Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa KAWAIDA aoaye zaidi ya MKE MMOJA KWA MAPENZI KAMILI kutoka MOYONI huoa WANAWAKE wasiofanana!:-(

>> Friday, December 24, 2010

Kuna uwezekano BINADAMU hana kipimo cha uhakika  kithibitishacho kuwa,...
....haiwezekani kwa MTU kupenda vyakula viwili vya aina tofauti tofauti kwa usawa,...
.... kitu kifanyacho WATU waamini kama wewe ni MPENZI  wa UTANDU SANA hauwezi kuupenda na UKOKO hivyo hivyo sawasawa kama idaiwavyo kama mtu anapenda sana UGALI hawezi kuupenda wali hivyohivyo kwa kipimo cha UPENDO sawa,....
... kitu kifanyacho watu waamini kuwa kama unampenda sana ASHURA kwa kuwa ana bonge la sura lenye MWANYA kama mfereji wa maji machafu na DIMPOZ kama kama  mashimo ya choo cha shule ya msingi ya jirani ihitajiyo msaada wa DANIDA ili choo kimalizike,...
.........
......basi huwezi kumpenda hivyo hivyo KWA MAPENZI SAWASAWA kimwana ASHA ambaye umpendeacho ni TABIA na  kiuno chake kama NYIGU mjamzito na MAKALIO YAKE aka SANGARA WAMO  kama masufuria  makubwa ya kupikia ubwabwa MSIBANI.:-(

Swali:
  • Kwani unauhakika UPENDO unapimika mpaka uamini aina tofautitofauti za mapenzi  yako KUMI kwenye mzani wa MAPENZI sio ngoma DROO?


  • SI ni kawaida hata kwa MPENDA magari  kununua magari ya aina tofautitofauti  kwa kuwa MAPENZI hutosha kupenda  zaidi ya PICK UP truck?


Ndio,...
....LABDA mapenzi ya MTU yanauwezo wa KUKUMBATIA upendo wa AINA NYINGI kiaina nyingi,...
.... ndio maana MTU MMOJA amepewa uwezo wa kupenda watu wengi wenye TABIA za aina nyingi TOFAUTITOFAUTI ,...
.... na hapa siongelei uwezekano wa kuwa mtu anaweza kumpenda MAMA YAKE sawa tu kiujazo na  ampendavyo SHEKHE wake amfundishaye DINI  na kumfanya ajisikie kuwa AHERA hata enda ,...
.....hata kama katika hilo KUNA wadhaniao kuna tofauti KIUPENDO.:-(

Swali:
  • Si nasikia kuna wadaio wanamapenzi tofauti kwa MAMA na kwa BABA waliowazaa kitu ambacho labda kungekuwa na mzani upimao tani za upendo labda ingegundulika hilo si sahihi kwa kuwa Mapenzi kwa MAMA hata kama ni tofauti bado = kwa mapenzi ya mwana kwa BABA?

Na samahani,...
.....labda kwa kuwa UMEPENDWA,....
.....weye unakuza uwezekano tu wa atakaye kuja KUPENDWA mwingine asiwe na LIPUA kama lako aka asifanane na WEYE kwa kuwa ni kweli DUNIA IMEJAA wengi wazuri na ukiacha wale wafananafananao na WEYE KIUZURI MWANANA ,...
... wapo  pia wengi tu aka CHUNGU MZIMA wenye sura na tabia tofauti halafu kwa bahati mbaya eti na kwa hilo nao WANAVUTIA na kupendeka tu.:-(

Swali:
  • Ukifuatilia uliowapenda tokea SHULE ya vidudu hustukiii labda umpendaye siku hizi ndiyo yule mwenye BONGE la pua?




Ndio,...
... UPENDO ni  KIBOKO,....
...na ndio maana kuna walitumiao PENZI kama kiboko kuwachapia wenzio na chamoto wanakiona!:-(

Naendelea KUWAZA!:-(

Hebu tumuachie Myahudi Barbra Streisand aimbe kuhusu wasichoamini WAYAHUDI katika-Silent night

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP