Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuhusu ile LAWALAWA ya SWEDEN hasa sehemu ya mlo iitwayo: CHAKULA!:-(

>> Tuesday, December 21, 2010

Nimesha  ondoka SWEDEN,...
.. na AKSANTE watundu wote tuliokutana na kuhangaisha songombindo.:-(


Samahani mabloga wa SWEDEN ambao nimeshindwa kukutana nao haswa,...
...EDNA mutoto ya MUJINI,...
... na YASINTA ,...
...hasa wewe ni kwa sababu TU  unaishi SINGIDA ya SWEDEN na muda ulikuwa  unabana chupi  KIMTOSHO kwa hiyo nilishindwa kukutokea ili kumtia wivu BABA watoto wako.:-(



ILA,...
...ashakumu si matusi muda wote nilioutumia SWEDEN  nje kulikuwa na baridi kweli kama NYOKO vile  yani!:-(


Ila kwa ndanindani hii ilikuwa mara ya kwanza kugundua MAMA ntilie NYOMI aka HOTELI iitwayo CHAKULA hapo  SWEDEN ambayo MPISHI apikaye UGALI na MLAENDA MZURI KITANZANIA karibu mara zote alikuwa ni MSOMALI,....
.....kama utamstukia kwenye picha zangu hapo chini,...

....imenisaidia kupata mpaka UGALI mara kadhaa  na katika maswala ya JUISI kulikuwa mpaka na SERENGETI BIA kutoka TZ , Bell kutoka UGANDA, Tusker kutoka KENYA ingawa kuna mara kadhaa nilijikuta napata mpaka SINGHA kutoka THAILAND yote ikiwa ni katika kunyegelesha siku ingawa  haki ya nani hakuna kimwana wa KISWIDI aliyefanikiwa kuvuliwa kificha nyeti safari hii:-(




NAACHA wazo !:-(


Hebu GORILLAZ wabadili mkao kwa kitumbua- Clint Eastwood




GORILLAZ wapandishe jazba ya nonihino kimaning'ining'i kwa jiwe-Feel Good Inc




Au tu Ying Yang TWINS wanong'one kwa -The Whisper Song



Au chungulia baadhi ya picha kwenye kijiwe kiitwacho CHAKULA mitaa ya Stockholm ,SWEDEN na baadhi ya maeneo ya jiografia hizohizo kiduchu za juzi ya jana ya leo yake ya kesho kutwa ile....
























































































































































6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:04 pm  

Naweza nikasema ni bahati mbaya sana muda kubana na kushindwa kuonana nawe lakini iko siko milima haikutani bali wanadamu hukutana. SINGIDA/SWEDEN ha ha haaaa! Simon Hiyo picha uliyochorwa itunze ni ya uhasili kabisa nimeipenda kuliko zote kusema kweli. Na huyo demu wa mwisho mmependeza ..lol

EDNA 3:39 pm  

Pole MTAKATIFU hatukuweza kuonana, ila usijali ipo siku.....Alafu umefanana na Pablo Machine ni ndugu yako nini? Nanukuu: haki ya nani hakuna kimwana wa KISWIDI aliyefanikiwa kuvuliwa kificha nyeti safari hii:-Hahahaaaa Mtakavitu hujatulia wewe.

Yasinta Ngonyani 3:52 pm  

Haswa Edna umesema! wamefanana kwa kweli nimeangalia ni kama wandugu vile sijui kama unajua....

Rachel Siwa 4:39 pm  

kaka picha za kwanza ulikuwa mpole kumbe ulikuwa unakulamingo za kumsogelea yule kimwana anayepiga gitaaaaaaaa!baada ya hapo ulichangamka kaka hahahhahaha!

Innocent Kasyate 6:10 pm  

Wow, Mtakatifu nimefurahi sana leo. Yaani mapicha yamenikuna unavyoshusha kinywaji. Nahisi raha gani uko majuu alafu unakutana na chupa yenye chata ya mbuga ya serengeti.
Naona tayari christmas imeanza,du! ndio nimekumbuka kuwa kuna christmass. Baba ubarikiwe sana.

Simon Kitururu 12:18 am  

@Yasinta:Ipo siku tutakutana na nitautunza mchoro!

@EDNA: Pablo Machine sio ndugu yangu..... halafu mie mtulivu sana tu mtu wangu!:-(


@Rachel: :-)


@Inno: Inafurahisha kukutana na vitu vya Tanzania ughaibuni ingawa miye ni mtu wa SAFARI LAGER zaidi na huwa kwa kawaida nikiwa bongo sigusi SERENGETI!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP