Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TIBA ya WOGA wa mende au tu ya wa WATU wengine WATASEMA nini!:-(

>> Sunday, December 26, 2010



Woga kiboko,...
....ndio maana unaweza kuogopa BILA sababu!:-(

Woga ni kiboko,...
... ndio maana ASILIMIA kubwa ya WATU huogopa bila hata kuchunguza KIOGOPWACHO kina madhara kweli YAWATISHAYO matokeo yake unaweza kukuta kuna WAOGOPAO mende , FISI au tu MBWA kuliko BINADAMU WENZIO wajulikanao kwa kuua WATU hata kuliko MBWA na fisi na kufanya hivyo hata BILA za maana sababu.:-(





Swali:
  • AU?

Na TIBA ya woga wa MENDE,....
..... labda ni kumkabili MENDE na katika kuchunguza na kuukabili woga kitu kiwezacho kuwa tiba kwakuwa kwa kumkabili MENDE unaye muogopa unaweza kustukia katika kupigana NGUMI kwa mtu na mende kirahisi sio MENDE atashinda!:-(



Na ukichunguza yote yaogopwayo kama GIZA na sio mende,...
....unaweza kugundua karibu WOGA wote hutokana na kutofikiria hasa nini kinaweza kuwa gizani huko chumbani kwako ambako mwenye funguo ni wewe tu mwenyewe na ukastukia kunauwezekano vyote viogopwavyo MTU hana sababu za kuviogopa kihivyo kwa kuwa labda kitishacho NI HIYO TU HOFU kuliko kitu chenyewe KISABABISHACHO HOFU aka WOGA hasa kwa kuwa ukweli uko pale pale UKIKABILIANA nacho kuna uwezo mkubwa tu ni weye utakayeshinda.

Swali:

  • Hivi leo unakumbuka UNACHOOGOPA ni nini na umekibingilisha kucheki kuwa kina sababu kweli ya kuogopwa au unaogopa tu?
  • SI nasikia mtu aogope asiogope HATA KUTETWA siku ya siku ikifika hata ufanye nini utajikuta umewekwa kati ukisutwa hata umbeya wa enzi za BIBI na MASHOGA zake enzi hizo wakisukana mabutu?


  • Na hata ukiogopa si siku ya siku KUFA kuko palepale tu hata kama kwa kumuogopa MENDE umefanikia kumkwepa maishani mwako yote?


Ndio,...
...KWA BAHATI MBAYA,....
.... labda MENGI yastahiliyo TUYAOGOPE ndio HATUYAOGOPI na yale ambayo tulihitaji kutotishika nayo ndio YANATUTISHA,...
... kitu kifanyacho yale yastahiliyo KUKUMBATIWA ndio tunatoka baruti kuyakwepa na YALE YASTAHILIYO kuogopa ndio twayaingia mpaka chumvini kwa kutoogopa na kulamba visivyolambwa kama ICECREAM aka AISHIKIRIMU  vile-LOH!:-(



Na nimelikatiza hili WAZO Mheshimiwa nisije KUPITILIZA bure likazidi utamu!:-(



Hebu MZEE Yusuf na  Zanzibar Stars waingilie kati kwa -Najiamini



James Brown aseme-I'm BLACK and I'm  Proud



Herbie Hancock aturudishe mwaka 1975 katika kitu-Chameleon


Au tumcheki tu Lenny Kravitz asipokuwa mbele ya kipaza sauti akiimba na badala yake awe kwenye Drums katika wimbo huuhuu wa Herbie Hancock ujulikanao kama -Chameleon

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

nyahbingi worrior. 10:53 am  

mkuu simon,umeamuwa kubadilisha kurasa?ile kurasa ya kwanza imekwenda wapi?

Simon Kitururu 11:29 am  

@Rasta:Nilipata matatizo na ukurasa kidogo halafu maswala yake nilikuwa sija -save mimi na Mdau aliyenitengenezea ile kitu na ku-save katribu kila kitu kwake ilikuwa vigumu kumpata kwa hiyo ikabidi niuchakachue ukurasa ili kuudhibiti ukileta maringo.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP