Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Na HAMU kweli ya kufanya DHAMBI leo, ILA namuogopa PADRE!:-(

>> Friday, February 11, 2011

NDIO,...
....labda kuna MAMBO mengi ,....
...... unaweza kukuta BINADAMU anakosea  wa KUMUOGOPA,...


.... na ndio maana  LABDA kuna waogopao WAZAZI watastukia wamemvulia  MTU nguo,....
..... kuliko waogopavyo labda WALIYEMVULIA nguo na kucheza pekupeku  labda ana gono na  UKIMWI kwa mbaaali,...
....KAMA ILIVYO kuna wamuogopao MWALIMU  wa SHULE mashuleni badala ya KUMUHESHIMU tu,....
..... na kumdharau bila woga MGAMBO wa shule YULE MWENYE hasira za chapuchapu  na apendaye aheshimiwe kwa kuwa anastahili heshima angalau OFISINI KWAKE  ambako ni pale kwenye MAZINGIRA  YASHULE mwenye SILAHA iuayo hata kama ni ya aina ya NCHALE,...


... au kama tu kulivyojaa waaminio MUNGU waogopao BINADAMU WENZAO kustukia wanadhambi,...
..... kuliko HATA waogopavyo MUNGU  waaminiye anaonakote mpaka MIGOMBANI  GESTI awaonaye  pale chobisi walikojificha wakifanya kwa starehe zao tu DHAMBI zao murua!:-(


Swali:
  • AU?
  • Umechunguza kuwa hadi leo hii kuwa unapatia wakumuogopa?

Ndio,...
.... labda WENGI wetu  tunabahatishabahatisha WAKUOGOPA,...
.... ndio maana unaweza kukuta hadi baadhi yetu tunasita hata kuandika majina yetu  tuki-``KOMENTI´´ kwenye MABLOGU ya watu kwa kuogopa tusije julikana bure ,...
.... na huku hatujui ni nini tunaogopa kama tukijulikana ni siye tuliyetukana mtu kama sio kumkumbusha  tu kwa sentensi kama`` Mchawi msenge  WEE  , lione vile tabia kama POPOBAWA!´´:-(


Samahani!:-(
NI  wazo tu hili JEMADARI Mheshimiwa,...
.......NA  wala USIKONDE  mie mwenyewe fulu DHAMBI!:-(


Hebu Paul Simon abadili wazo na kurudisha ustaarabu tena hapa kijiweni kwa ndude-50 ways to LEAVE your LOVER




Au tu Paul Simon amalizie tu na-Diamonds on the soles of her shoes

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP