Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KICHEKESHO KILEKILE kilichowahi kukuchekesha KIKIRUDIWARUDIWA,...

>> Sunday, February 20, 2011

....kwa kawaida huacha KUCHEKESHA ,...
.... na kikizidishwa dozi ya KURUDIWARUDIWA chaweza kukukasirisha MTU  baada ya kufanikisha KUKUBOA,...
..... na istoshe chaweza mpaka kugeuka kabisa na KULIZA mtu!:-(

Swali:
  • Unabisha?


JUMAPILI NJEMA !:-(

Hebu Reggie Watts arudishe ustaarabu kwa kitu - Big Ass Purse


Aendelee kwa ...Au tu Reggie Watts arudie tu na pambio-Fuck SHIT stack


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 5:10 am  

NAAM...
Ucheshi ni pale tu unapochekesha.

NA...
Mara zote huwa ni kichekesho kama unachekesha na si kuwa na uhalisia wa ucheshi huo.

UNADHANI.....
wanaorekodi movies ambazo wasomaji wa hapa wanazipenda, wangependwa ikiwa movie hizo zingekuwa zinaua watu kwelikweli?

LABDA......
Watawala wa Tanzania hawajajua kuwa ya Gongo la Mboto yangechekesha kama yangekuwa yameigizwa "Mbotowood" na sio uhalisi wa vifo na milipuko iliyotokea.

PENGINE.....
ni yaleyale niliyosema kuwa "hakuna wa kulaumu kwa kuwa wa kulaumiwa ndiye mlaumu."

NINALOMAANISHA HAPA NI KUWA....
wale wanaostahili kulaumu sasa ndio WALAUMIWA kwa kuwaweka WATAWALA WASIOJALI wala KUWAJIBIKA.
Matokeo yake ni kuwa tunaogopa kulaumu kwa kuwa tunaogopa kuambiwa kuwa NI CHAGUO LENU.
Ni wakati wa KUBADILI MFUMO LA SIVYO TUTAENDELEA KUWA WAHANGA WA MIFUMO YETU YA MAISHA.

Well...Hakuna ushuhuda wa asiye na dhambi na hakuna furaha kama hakuna karaha, nadhani ili tusonge mbele ni lazima tuweke kando SIFA YA KINAFIKI ya kisiwa cha amani.

TUSIUANE, TUSIPIGANE, LAKINI TUTIMUANE.

SIMON KITURURU 7:29 am  

@Ras Mubelwa: Nakubaliana kabisa na ulivyokabili hiki kidude!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP