Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kutokana na taarifa zangu mwenyewe za KIINTELIJENSIA- nahamu kweli ya MAHINDI ya KUCHOMA!:-(

>> Sunday, February 27, 2011

Leo tokea niamke nahamu ya MAHINDI ya KUCHOMA ,..
....halafu yale yachomwayo BARABARANI.:-(

Halafu mahindi ya kuchoma ,...
....niyatamaniyo ni yale yachomwayo pembeni ya barabara kwa kuwa kwangu  sijui kwanini huwa napenda ZAIDI mahindi ya kununua pembeni ya  barabara  kuliko ya kuchoma mwenyewe nyumbani!:-(


DUH! Halafu leo ningepata na MAFENESI  nayo baada ya kumalizana na MAHINDI ya kuchoma,...
....halafu yawe ni yale ambayo YAMESHA POKOCHOLEWA kutoka kwenye TUNDA MAMA ili  nisihangaike nayo kuyatoa kwenye FENESI mwenyewe ingekuwa BABU KUBWA  yani!:-(

 DUH au angalau basi nimgepata CHIPSI DUME kwa kachumbari , Juisi ya UKWAJU, madhambaru au angalau MAHINDI ya KUCHEMSHA kama sio yale ya KUCHOMA,...
.....  au angalau nipate TU mua uliokatwakatwa kabisa vipande ingekuwa MURUA kweli yani.:-(Kwa kifupi :

....Niko hapa TALLIN - Estonia nikiwa na bonge la Homesickness na kungekuwa na angalau KIMWANA wa KIBONGO hata wakulipia a.k.a  MALAYA wa KIBONGO - hapa nahisi ningeingia dhambi ya angalau kufikiria au kufanya kabisa kitu  KIMHONGO angalau tufanikishe kufanya dhambi za KUDANGANYANA au hata za MATUSI KABISA angalau  kwa kiswahili  tu katika kujaribu kujisahaulisha nje kuna baridi FRIJI halioni ndani na halihalisi inachangia kutojisikia hatuko HOMU yani :-(
Ee BWANA eeh!
JUMAPILI NJEMA na samahani kama nimekukwaza kwa kuwaza KWANGU NYOKO  hapa KIJIWENI kwa SAUTI!:-(

Na moja kwa moja wakati nawaza TOTOZ za KIBONGO ambazo natarajia hapo mbeleni maishani  KUCHUKUA MMOJA wotewote kama MKE -  ambao  hapa nilipo ni hadimu KWELI kama manyoyanyoya YA KIKUBWA  kwenye kwapa la mtoto - ngojea niendelee kujituliza kwa kusikiliza Jamhuri Jazz Band wakati wanamuongelea mtoto mzuri mwenye -SHINGO ya UPANGAJamhuri Jazz Band wanifikirishe maswala ya kuangalia uwezekano wa  kurudi  SHAMBA katika-Nafikiria Kurudi Shamba

Au tu PATRICK BALISIDYA na AFRO 70 Band waingilie kati tu TENA  mwisho wa wikiendi yetu hii kwa wimbo-WIKIENDI

Bado nipo hata kama kwa mtu mwingine anaweza kufikiri niko kipumbavu! !:-(

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 1:38 am  

Kweli nimeamini leo una hamu ya mahindi ya kuchoma ya barabarani..

SIMON KITURURU 7:11 pm  

@Da MIJA: Si jui kwanini baada ya kusoma komenti yako ghafla nikahisi labda hamu yangu KIMFUKUTO labda si ya mahindi ya kuchoma ki vile .:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP