Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

PROPAGANDA zitumiwazo na SERIKALI kwa watu wake wenye AKILI!:-(

>> Tuesday, February 01, 2011



Moja ya PROPAGANDA zilizowahi kufanikiwa sana hapa DUNIANI ni propaganda za serikali ya ADOLF HITLER ambayo ilifanikiwa kufanya karibu TAIFA ZIMA la WAJERUMANI kutostukia kitu na kuamini ,...

.... mawazo ya KIONGOZI huyo na uongozi wake ni BOMBA,...
... na kutostukia hata maswala ya WAYAHUDI wa KIJERUMANI, na WAROMANI aka majipsi ambao serikali yake inasemekana ilikuwa inawaua kipindi hicho!:-(



Propaganda kiboko na labda hata sasa hivi BAADHI ya WAYAHUDI haohao waliokoswakoswa na PROPAGANDA za HITLER hata kama huamini,....
...... wanaweza kuwa nyuma ya PROPAGANDA za serikali ya Israel ili kuhakikisha watu wake wanamtazamo fulani ambao unaweza mpaka kufanya waamini kuwa wao ni tofauti kuliko watu wengine kitu ambacho hata kama HAKIUI Wajerumani leo hii ila bado kuna kiwatengao,...
....na tofauti na pia chuki zijengekazo kutokana na hilo  zaweza kurudia kama yaliyowahi kutokea UJERUMANI kwa kuwa PROPAGANDA labda ndio kinachounganisha yatokeayo leo katika eneo hilo WAISHIO WAYAHUDI na WAARABU  wakati tunaendelea kushuhudia SIKU HIZI kwa jicho na kilichotokea UJERUMANI hata kama kuna wadaio hawakukishuhudia kwa MACHO.:-(

Swali:

  • AU?


PROPAGANDA Tanzania hasa zile za NYERERE zilifanya watu TANZANIA kujisikia ni WATANZANIA,...
...na zikafanya mpaka watoto wa shule za vidudu kuimba KABURU ni MBAYA ila ,...
...ziliruka vitu pia ,...

..... mojawapo LIKIWA NI kuwa bado kuna WATANZANIA ambao hawaamini TANZANIA BARA na TANZANIA VISIWANI ni nchi moja,au tu pia WENGI waliokuwa wanaimba UJAMAA na KUJITEGEMEA katika zidumu fikira za MWENYEKITI walikuwa moyoni ni MABEPARI:-(

Ndio,...
...PROPAGANDA zinamchezo wa KURUKA VITU,...
.... na kukazia baadhi tu ya MAMBO na kwa mtazamo fulani tu wa jambo kitu kifanyacho,...
.... baadhi kuamini WANACHOJUA WAO ndicho SAHIHI na wengine wote wamepotoka,...
... kitu ambacho labda  NI HATARI ukifikiria kwa staili hiyo,...
... kwa kuwa sataili hiyo inaweza kufanya  JAMII ya watu wenye AKILI kuchekesha  kwa kuamini PROPAGANDA   kwa kuwa ,...
...PROPAGANDA za uongo ZIPO PIA!:-(


NAENDELEA kuwaza na ni MTAZAMO TU HUU MHESHIMIWA !:-(

Swali la nyongeza:
  • SI unajua labda  hata hapa nifanyacho labda ni PROPAGANDA?





Hebu EIGHT MILE ROAD waingizie -Life is a traffic JAM





Au tu ngojea Vybz Kartel alainishe staili na hoja kwa -Don't diss me

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 5:15 pm  

Walikuwa wakisema ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE! na watu huitika ZIDUMU! Pamoja na kuwa binafsi ninampenda Nyerere kwa kutokuwa mbinafsi kama warithi wake,lakini watu tulikuwa gizani kwa kiasi fulani. Cha kushangaza ni kwamba utamaduni huu wa kuabudu viongozi unaendelea hadi leo hii kwa kuwaita viongozi "waheshimiwa" au "watukufu"

chib 9:28 pm  

Baadaye Nyerere alishtuka walipokuwa wakisema zidumu fikra sahihi, kwani aliona wanampiga kijembe ya kuwa kuna nyingine sio sahihi

Goodman Manyanya Phiri 9:43 pm  

Ukweli hamna duniani, Bwana Simon. Ukweli ni mawazo ya mtu binafsi tu na ndio maana ubishi ndio roho na kiini cha siasa.

Kusudi chama chako kipate ushindi kwa wananchi, lazima utie chumvi kidogo lakini siyo utie chumvi nyingi leo, kesho ndogo, na keshokutwa hamna chumvi kabisa. Hutakuwa na walaji wakwaminika kuja kula hotelini mwako daima namna hiyo.


Pamoja na utaratibu katika kutunga PROPAGANDA yako, lazima unaingiza hata jinsi unavyoendesha maisha yako (LIFESTYLE). Hutakuwa na mafanikio katika siasa kama maisha yako kama kiongozi wachama hicho hana mwelekeo au PATTERN sawasawa na PROPAGANDA yako.

Kumaliza, jinsi unavyotia chumvi kwa kiasi sawasawa na ile PATTERN yako... hiyo ndiyo propaganda. Nami ninayo, nawe unayo, CCM inayo, ANC, PAC na vyama vyote duniani PROPAGANDA ni lazima tu! Ila ni aibu kukubali kuwa "maandishi yangu yote ni PROPAGANDA tu" kwasababu kwa watu wakawaida, wanafikiri PROPAGANDA=uongo.

Propaganda yenye mafanikio ni ishara ya ubongo unaofanya kazi vizuri. Na kweli, Julius Nyerere alikuwa PROPAGANDIST mwenye mafanikio. Barani Afrika tunaweza kumhesabu pamoja na PROPAGANDIST kama Pixley ka Isaka Seme (mwanzilishi 1912 wa chama cha African National Congress Afrika Kusini), vilevile na Kwame Nkrumah (Ghana).

Simon Kitururu 2:53 am  

@Mkuu Malkiory: Inasemekana MAZOEA yanatabu zake ati!:-(

@Mkuu CHIB: Moja ya kitu nachomzimia NYERERE ni jinsi alivyokuwa na machale!

@Mkuu Goodman:

Kuna wengi lakini wanaweza kubisha kwa kusema duniani ``UKWELI UPO PIA!´´ Na ni hizo chumvi kidogo ndio vyazo vya vipotezavyo UKWELI DUNIANI.

Tatizo ni kwamba kwa kuwa BINADAMU hana uwezo wa kujua yote kutokana na udhaifu wa KIBINADAMU basi ndio maana PROPAGANDA hatutaweza kuachana nazo na WAJUAO KUSHAWISHI upande wao wa jambo ndio watakuwa kwa muda fulani wanafanikiwa kuzubaza watu na PROPAGANDA zao.

Ila nakubaliana kabisa na mengi katika mtazamo wako wa hili jambo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP