Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KIFIKIRIWACHO ni PENDO na mapenzi wakati KINADHANIWA ni mapendo na MAPENZI!

>> Thursday, February 17, 2011

NDIO,...
... kuna UPENDO ambao unadhaniwa UPO kwa kuwa tu AHITAJIYE kupendwa katika kujishughulisha kwake kustukia dalili za PENDO,....
.... kajifunza jinsi ya kutafsiri dalili tu fulani nakuamini huo ndio  UPENDO!:-(


Ndio,...
.... kila KIDHANIWACHO ni PENDO,...
... bado sio MAPENDO hasa kama kigezo cha kutambulika HIVYO ni kuwa tu adhaniacho ni UPENDO ni kwa kuwa kinamfanya ahitajiye KUPENDWA kujisikia anapendwa kutokana na vifanyikavyo kufiti tafsiri zake za ni nini UPENDO!:-(

Swali:
  • Si umeshawahi kusikia kuwa ni KWA MAPENZI MAKUBWA YA WAZAZI KWA WANAO ambayo hufanya mpaka WAZAZI FULANI wachape aka WAWAPE MKONG'OTO watoto wao kitu ambacho kwa WATOTO labda KUPIGWA na KUPENDWA vinaweza kuwa havina UHUSIANO?

  • Si unafahamu kuwa labda si kila AKUSIFIAYE anafanya hivyo kwa KUKUPENDA hasa ukizingatia SIFA zaweza KUUA?

Ndio,...
....inasemekana hakuna MSIFIAJI mzuri DUNIANI kama yule MNAFIKI,...
.... na mara nyingi apendaye MTU sana KIKWELI inasemekana ni yule ambaye MAPENDO YAKE kwa apendwaye huwa HAYASTUKIWI!:-(




NI WAZO TU HILI Kingunge!:-(






Hebu Nusrat Fateh Ali Khan arudie -ALLAH HOO



Na hebu Kamalakar na wenzake wakatizie denge kwa -Hallelujah Yesu Prabhu



Au tu Tamisha Nicholls arudishe tu rithimu ya wiki ile -BADDER dan DAT

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 4:11 pm  

!!!!!!!!........"""""'
"""" """"""
""" """ """ """""
"" __ __ ""
"
"" / \ ""
" ---- "
' {========) ,,
' """ '
' """ '

chib 6:28 pm  

Hii njemba inajua ya kuwa mko nchi mmoja au!!

Simon Kitururu 6:44 pm  

@Mkuu CHIB: Huyu jamaa bado sinauhakika naye bado kama kitumacho ni YEYE au computer programu kutokana na maeneo mbalimbali nikutako komenti yake hiihii!:-(

Goodman Manyanya Phiri 8:48 pm  

Siku binadamu tutakapoweza kutambua uhusiano barabara katika upendo na chuki ndio mwisho wa ubinafsi wetu. Na amini upendo na chuki ni ndugu kabisa lakini sisi kwa udhaifu wetu tunajaribu kuwatenganisha na baada ya hapo kumpendelea mmoja na ndio maana tunajishughulisha na dalili. Matokeo, dalili za Ndugu Kulwa tunampa Doto na zile zaDoto, kumpa Kulwa.


Tumechang'anyikiwa, Mkuu!

Simon Kitururu 7:31 am  

@Mkuu Goodmana: Si utani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP