Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa mimi ni Andunje -MTANZANIA!

>> Friday, February 25, 2011

Tatizo moja  kubwa la UTAIFA ni kufanya wenye TAIFA wafikiri ,...

.... kwa kuwa TU wao ni watu wa TAIFA HUSIKA  basi kila kitu kuhusu hilo TAIFA wanajua.:-(


Kwa bahati mbaya kuwa mtu utokaye TAIFA fulani kama ukifikiri,...
... hicho sio KIGEZO wala KWALIFIKESHENI kuwa kila kitu kuhusu hilo TAIFA mtu anajua ingawa labda kuna ukweli kuwa ukiwa MTANZANIA kuna uwezekano mkubwa ukitaka ya TANZANIA kujua.Swali:
  • SI unajua WATANZANIA ni miongoni mwa BINADAMU wasiojua sana kuhusu hata YA MBUGA ZA WANYAMA Tanzania kwa kuwa waendao kwenye MBUGA za WANYAMA na wafanyao tafiti za wanyama walioko katika MBUGA ZA WANYAMA Tanzania kwa kawaida sio WATANZANIA?

  • Unauhakika unajua MLIMA KILIMANJARO unaurefu gani bila kuangalia MAHALI kama nikichukulia kuwa wewe ni MTANZANIA  ujivuniaye mpaka MLIMA KILIMANJARO na ya TANZANIA unayajua?

  • Unauhakika rangi ya BLUU iko chini au juu kwenye BENDERA ya TANZANIA bila kutafuta picha au kukimbilia kuiangalia kwenye MLINGOTI ilipopandishwa?


Ndio,...
.... pamoja na kuwa natokea MOROGORO ,...
.... labda huo sio ushahidi nayajua ya MATOMBO ambayo ni ya KIJIJI au sehemu iliyopo MOROGORO.:-(


Ndio,...
... na labda ni kwa sababu natokea mjini MOROGORO ,...

....hicho ndio kabisa ndio KIKWAZO kifanyacho sijui vizuri ya MOROGORO MJINI kwa kuwa tu nadhania kwa kuwa nipo au natokea MJINI HAPO  basi najua karibu kila kitu kuhusu MOROGORO MJINI kitu  kifanyacho niondoe MOYO wa KUJIFUNZA hata ya hapohapo mjini YANIKODOLEAYO MACHO ila kwa mazoea tu hunifanya nisiyaone au kuyastukia hapohapo mjini MOROGORO.


Swali:

  • Si unajua kila siku njiani ingawa mtu UMEFUNGUA MACHO - sio kila kitu ukielekezeacho MACHO huwa ni kweli UNAKIONA kitu kifanyacho safari nzima ya kutoka kazini au shuleni mpaka nyumbani nikikuuliza ni vitu vingapi unakumbuka uliviona inawezekana ni vichache sana unavikumbuka kuviona ingawa njiani ulivitumbulia macho vitu MAELFU?

Ndio,..
.... kuzoea hata njia ni moja ya KIPOFUACHO watu MACHO katika kuona vilivyopo hata kwenye hiyohiyo njia,..
....na inawezekana ni MGENI kwenye njia ndiye astukiaye hata kuwa hapo pembeni ya njia ULIYOIZOEA kuna MAUA ROZI ambayo  kwako weye mwenye MPENZI kimwana  kipotabo apendaye mambo ya kimagharibi mwenye pendo a.k.a  MALAVEDAVE  ya KIMAGHARIBI  yenye mchezo wa kusaidiwa kupandishwa MDADI kwa maua kama zawadi,...
... ungebanana BAJETI kwa kuyachuma tu ya bure hapo NJIANI kitu ambacho kingesaidia kuongeza bajeti ya PIZZA kitu ambacho kinafagiliwa na TOTOZ siku hizi MOROAGORO.Samahani nilipoteza muelekeo kidogo wa TARARILA hapo juu!:-(Hebu tuendelee....


Na moja ya kitu MTU wa KIGOMA awezacho kujifunza akiondoka KIGOMA,...
... ni jinsi ya kuiangalia KIGOMA kutokea kwa nje,...
.... na yajulikana kuna aina mpya MTU awezayo kuipata kwa kuangalia hata TANZANIA kwa jicho tofauti kisa hajafungamana tu na TANZANIA na UTANZANIA kitu kifanyacho kuwezesha  HUYO MTANZANIA kuiona TANZANIA kutokea engo ya nje,...
....na labda ni kama  MKENYA katika engo hiyo ANAWEZA SASA  kustukia  pia DILI ambalo MTANZANIA amelikalia na wala halioni kwa kuwa kwake ni kitu tu cha kawaida ambacho hakina mpango kwa kuwa haangalii vitu KITOFAUTI na UTANZANIA wake ambao unamfanya aone kwa ndanni na kutofikiria kuangali KITOFAUTI kama aangaliaye kitu kutoka NJE.

Swali:
  • SI umewahi kusikia jinsi waliokuja kuchimba almasi TANZANIA huko mwanzoni walivyoula kilaini kwa kuwa kwa jicho la WATANZANIA almasi lilikuwa ni jiwe tu kama mawe mengine ambalo halina mpango sana zaidi ya watoto kulitumia kuchezea mdako?

  • Na si unajua KENYA inauza zaidi TANZANITE ya TANZANIA na utalii wa MLIMA KILIMANJARO kuliko TANZANIA?NDIO,...
... ukiwa shimoni kuona kwako ni tofauti na AONAVYO aliyeko nje ya shimo ambaye labda anakuona wewe shimoni na analiona SHIMO na yaliyoko nje ya SHIMO kama tu isemekanavyo mwenye uchi anaweza akawa haoni TUNDU la uchi wake kama wamchunguliao uchi ambao wanadeku ndude kutoka kwenye ENGO nyingine kimtazamo wa kishimo au ujazo.:-(


Ndio,...
... na kwa kuwa mimi ni MTANZANIA,...
.... hilo laweza kuwa ni moja ya swala lipofualo jinsi nionavyo ya TANZANIA kitu kifanyacho kuwe na uwezekano nahitaji sana kuwa muangalifu kama WEWE VILE katika ujuaji wangu wa TANZANIA ili usiwe wa KUJIAMINISHA TU NAJUA kuliko ukweli wenye na kuwa labda kama tu ule uliozoeleka kwa WATANZANIA kuwa kwa kuwa NI WATANZANIA hata kama ni watokeao KILIMANJARO basi hata ya SINGIDA wanajua na  ni wataalamu kitu ambacho kinaweza kuwa ni UJUZI HEWA tu ndio wakati wajivunia wanajua ndio ULIOTUNA kiujazo.:-(


Swali:
  • SI unajua kuna watu wengi wenye mgongo hawajui MGONGO wao unaonekanaje ingawa kila siku wanaotu kwenye miili yao?

  • Kwani unafikiri ni wangapi WENYE MGONGO ambao kwa kuwa wana mgongo hicho ndio kikawa hasa ndio sababu hawafikiri hata MGONGO katika MWILI wao au katika kukata kiuno una msaada gani?

  • Unauhakika unajua sehemu zako za siri zina sura gani sasa hivi wakati UNANISOMA  hata kama tunajua kunauwezekano UNAJIJUA maeneo ya faragha na sio wakati tu yana vipele ndio unayachungulia ?

  • Kama MTANZANIA utokeaye DAR ambaye labda hata KIBAHA huijui vizuri -je  unauhakika unaijua TANZANIA kuliko  balozi wa MAREKANI  nchini TANZANIA aliyekuja juzijuzi TANZANIA?

Ndio,...
.... kwa kuwa mimi ni MTANZANIA,...
... labda ni muhimu kujua hilo laweza kuwa ndio chanzo cha kutojua ya TANZANIA.:-(


SAMAHANI hili ni wazo tu MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(
IJUMAA na WIKIENDI njema MHESHIMIWA!


PS:
-Niko Tallin -ESTONIA kwa hiyo kama uko hapa nitonye tukutane  na namchezo wa kula pale African Kitchen kwa hiyo unaweza kusababisha tugongane kirahisi pale kama ukipenda!Hebu tubadili mshawasha kwa kwenda Sierra Leone tukakutane na Vick Fornah adinye-CRY AFRICA

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Swahili na Waswahili 1:40 am  

Nakuunga mkono kaka,hata wimbo wa Taifa unamung`unywa!!.

SIMON KITURURU 9:56 am  

@Rachel: SI ndio hapooo!

Yasinta Ngonyani 10:27 am  

Hakika kaka Simon leo umemaliza ni mada nzuri sana. Kama wengi wangejua haya nadhani kungekuwa na mabadiliko...Wiki end njema nawe na uwe na muda mzuri huko Tallin-Etonia.

Goodman Manyanya Phiri 10:51 am  

Tunahitaji majirani zetu kutwambia ukweli kuhusu sisi na mali zetu. Mtu mwenyewe huwezi ukawa mkweli (OBJECTIVE) kuhusu yako tena yale ya kwako uliyeyazowea.

"Mali iko mfukoni mwangu," mwenye chako unawaza.
"Sasa yanini pupa kuchungulia mfukoni na kuikodolea macho mali ikiwa ni yangu milele?"
Inasemekana mkweli kwako siyo wewe, wala ndugu yako wala rafiki. Bali ni yule mtu asiyekupenda na akutukanaye.

Unaambiwa sikiliza kwa makini maneno ya mtu mwenye hasira kwako na uyatafakari zaidi utakuta UKWELI MTUPU!


"Wewe mpumbavu sana!" (nawe unajibu rohoni mwako: "Mungu, asante! Kumbe ninao uvumilivu kama anavyosema huyu ndugu?"


"Wewe mbishi sana!"/ "Mungu nakushukuru! Kumbe mimi ni mtu asiyeachia ngazi hivihivi?"


"Wewe unaringa sana"/ "Nashukuru, kumbe mie ni mtu mwenye kujiheshimu?!"

Naam, Mkuu Simon! Tunahitaji wale wang'ambo na mto wetu kutwambia ndoo zetu chafu au zinang'ara tunapokwenda kuchotea maji.

Na usifikiri ndoo zikiwa chafu ndio sababu pekee inayoweza kuwa kisa na mkasa wa maneno.


Wakati mwingine wang'ambo na mto watawarushieni mawe na kuwapiga kwa hasira siyo kwasababu Watanzania mmechafua mto na hizo ndoo zenu, hapana. Mtapigwa hata kwa 'kosa la' kufanya hizo ndoo zenu kung'ara na kuzagaa kuliko zile za kwao hata 'kwa kosa la kuwaumiza macho' eti, kwa ndoo hizohizo!

Wikendi njema kwako nawe Yasinta, kwako Simon, kwako Swahili-na-Waswahili pia na kwa wasomaji wote wa blogu yake Mkuu Mtakatifu.

Mzee wa Changamoto 12:35 pm  

Ntarudi.
Nataka NIKAISOME KWA SAUTI

Duh!!!

Swahili na Waswahili 11:14 pm  

Asante kaka Manyanya!nawe uwe na wakati mzuri na wengine wote!.

SIMON KITURURU 9:24 am  

@Mkuu Goodman:Yani nakubali kweli pointi zako!
:-(

Wikiendi njema Mkuu!

@Yasinta:Asante mtotomzuri!

@Rasta Mubelwa: Nakusubiri ubiringishe hoja!

@Dada Rachel: Asante tena kwa kutonichoka!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP