na vigezo,....
.....kwa kuwa labda UMUARUA wa kitu ni MURUA tu kwa kuwa umetungiwa SABABU!:-(
Naendelea KUWAZA !:-(
Na samahani NI WAZO TU hili ndani ya MAWAZO ambayo wengine siye KWA BAHATI MBAYA huwaza mpaka UPUMBAVU!:-(
Siku Njema!:-(
Na moja kwa moja ili tutoke kwenye wazo hili nyoko ngojea Sing The Truth wadinye -Four WOMEN
Au hebu NINA SIMONE arudie tu alivyodunga hiihii masantula ngoma ya mpwito-Four WOMEN
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
mmmmhhhh kaka jamani majaribio au uzoefu wa vitu vingine hapana,si vyote unaweza kujaribu unaweza jaribu Sumu!na vingine vizuri uvianze mwenyewe kwa kuepuka makombo au kuchakachuliwa kaka!.
Nami nimewaza tuu!.
@Dada Rachel: SI ndio hapooo!:-(
There's first time for everything ;-)...baada ya hapo sasa ndio unachagua kuwa mzoefu ama vipi...I like this another perspective ya "bikira" kama ile uliyoandika months ago...ni kama muendelezo..mwanzo ilikuwa mtu huja-experience kitu fulani...sasa uzoefu...ila kweli kama alivyosema hapo juu...vitu vingine sio vizuri kuanza...That's lyf!..I mean life. :-)
@Candy1: Mmmmmhhh!
Post a Comment