Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nahamu kweli ya kubadili MANENO,...

>> Monday, February 28, 2011


.... ili LABDA hata kwenye BLOGU hii KAMA SIO KWINGINE  niseme maneno ambayo kwa WAHESHIMIWA kiheshima ni lugha nzuri!:-(

Na labda niongee daima MANENO,...
.... ambayo ni ruksa KUTAMKWA kama waheshimiwa wamejifunza kuwa KUSIKIA hayo ni RUKSA hasa kwa sababu kama unataka KUHESHIMIWA  nitamkayo sio kama ya mheshimiwa aliyonayo wakati anapiga punyeto AMBAYO HAYAPAYUKI  kwa kuwa hadharani afanyacho hakitamkwi na WAHESHIMIWA ingawa labda waliokubuhu kwa hilo ni WAHESHIMIWA HAOHAO  WAHESHIMIWAO KWA MANENO WASIKILIZAO AU WASOMAO WAFIKIRIAYO NI YA HESHIMA hasa kwa kuwa kuna vitu hadharani hawatamki  hata wao na kuna waaminio hicho kitu ndio moja ya kifanyacho wao ni WAHESHIMIWA hasa kwa MANENO  wajifanyao ni watu wazuri!:-(

Swali:
  • SI kuna uwezekano kuna WAHESHIMIWA kwako ambao ni WAHESHIMIWA kwa sababu tu hujui kitu fulani kwa kuwa hujasikia NENO na kifanyacho kwako HAO ni waheshimiwa ni kwa sababu tu ya maneno yao tu wakati kivitendo labda uheshimiwa wao ni kama mavi ya jana tu ya mwendawazimu aliyekula mayai viza?

Ndio,..
... kuna watu wanakidhi tu mahitaji yao YA KUHESHIMU MTU kwa kusikiliza tu MANENO ya mtu ,..
... wakati wangefuatilia zaidi ya maneno ya MTU labda wangeheshimu NGURUWEE zaidi ya MHESHIMIWA asiye bitozi!:-(

Ndio,....
...hili NI WAZO  tu MKUU kwenye neno!:-(Hebu chapchap Youssou N'Dour abadili mkao kwa - Marley
Youssou Ndour akiwa na Morgan Heritage adinye- Don't Walk AwayYoussou N'Dour akiwa na Patrice adinye pia ~Joker
Au tu anyokolishe tu na -Birima

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:24 pm  

Duh! kaazi kwelikweli hii ya leo ni kali...Simon jamani unaweza kuunganisha maneno!!

SIMON KITURURU 2:09 pm  

@Da Yasinta:

DUH ! Sijui kwanini siaamini kama mie mzuri hivyo KIKUUNGANISHA maneno hasa ukizingatia bado nasikia waunganishao maneno vizuri wameolewa au kuoa bonge la MTU walioweza kumuunganisha kwenye maisha yao kimaneno kama wewe VILE ,...
.... halafu mie yani anikunaye MTAMANIO labda yani hajakubali bado kimaneno MALAVEDAVE yani.:-(

Swali:
AU?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP