Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa MSWAHILI ajuaye KIINGEREZA : ``ILOVE U!´´ vs ``NAKUPENDA KIMWANA!´´:-(

>> Friday, February 04, 2011

Kwa MSWAHILI ajuaye KIINGEREZA inasemekana ni rahisi kumuambia MSWAHILI mwenzake ``ILOVE U!´´ kuliko kumtonya: ``NAKUPENDA CHEUSI DAWA!´´:-(


NDIO,....
...inasemekana  kwa lugha ya kigeni,...

...  hata MATUSI yake hayana ukali sana  ,....
... kama ukifananisha na MAKALI  na UTAMU wa kumtusi  MHESHIMIWA  azungumzaye KISWAHILI tusi la NGUONI kwa lugha ya KISWAHILI!:-(



Swali:
  • SI unastukia  kuna UWEZEKANO kuna uvumilivu  zaidi ujitokezao kwa WAHESHIMIWA  WASWAHILI  wa KIBONGO waangaliao sinema za HOLLYWOOD  na WATOTO WAO ambazo asilimia kubwa lugha zake ni MATUSI mtupu  na hapo ni tukiruka  matendo  kwa mtazamo wa WAHESHIMIWA wa KIBONGO kwa kuwa unajua MOVIE hizo zingekuwa ni  za KISWAHILI  kwa LUGHA HIYOHIYO  wangedai hawawezi kuangalia USHEZI huo au angalau wangefukuza watoto sebuleni kwa kuwa  GHAFLA ndio zingegeuka ni matusi KIKWELI?

Ndio ,..
... inasemekana  kwa WABONGO ,...
...hata SHENZI kwa ung'eng'e,...
... sio SHENZI sana,....
... na ndio maana yadaiwa  hata  katika KIMWANA hasa ASIYE MZOEFU wa kucheza na HISIA  ZA WATU ,...
....katika kumuingiza  mjini  MUME  wa MTU ili apagawe na kulainika ili afikishwe kwenye kipengele ambacho ANACHUNIKA BUZI kirahisi,...
....``I LOVE U !´´yasemekana inatoka kirahisi kuliko ``NAKUPENDA  SANA na nakuwaza wewe tu !´´,...


... hasa HAPA UKIZINGATIA  hatuongelei maswala ya UJUMBE WA KUANDIKIANA  kwa barua , KITEXT za VIMOBITEL au tu e-mail zitumiwazo siku hizi na watoto  wa siku hizi katika kuwekana sawa  KIMLAINISHO  kabla hajalizwa mtu  au kuliwa kidude mtu!:-(


Swali:
  • Hivi wewe unafikiri unakawaida YA KUMDANGANYA  kirahisi MGENI asiyekujua sana au  MTU udhaniaye anakujua kisawasawa?

Ndio ,...
.... ningetaka kweli   kusema ni UKWELI MTUPU kuwa ,...
.... lugha ya kigeni  inarahisisha KILA kudanganya au hata KUMTUSI mheshimiwa  kuwa ngorojo yake inanuka uvundo,...
...  ILA  twajua kuna MIJITU hasa ile MIOGA  ijitutumuayo kama vile HAIOGOPI KITU  ikikujua ,...


...ndio HASA   na ikikujua haina sababu ya kukuogopa kwa kustukia kuna maeneo  weye MDHAIFU au kwa ujumla weye KIBONDE TU ,...
... basi ndio itazidisha  kuwa  MIONGO kweli na kwa mitusi ndio balaa kwa kuwa inajua ukichukia inaweza hata  KUKUBONDA pia na ukashindwa kwenda kusemelea kwa MAMA.:-(


Ndio....
..... nasikia MIJITU MINGINE  ikujuayo unahitaji BWIMBWI  ndio hasa kwa makusudi ina  mchezo wa kugida BWIMBWI yote ikaisha ILI WEYE ukose kabisa,...
.... na  kwa kuwa inakujua UZALENDO WAKO basi imeshastukia na haikupi ``I love U !´´ ng'o  wakati lugha muongeayo ni  KISWAHILI kwa kuwa inajua unachukulia wafanyao hivyo huwa ni wale WAJISHEBEDUAO wanajua UMOMBO na eti ni TOTOZ za KISASA fulu KUFACEBOOK kitu ambacho hupendi ,...
... kwa hiyo KATIKA KUKUINGIZA KICHWAKICHWA  inakupa bonge la ``NAKUPENDA SANA kuliko HATA nanilii yangu!´,...
....wakati kumbe  huo ndio  WIZI MTUPU!:-(



WAZO limenishinda!:-(

Na ni  WAZO TU HILI  hata kama liko  zigizaga wajameni a.k.a WAHESHIMIWA loooh!:-(
Na nawatakieni IJUMAA na WIKIENDI NJEMA  ndugu , jamaa , marafiki na MAADUI!


Hebu STEEL PULSE warudishe  usiriasi hapa kijiweni kwa-Ku Klux Klan




Steel PULSE wasawazishe mnesoneso kwa-SOUND SYSTEM





Steel PULSE wakune kipele kwa- Babylon Makes The Rules



Steel PULSE waingilie kiundani zaidi shughuli kwa -Tribute To The Martyrs





AU tu wamalizie tu kwa -CHANT a psalm

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

John Mwaipopo 11:01 am  

pia ni rahisi kwa njemba iliyokuwa haijatahiri mpaka kufikia miaka 40 kumjulisha mwenzie kuwa nimefanyiwa CIRCUMCISION kuliko kusema nimetahiriwa

Yasinta Ngonyani 1:06 pm  

Darasa nzuri! Ijumaa na wikiend njema nawe pia:-)

Goodman Manyanya Phiri 8:34 pm  

Ukoloni umemmaliza kabisa Mswahili, Nduguzanguni na sijui tutapata lini marekebisho ya kiakili.

Mwanangu wa mwisho amezaliwa mwakajana na Mungu amenibariki ilikuwa tarehe kumi mwezi wa kumi mwaka elfu mbili NA KUMI, kasoro dakika kumi ya saa nne asubuhi.

Sasa kwa undanganyifu wangu nikafikiri lo, ni mtoto maalum; na namtafutia kila kitu kizuri tena MAALUM.

Leo asubuhi mama yake aliposema: "Tutafute mwanasesere", nikafikiri "lazima nimpate waKiswahili". Lakini madukani hayupo nami sijawahi kumwona maishani mwangu.


Jioni hii nikamwuliza mama mmoja kwenye TAXI "IKUPI NGINGAKONA UKUTOLA UNODOLI OMNYAMA?...Wapi naweza kumpata mwanasesere mweusi?"

Naye akajibu: "Wapo tele ukienda upande wa CENTURION huku PRETORIA"

"Kwanini sijawahi kuwaona?" nikamwuliza.


"Niwabaya kama nini!" alinijibu. "Sura zao silaini kama zile sura za wanasesere wa Kizungu."

Mswahili hajipendi yeye mwenyewe; wala lugha yake haipendi!

Mzee wa Changamoto 5:09 am  

Natafuta tafsiri za kiswahili sahihi cha LOVE, LIKE na LUST.
Maana watu wana-love kitu, mtu mpaka vitu vya mtu ilhali wana-love na ku-lust hivyohivyo.
Kwani ni kitu kimoja?
Nawaza enzi za kutokea, kama ungemtokea binti na kumwambia "napendezwa nawe" ama "nakutamani", unadhani ingekuwaje?
Kwanini vitu tofauti viwe na kitu kivifanyavyo viwe tofauti kwa umoja?
Hivi naeleweka? Maana huu UJINGABUSARA unabusarisha wajinga na kujingisha wenye busara.
Labda ndio maana wote (wajinga na wenye busara) wapo na ndio maana ujinga na busara vyote vipo.
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUU!!!!!

Simon Kitururu 6:39 am  

@Mkuu John THE Baptist: Ila kutahiriwa wakati KIDUME una miaka AROBAINI yani!:-( Kama ningekuwa miye wala nisinge ongelea topiki na nnikiwa na matumaini hatuna atakaye stukia !:-(

@DADA Yasinta: Ingawa umelisifia darasa hili! Sijui kwanini nahisi umesifia tu kama kawaida yako! Kwa kuwa sijawahi kukuona umekomalia kitu sehemu yoyote ki HASI! Ningefurahi kweli kama angalau mara moja moja ungesema tu kitu hasi kama vile katika topiki hii kuwa`` UNNAJUA weye Simon Kitururu- koma wee huu ni UJINGA mtupu unauweka hadharani na hivi ukufunzwa heshima kwenu? KOMA weee KOMA kabisa weye Mtoto wa KITURURU kutia aibu hadharani!´´. Samahani! Kila siku uko chanya tu kila sehemu DADA yASINTA. Hudhani hicho sio kitu cha kawaida?

@Mkuu GOODMAN:Mhhhh!

@Papaa MUBELWA: HIZO love , lust na LIKE si tutungie tu kama alivyokuwa anafanya Rais NYERERE? Maana toto tundu NYERERE lilikuwa likikosa neno linaingizia KIJITA halafu WABONGO ghafla tunakubali ni KISWAHILI . SI unakumbuka hata wakati TOTO tundu NYERERE wakati linaachia UHESHIMIWA likadai kitendo kile kilikuwa sio kujihudhuru bali ni KUNG'ATUKA?

Na nakuhakikishia toto linalotaka kusikia linapendwa ULILOLITOKEA ukianza kutumia hayo maneno uliyokuwa unayapapasa kama "napendezwa nawe" ama "nakutamani", ...
.... unaweza kujikuta umenyimwa UTU UZIMA wa mtoto mzuri hivi hivi na adanganyaye ndio anapiga bao KI jemadari GENERALI MSUGURI hivihivi.:-(

Na kuhusu huuu UjingaBUSARA:

Hivi unajingisha eeeh?:-(

Rachel Siwa 6:49 pm  

hahhahaa wanaongeza msisitizo kaka Kitururu!!!!!!!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 8:41 pm  

Nilikwenda kutafuta kadi za Kiswahili za Valentine pale Posta mpya kwa lengo la kum-surprise mama watoto wangu.

Nilishangaa nilipoambiwa kwamba kadi za Kiswahili hazipo mpaka nifanyiwe oda maalumu kutoka huko viwandani kwa Wahindi zinakotengenezwa. Nilipouliza ni kwa nini hakukuwa na kadi za Kiswahili, jamaa waliniambia kwamba hakuna mtu anayetaka kuzinunua. Mwingine akaniambie eti lugha ya Kiswahili huwa "hainogi sawasawa" katika kadi.

Nilitoka hapo nikiwa najiuliza sababu zinazoifanya lugha moja "inoge" na nyingine "isinoge".

Simon Kitururu 8:25 am  

@Rachel: DUH!
@Mkuu Matondo:Duh! eti KISWAHILI hakiwanogei ! Nimewazishwa sana na ulichosema!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP