Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda KUNA maigizo KANISANI , maigizo katika GWARIDE la KIJESHI uwanja wa TAIFA kama tu ilivyo ni maigizo kwa WALIOVAA ULIMBWENDE watikisao tako MTAANI!:-(

>> Saturday, December 25, 2010

Ukiangali,....
...... kuanzia majoho ya MAASKOFU na WACHUNGAJI makanisani,....
..... mpaka mwendo wao  katika kutaka kuonekana ni watakatifu zaidi  labda  NI MAIGIZO tu kwa kuwa MUONEKANO wao  hauna uhusiano na neno  waumini walilolifuata lile la MUNGU.:-(





Hebu mchungulie PAPA BENNY  kabla hajaanza kuongea KITU katika mavazi na UTEMBEAJI wake na uniambie kifanyikacho hapa hakina uhusiano na VIFANYWAVYO na akina Mzee Jangala katika kudaka watazamaji ki-THEATRICAL a.k.a kimaigizo....



Ndio,...
....naamini MENGI yafanywayo na WAHUBIRI katika sehemu za DINI karibu zote nizijuazo,....
....hayana tofauti  sana na yafanyikayo kwa WAGANGA wa kienyeji katika kufanya vituko KUCHEZA MAIGIZO ili kukuweka mkao wa KUINGIZWA mkenge  ,...
......kwa  kuwa vingi ni vituko vya MAIGIZO TU ambavyo kwa mfano MAKANISANI havina uhusiano na NENO la MUNGU na kwa mganga wa KIENYEJI huwa wala havihusiani na tiba utakayo pewa ni kwanini MGANGA anatoa sauti za ajabu na kukuvalia mafuvu ya BUNDI au kibwaya cha ajabu ajabu katika MAIGIZO ya kukufanya uamini afanyacho kina ukweli  kwa kuwa kinakufanya ukae KISAIKOLOJIA mkao wakutishika au kujisikia unashuhudia kikweli NGUVU za KILICHO na nguvu zaidi yako.:-(


Swali:
  • AU?
  • Unafikiri MAJOHO ya WAHUBIRI neno la MUNGU pamoja na sauti zao walizojifunza kutolea NENO LA MUNGU vina uhusiano na nini hasa MUNGU anataka kusema?



Tukiachana nahilo,....

...... na  tukiangalia wafanyayo WANAJESHI kwenye magwaride ya KIJESHI  mpaka ya KUPIGA KWATA mpaka VIATU VINACHAKAA SIKU MOJA kama sio mpaka kuruka juu mbele ya JUKWAA LA WAHESHIMIWA,...
.....hasa wakati wa AMANI ,....
....unafikiri sio MAIGIZO tu wafanyayo na YUNIFOMU zao ili WANANCHI waingie mkenge kuwa mpaka TANZANIA inaweza kulidindishia hata jeshi la Africa Kusini kama likileta KIBEZI  tu kama cha JESHI la MAREKANI,...
.....kitu ambacho inaweza kuwa ni ALINACHA ukizingatia hata RADAR yenyewe mtumba wajanja walio kula dili kuna uwezekano ni moja ya pambo tu  kama mapambo mengine ya uwanja wa MAIGIZO kabla MZEE JANGALA hajaingia kuigiza?




CHeki tisha toto za wanajeshi KOREA KUSINI.....



Tukiachana na hilo.....

..... bado  nadhani kuna atakaye kubaliana nami kuwa,....
...... kuna watu wana mwendo wa MITAANI kama ilivyo kuwa kuna nguo wazivaazo tu MITAANI kwa kuwa wanategemea kuangaliwa na watu kama tu walivyo wenye nguo maalumu CHUMBANI na vitendo tofauti kama ni a ni kuangaliwa na mpenzi  ,....
.....kitu kigeuzacho wafanyayo mtaani KAMA CHUMBANI katika MWENDO na vitendo kuweza  kukwalifai kama MAIGIZO tu .lwa kuwa kihalihalisi CHOONI kusiko na washuhudiao mambo huwa tofauti.:-(



Swali:
  • Unafikiri umzimiaye kwa mwendo na sauti OFISINI ana mwendo uleule na sauti ileile nyororo katika choo cha ofisi aliko pekee?


Nawaza tu kwa SAUTI Mheshimiwa na wala usikonde!:-(


Hebu Tabu LEY arudie- SARAH




Jacob Desvarieux aingilie kati na-Mwen malad aw


Au tu naye  Papa Wemba amalizie tu tena kwa kinu-Oldies are goodies

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP