Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Halafu BINADAMU akaingiza KIDOGO!:-(

>> Wednesday, December 29, 2010

Yaweza kuwa:

Ilikuwa  ASUBUHI isiyotegemewa BAADA YA ya  usiku  ambayo hayakutegemewa,...
....kidume PASKALI  aliamka  na KUJINYOSHA huku akitabasamu kwa sana tu bila kujizuia,...
.... kwa kuwa USIKU WA JANA kuna kitu aliingiza kidogo.





Na ilikuwa ASUBUHI nyingine yenye MAMBO MENGINE ingawa  kwa ASHURA hayo yalitegemewa,....
....Ashura aliamka kwa haraka na kutupilia BLANKETI kule mbali  huku akijamba kidogo kwa sauti kama afanyavyo kila akiwa peke yake kwa UHURU ambao hadharani anajizuia,...
....lakini AKILINI  akiirudia mistari ya UJUMBE ambao kuanzia kwa apangacho tu KUVAA hata kabla  hajasema kitu atakacho KUSEMA akitoka nje kwenye UMATI anajua nia  YA APANGACHO  ni HEKIMA na BUSARA hasa katika yale ambayo JAMII kwenye ubongo ingawa ni YA MSAADA watu hawataki kwenye UBONGO  kuyaingiza hata angalau  KIDOGO.:-(

Swali :
  • SI  labda  ni tatizo kwa kuwa BINADAMU hutosheka na KIDOGO   kitu kifanyacho waendao shule baada ya MTIHANI kutupa vitabu kwa kuwa kama wamepasi MTIHANI basi yanatosha waliyo ingiza  hata kama ni kidogo?


Na labda yote ya AJIVUNAYE kwa kujua ni yale tu ,....
.... ubongoni yaliyoingia  tu KIDOGO!:-(


Ni wazo tu MKUU na kutolielewa RUKSA!:-(

Hebu EDDY GRANT atusaidie kurudisha ustaarabu hapa KIJIWENI kwa ndude-Hello AFRICA





 EDDY GRANT arudie -War PARTY




Au tu hebu Eddy Grant amalizie tu na -LIVING on the FRONTLINE

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 11:04 am  

Bado naitafakari falsafa hii, sijui kwa nini sijaielewa ingawa inawezekana ni kutokana na kutupa madaftari baada ya kupasi.

Nitarudi tena.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP