Kwa WAISLAMU na WAKRISTO wa Tanzania!
>> Saturday, February 26, 2011
Kama MNAFUATILIA labda mmeshasikia malumbano yameshavuka hatua ya MANENO ,...
... nakuingia katika kubwengana huko Mto wa Mbu wilaya ya Mondulu mkoani ARUSHA.
Inasikitisha tunakoelekea!
Tukumbuke kuwa kama DINI kazi yake ni kuunganisha watu na MUNGU labda ni kumkosea MUNGU kuendeleako kwa kutumia jina la dini kama watu wa MUNGU watafikia KUPIGANA na hata kuuana kisa ni wadaiyo waliyoyasoma MANENO,...
.... ambayo naamini kama yanasababisha VITA na sio AMANI hayo hayana uhusiano na MUNGU WA UPENDO - na nimatumaini kwa wampendao MUNGU na AMANI Tanzania kuepuka kufuata mkondo wa yaendeleayo ARUSHA!
Inasikitisha tunakoelekea!
Na itasikitisha sana ZAIDI kama itakuwa ni DINI zisemekanazo ni za AMANI na upendo za MUNGU wa UPENDO ndizo zitakazoharibu kabisa TANZANIA na kuua hata zile dalili za amani na UPENDO zitufanyazo WATANZANIA kusifia kuwa nchi yetu ni ya AMANI na watu wake ni wenye UPENDO zilizookoa TANZANIA mpaka sasa!
WAKRISTO na WAISLAMU kwa pamoja jaribuni kusitisha UDINI jamani ,...
....na kumbukeni nchi sio ya WAISLAMU na WAKRISTO tu!
Tukumbuke pia SISI wote ni NDUGU jamani!
MUNGU IBARIKI Tanzania!
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Dini ni vyama tu kama vyama vingine. Binafsi nashukuru kuwa katika zama hizi, nimeshuhudia vyama hivi vya dini vikianzishwa (labda ni mfumo wa vyama vingi vya kidini) kama vile vya kisiasa vianzishwavyo kwingi duniani.
Nimekuwa nikitumia kamuda kangu kutafakari dini na imani. Kuna jambo ambalo binafsi naona twalikosa. Bado hatujaitambua "dhana" sahihi ya Mungu.
Watu tumekuwa tukijiuliza swali rahisi, hili la Mungu ni nani. Lakini mimi naona umefika wakati sasa wa kwenda mbele zaidi na kujiuliza "Mungu ni nini" na kama watu tulishajiuliza, nahisi bado hatujapata majibu sahihi. Kiashiria cha hili ndio hayo machafuko ya kidini na kuwepo kwa ugumu wa watu wa dini tofauti kushindwa kuoana au kuishi pamoja katika maisha ya kawaida.
@Mkuu Albert: Mmmmmhhh!
Post a Comment