Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mwisho wa siku labda YOTE HAYANA MAANA kama MTU hajayatafutia MAANA!

>> Wednesday, December 01, 2010

Kama tu ifahamikavyo kuwa,....
......hata PESA hazina maana kama hazijatafutiwa MAANA ili hata KIPESA,.....

......ziwe na MAANA.


Na ukipata kutambua maana ya KITU maishani mwako,.....
.... hata jambo DOGO KWA WENGINE hata lile la kusalimiwa tu na MTU,....
.....laweza kufanya siku yako au tu hata chaguo lako la kukatizia uchochoro wa MIGOMBANI STREET kufanya siku yako nzima iwe na MAANA.


Swali:
  • Si unajua hata MAVI YA KUKU ukiyatafutia maana yanaacha kuwa ni kinyesi tu cha kuku na KUGEUKA MBOLEA yenye thamani tu?

Na kama MTU,....
....afanyacho au alichonacho kwako HAKINA MAANA,......
.......hata kikiwa ni dini, FEDHA, nyumba ya thamani, kupendelea NDUGU au tu hata ELIMU YAKO,.....
....vyote vyaweza kuwa havina mchango HUSIKA kwako NA KWA HILO ndio maana hata kama ni VYA MAANA  bado kwako HAVINA maana.:-(

Swali:
  • Si unajua hata BIBLIA na KORANI  kwa mpagani  vyaweza kuwa havina MAANA kwa kuwa maishani mwake havina mchango uletao kwake  MAANA kama viletavyo maana kwa MLOKOLEA au tu mswalihina ?

Ndio,.....
.....bado MAANA  ni kitu fulani CHAAJABU na kunaweza kufanya mtu afikirie afanyalo ni LA MAANA/ajifunzalo ni LA MAANA,.....
......hata kama ni kwa kujifunza kwa kuona mtoto mzuri  BIKINI  aka AINA TU LA LICHUPI aogelealo nalo mtu inaleta maana kwa  aogeleaye ,....

 
......na kuamua INALETA MAANA hata kuoga na chupi pia katika bafu tu la kawaida nyumbani :-(

Ndio,......
..... maana HUFARIJI,.....
......ingawa kwa kupata maana LABDA kiletacho maana bado HAKINA MAANA kwa watu wengine,.....
....kitu ambacho ni MUHIMU kwa mtu KUJUA HILO hasa kwa kuwa katika maisha ya MTU cha muhimu sio watu wengine na MAANA ZAO katika ya wengine MAISHA yao.:-(


NI wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu Simba Wanyika watuimbie la maana kwa watu wengine katika-Shilingi yaua tena ni maua
Les Mangelepa wadai ambalo ni muhimu kwa wengine katika kibao - MimbaAu tu Jamuhuri Jazz Band waongelee tu tena -Shingo ya Upanga

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 11:57 am  

Ndio mkuu, mheshimiwa sana, hata waheshimiwa hatawakuwa na maana kama hatutawapa huoo uheshimiwa!
Ni kweli hata mavi ni kinyesi ndio maana kuna choo, shimo kubwa la kufanya yasionekane, kwani haya maana yakitoka tumboni kwetu, lakini kwa wengine ni mbolea, na in maana kubwa kwao! Na wadudu ni chakula, kwayo ni maana kubwa kwao.
Kwahiyo umihimu wa kitu ni matumizi yake, yakihitajika yana maana, na wakiwa wengi wanahitaji sana, hugeuka kuwa `alimasi' lakini pindi umuhimu ukikatika basi maana imeisha, kama binadamu ulivyo, umuhimu wako ni ukiwa hai, ukifa..mmmh, kaburi ni makazi yako!
Ujumbe murua mkuu, hata wale tuliosoma masomo ya nanihii tumenyaka kidogo!

SIMON KITURURU 3:22 am  

@M3:Yani hapo hata nyongeza sina Mkuu, isipo kuwa na wasiwasi tu na kauli kuwa MTU akifa umuhimu wake unaondoka ukizingati kuna wajanja kama akina Yesu , Nyerere,.....Idi AMINI.....nk ingawa wameshaanza kivyao bado mambo zao kuna ambao KIUMUHIMU yanawakunisha kichwa!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP