Leo ni MWAKA mpya KICHINA!
>> Thursday, February 03, 2011
Wakati na wasiwasi labda TANZANIA hatujastukia tu ila huu mwaka 2011 kutoka kwenye KALENDA za WATU WENGINE tuliyoirithi,....
....ni mwaka wa KUMI tu au angalau WA HAMSINI tu kwa TANZANIA kama tungekuwa wajanja wakuwa na KALENDA yetu ,....
.... na wala hata sio wa ELFU MBILI NA KITU kama ilivyo kwenye nchi NYINGINE kama USWISI na MAREKANI,........hata kwa kuangalia baadhi ya mambo kinamna hata kwa kupiga CHABO walipo WABOTSWANA, ......
....ILA :
....Nawatakieni kila la kheri WADAU WOTE katika MWAKA HUU wa 4709 wa KICHINA!
HAPPY new year WADAU!
Kwa habari zaidi kuhusu mwaka huu,...
.... nenda HAPA
......au HAPA
Au google tu hii ndude MHESHIMIWA !
AU?
Kwa kiduchu:.....
.....Chinese New Year
By the Chinese Calendar
2011 is the Year of the Rabbit,
which is also known by its formal name of Xin Mao.
AAHHG! -hebu tubadili tu WAZO kwa kumpata MADILU SYSTEM akirudia -KOKO
Au tu ngojea tu MADILU arudie tu na -KUPANDA
Na hebu CARLYTO naye aimbe tu wimbo wa Simaro Massiya Lutumba uitwao - Maya
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Haya Heri ya mwaka mpya wachina!! Dunia hii jamani....
kwa maana hiyo inabidi kufanya mambo kijanjakijanja sana mwaka huu kama sungura....lol!
Kweli kila mtu ana mwaka wake mpya, sembuse nchi, au bara au dini...lakini mmmh, itabidi ufanye kazi ya ziada kumfahamisha `mbongo'!
@DA Yasinta: Dunia hii mambo yake valuvalu ukiingia kichwakichwa lazima uchekeshe!
@Kadinali CHACHA: SI ndio hapooo!
@M3:Lakini inasemekana wasiofahamu wanakaunafuu kao pia kwa kuwa kufahamu saa nyingine ndio kuumizako watu VICHWA!:-(
Kuumia vichwa sisi Waafrika lazima tuumie tu kwani tunadai sehemu yetu kama Kaka-Watu!
Wachina na hesabu zao zote, kama makabila yote duniani, ni watoto waMswahili tu.
Inasemekana tukiwashawishi watoto wetu kusoma mambo ya kale ya nchini Misri ("KAMETA", kwa lugha ya Kiswahili), hasa yale maandishi ya HYROGLYPHICS ("KAMETOGRAFIKA"), tutakuja kujua jinsi nasi Waafrika tulivyohesabu miaka zamani.
Hizo zote ndizo hesabu na maandishi ya kwanza kabisa duniani miaka elfu ya maelfu kabla ya kuzaliwa kwa huyo Mtoto wa Kiswahili Yesu/Issa.
Kumbuka, wakati huo wa ???ugunduzi??? (INVENTION) wamaaindishi hayo (KAMETOGRAFIKA) ambayo ni ya zamani kuliko yale ya Mesopotamia, Mwarabu alikuwa bado kabisa hajarejea Afrika kaskazini iliyokuwa ni yaWaswahili tupu kuunganisha na kabila lakisasa Afrika Kusini la Wazulu wa Shaka pamoja na Waxhosa wote waliyokuja Afrika Kusini majuzijuzi tu tuseme karni chache kabla ya Wazungu na wote waliokuta Afrika Kusini ni ya Watonga/WaDzonga/WaZn/WaAzania/ WaZion.
Kwa kumalizia: Wachina nawapenda sana kwa sababu historia yao yatuwezesha kuchimba zaidi juu ya Uswahili wetu. Vilevile PROPAGANDA zao kuhusu historia ya ulimwengu si nyingi kama zile za Mzungu.
@Mkuu GOODMAN: Hilo nalo ni neno!
Post a Comment