Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika jamii YA KINAFIKI mtu akificha TABIA ZAKE MBAYA eti hudhaniwa ana TABIA NZURI!

>> Thursday, December 02, 2010

Na kwa kuwa kuna YA KINAFIKI,.....
..... kuna mpaka WACHAWI waheshimiwao tu na wachukiao wachawi kwa kuchukuliwa siriasi UASKOFU WAO, ushekhe wao, ULOKOLE WAO kwa kuwa tu waonyeshayo watu huchaguliwa kwa uangalifu  kwa kuzingatia tu ni nini JAMII inafagilia.:-(Ndio,.....
.... na kuna MPAKA wateteao SIASA ZA UJAMAA hadharani ambao maadili yao ya KIBEPARI YAKIBUMBURUKA hata MAFISADI wenyewe hustuka na kustukia kumbe kuna NJEMBA  kwa wizi  zimezidi ukistukia ,.....

.... kama tu baadhi ya MALAYA ambao kwa juu juu unaweza kudhania ni BIKRA WA KILOKOLE  mpaka siku  wewe kama daktari wa sehemusehemu ustukie inakuwaje BIKIRA HUYU MTOTO WA GETI KALI mwenye MAPENZI NA KANISA  kila siku anakuja na ainaaina tofauti za KASWENDE na ndugu zake wengine kama akina gono zikiwa tu zina hari mpya na nguvu mpya ingawa MABWANA HESHIMA WAHUSIKA WA MTUNGUO KIASHERATI   hata siku moja kwenye BAIBO STADI  huwaoni na mahausi boy nyumbani hakuna.:-(


Swali:
  • Lakini SI INAKUMBUKWA  kwa kuficha TABIA MBAYA bado haibadili ukweli MTU anatabia MBAYA?
  • Na si kunauwezekano BINADAMU sasa wanazidisha KUFICHA MPAKA UNAFIKI umegeuka ndio SIFA ZA WENYE TABIA NZURI  hata kama uwezo wa kuficha ndio wanao?

Ndio,...
.... kwa kuficha TABIA MBAYA hata Rais BILL CLINTON kabla ya kudakwa na ushahidi,.....
.....kuna waliomdhania ni MHESHIMIWA mwenye tabia ya kutuliza kipele cha ngono kutoka kwa mke wake tu wa ndoa,....
.....kitu kimfanyacho Rais ZUMA wa AFRIKA KUSINI labda apewe utakatifu kwa kukiri ukimchekea hana noma na ikibidi anakuoa kabisa bila SIRI.


NI WAZO tu hili MKUU na usikonde kama WEYE NI mfichaji usije ukafichua mitabia yako ukafukuzwa kazi bure!:-(


Tubadili basi tena kwa msaada wa moja ya wanamuziki naowaheshimu sana tu BILL WITHERS ashuke-Lean on ME
Bill Withers alainishe pia na ndude-Ain't no sunshine when SHE is gone


Au Bill WITHERS amalizie tu na kitu-Use me

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Candy1 2:01 am  

Hahaha, basi nitaendelea kuficha makucha yangu...napaka rangi juu ila ndani mmh...nimesema tu! By the way "Lean on me" song is TIMELESS! I love love love it!

Fadhy Mtanga 5:56 am  

mkuu si unajua kuna wale waonekanao ni wasafi sana kwa kuwa wameuniga vyuti vya maana na kuficha harufu ya chupi ambayo haijafuliwa siku nne....ama mkuu ni kama tu akumbukaye kunawa mikono kabla ya kula hotelini wakati akiwa njiani alipenga kamasi kwa mikono na wala hakujishtukia kunawa kwa kuwa watu hawakumpiga chabo...
Mtakatifu kiukweli tabia nzuri huneshwa tu mbele za watu ndo maana utashangaa bingwa wa mihadhara ya kupiga vita UKIMWI ni bingwa wa kumendea vitoto vya shule kwa kuvidanganya na lift kwenye kiStarlet chake...kumbe na wewe umeshitukia mkuu? basi fanya kama Candy1 full kupaka rangi tabia yako ili hata binti Kidawa Cheusi Dawa aone wewe ni bonge la brazameni kwa kuwa tu una tisheti na jinsi unang'ara ingawa hakuna mtu ajuaye kuwa hutumiagi maji wala tp ukiingia public toilets nyakati za mchana

Ney Kitururu 11:21 am  

Umenifurahisha na mada ya kuficha tabia ha ha a a wanasema Tabia ni kama ngozi huwezi kuibadilisha kaka kwahiyo huwezi kupretend for life lazima kuna siku utajisahau duh! Tuko pamoja!

emu-three 12:44 pm  

Kuna usemi kuwa dalili za mnafiki ni hizi: akisema, husema uongo, akiahisi hatimizi, akiaminiwa haaminiki!
Sasa hata ufiche tabia zako kwenye nanihii, matendo yatakusuta! Ila kumnyoshea mwenzako kidole, ili hali vidole vitatu vyakuelekea wewe ni moja ya unafiki!
Mkuu hii mada mmmh, nawaza tu mkuu!

Yasinta Ngonyani 3:27 pm  

Haja bwana:-) au haya jamani:-)

Swahili na Waswahili 6:11 pm  

Kumcha Mungu si kilemba cheupe na si wote wanaosema bwana ni wakweli,usafi wa mtu si kuoga na kuvaa vizuri upo ndani yamtu!

SIMON KITURURU 3:18 am  

@Candy1: :-)

@Papaa Fadhy: Si utani natafakari ushauri wako Mkuu!:-)

@Da NEY: Tuko Pamoja sana tu mtu wangu!

@M3:Umenigusa kweli hapo mimi kwa kuwa hata sasa hivi yote uliyosema kuna watu naamini wanaamini ni mie nayefit ulichofafanua ni nani mnafiki!:-(


@Mtoto Mzuri Yasinta: Haya mwaya WEE haya tu!

@Rachel wa SWAHILI na WASWAHILI:Nakubali sana tu ulonena mtu wangu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP