Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna MAMBO ni MAARUFU kweli - kama UCHAWI kwa wasiojua UCHAWI!

>> Tuesday, February 22, 2011

Kuna mambo ni MAARUFU,...
.... hata kama wengi ambao jambo HILO ni MAARUFU kwao,...
.... hilo ni MAARUFU kama  neno au JINA tu!:-(

Na kwa kuwa wa kitu UMAARUFU,....
......unamchezo wakufanya watu wadhanie KITU  kinajulikana kwao,....
.....kuna wadhaniao wanajua  mpaka kinachoendelea nyumba ya jirani kwa kuwa ni nyumba iliyoko jirani na WAISHIO HUMO ni majira tu.:-(

Swali:
  • Si kuna ambao kwa kuwa wanajua jina la RAIS ni KIKWETE au OBAMA wadhaniao wanajua kazi ya URAIS ni ipi?

  • Na si uchawi labda ni maarufu zaidi kwa WASIO WACHAWI hasa kwa kuwa kwa WACHAWI  uchawi ni kitu tu cha kawaida kama tu ilivyo umalaya kwa MALAYA?
  • Unafikiri  ni watu wangapi wanajua UCHAWI ambao wamekatashauri wanaogopa UCHAWI kwa kuwa tu wasikiayo kuhusu UCHAWI ni maarufu kwenye stori tu?


Ndio,...
... labda tuwewaangalifu na vitu MAARUFU kwa majina tu,...
.... kwa kuwa vinamchezo wakutusahaulisha kuwa KIUKWELI KABISA  labda hivyo  HATUVIJUI,...
.... na kwa kuwa hatuvijui tunaweza kuogopa SIMBA kuliko MENDE wakati labda ni MENDE ndiye hatari zaidi kwa kuwa anamchezo WAKUWA na ACCESS mpaka ya VYAKULA VYETU na  kwa starehe zake  kunyea chakula kiliwacho na watu huku twajua anauwezo mkubwa wakuwa na vijidudu vidhuruvyo BINADAMU  !:-(Swali:

  • AU?

Na ,...
....ukweli ni kwamba NAWAZA TU hapa MHESHIMIWA!:-(Na hebu BOB MARLEY abadili kitu ghafla kwa -JOHN was
Au tu  GURU achakachue wimbo wa BOB Maliya huohuo-John was

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 9:27 am  

Nakweli, Mkuu! Lakini mimi sijui Kiswahili chake itakuwa nini hiyo "KNOWLEDGE IS POWER" labda "ujuzi ndio nguvu"?

ANYWAY, mimi nafikiri hakuna kitu kizuri kwa mzazi kuliko kumsaidia mwanae katika masomo ya Sayansi kwasababu palepale ndipo ataelewa "kama mchawi analoga kweli analogaje au habari zote hizo ni utumbo mtupu tu ili mradi unachunga huyo mende na sumu ya mchawi visiingie kwenye chakula chako".


Nje ya tundu: vipi huko Christchurch? Mmepatwa na nini kama nimekwelewa vizuri uko hukohuko?


Kama sikukosea, basi POLENI SANA!!!

SIMON KITURURU 10:12 am  

@Mkuu Goodman: Kanisani Christ church ni poa tu! Pale nilileta tu ile wkati nataka kujadili Muafrika ni nani hasa ukizingatia huwa watu automatically huchukulia mie ndio MUAFRIKA na kuzinguka kidogo wakistukia waliowengi kwenye kwaya waonekanao ni WAZUNGU wote wakijitambulisha kama Waafrika.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP