Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Pamoja na yote ,LABDA kunasababu BINADAMU hanusi vizuri kama MBWA na haoni vizuri kama DARUBINI!:-(

>> Friday, December 10, 2010

Kama BINADAMU angenusa vizuri ,...
...LABDA angestukia binadamu wote wananuka KITU FULANI HARUFU MBAYA  kisicho mwanana,...
......na angekuwa anaona vizuri kungekuwa hakuna ubishi kuwa KARIBU dunia nzima BILA KUSAHAU HEWA YAKE PIA kuwa  imejaa MADUDU na hakuna aogaye akaondoa UCHAFU wote ,...
....kitu kiwezacho kufanya MAISHA ya BINADAMU hapa duniani yawe ni ya BALAA zaidi ya yalivyo balaa hivi SASA.:-(



Swali:

  • AU?
  • Si unajua BINADAMU hata angekuwa anajua vizuri angalau AFYA yake kwa usahihi KABISA labda kuna NJEMBA kadhaa  uzijuazo zingeshakufa kwa MSHTUKO WA MOYO kwa jinsi tu zisivyo kuwa na AFYA NZURI na liwaokoalo ni KUTOJUA TU hilo kuwa hawana AFYA NZURI?



Kwa hiyo labda tushukuru tu HATA KWA KUWA hatuna macho ya X-RAY kwa maana ,....
...LABDA tungetishika kwa kuona TUSIYOYAONA SASA HIVI KWA MACHO YA KIBINADAMU ambayo hata kuyatumia kuchungulia mtu chupi yake NDANI YA SKETI ni KAZI,...
....kitu kifanyacho  TUISHI ANGALAU KWA  UAHUENI kuwa  HATUONI  angalau  yafanywayo MAJUMBANI  mwa waliojifungia MILANGO,...


....ambayo  labda siyo hata yale utegemeayo  ya KICHAWI au KIFARAGHA ZA KIKUBWA kwa kuwa ungestukia tu labda UNATISHIKA mpaka  na yale tusiyoyajua YA -  pamoja na yote  bado labda mpaka leo MHESHIMIWA FULANI  tumuheshimuye ambaye kaenda CHUMVI NYINGI  na SHULE kama ALIBUNI YEYE SHULE ,...
....au tu  RAIS FULANI umheshimuye KUMBE  akijifungia chumbani hasa mke wake asipokuwa NYUMBANI bado anachezea MDOLI aka MWANASESERE aliyewahi kumuibia binti yake MWENYEWE na kumficha kabatini kwake ili watu wakiondoka nyumbani AMCHEZEE,...
....halafu eti  bado  KWA KUNYONYA KIDOLE  hawezekani!:-(



Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Ijumaa na wikiendi NJEMA!




Hebu tu tubaki hapahapa TANZANIA ili Super Nyamwela na Luiza Mbutu waingilie kati kwa - Amani Africa



Au tu Msondo Ngoma wamalizie tu kiutu uzima na - Mtanikumbuka.

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 1:47 pm  
This comment has been removed by the author.
emu-three 1:47 pm  

Mkuu tungekuwa tunaona kama x-rays, mbona ingekuwa mambo..sidhani hata wale wavusha madawa wangefanyaje..hebu fikiri tungekuwa tunahisi zaidi ya sasa, ingekuwa hakuna uongo...ukitaka kuongea uongo, nishahisi...kungekuwa na amani, lakini...mmh kwa wale wasio na subira ingekuwa namna nyingine...unamtamani mke wangu...nitakuonyesha...! Mungu anajua zaidi ya tunavyofikirai sisi ndio maana akatupa yale yaliyo kwenye uwezo wetu!

chib 1:49 pm  

Habari ndiyo hiyo Kitururu.
Lakini watu wanapaswa kujua kuwa hata rais, askofu, shehe, na hata muhubiri maarufu wote ni binadamu tu, kuna nyakati fulani hususan za faragha wanakuwa kama vichanga :-(
Mkuu, weekend njema. Pata bia moja, bill nitumie kwa posta :-)

Ney 2:42 pm  

ha ha aaaaaaaaaaaaa sina mbavu yaani nimecheka sana macho yangekuwa kama x-ray au ultrasound nobody angefanya cheating kila mtu angekuwa innocent. Nakutakia weekend njema.

Simon Kitururu 1:22 pm  

@M3: Nanukuu``Mungu anajua zaidi ya tunavyofikirai sisi ndio maana akatupa yale yaliyo kwenye uwezo wetu!´´ - mwisho wa nukuu.

Nakubaliana nawe kabisaaa!:-(

@Mkuu Chib: Si utani! Halafu Bill ya ile Bia Moja nimesaituma kwa njia ya POSTA. Au weye ni wale ambao wamesahau matumizi ya POSTA kutokana na e-mail kuingilia ufundi wa kuandika barua kwa mkono?:-)


@Dada Ney: Yani ingekuwa kazi maana watu tungepofuka kwa kuona tusiyotakiwa kuona!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP