Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

JICHO katika MAISHA lisipozoea KUONA watu wafananao NAWE wakila KUKU kwa mrija,....

>> Friday, December 03, 2010

Usipoona WAFANANAO nawe  hawako JELA,....
....yasemekana unaweza kudhania WATU kama wewe JELA hawaendi!:

Ndio,....
....BINADAMU hufananisha,...
....na wafananao na wewe JAMII ikiwaitaita ni WAREMBO,...
...ni rahisi na wewe kuamini kuwa ni MREMBO kama tu wafananao na SISI  wakidhaniwa ni WAVUTA BANGI,...
... uwezavyo kirahisi kufikiri WOTE kama sisi KIMFANANO  tunavuta BANGI.:-(

Swali:
  • AU?


Katika kuuingia KIUNDANI uchi wa HOJA kimnyambulisho:

Inasemekana KISA cha WANAWAKE wengi  kutokuwa  MABOSI au tu VIONGOZI  hata kwenye SIASA Duniani,....
..... hutokana na ukweli WANAWAKE wengi hudhania WAO sio VIONGOZI MATIRIO kwa kuwa tokea MAJUMBANI KWAO  walikua BILA KUONA WANAWAKE WAFANANAO NAO wakiongoza kwa kuwa tokea huko MAJUMBANI  ni BABA MWENYE NYUMBA aliyeitwa KICHWA CHA FAMILIA na kwa hilo labda aliongoza mpaka katika kupewa MINOFU minono ya KUKU   yeye ,....

......tukiachilia mbali kuwa  hata MAMA MWENYE nyumba alijua  ni HILO LIBABA KWA KUWA NILIKIONGOZI  ndilo liamualo ni muda gani MAMA MWENYE NYUMBA HUYO  hata kama kachoka ,....
.... itabidi  tu alikatikie KIUNO.:-(



Na kwa WANAWAKE WEUSI  TII   kutokana na kutokuwa wengi hata katika MAMODO a.k.a wauza sura  UGHAIBUNI  wasifiwao KWA UZURI  kumefanya WANAWAKE WEUSI  ughaibuni mpaka KISUMU ,KENYA  katika swala la nani ni MZURI ZAIDI,....
.....yasemekana kuingia unyonge  eti kwa kuwa wao NI  WEUSI TIII  KAMA MIMI hasa kwa kuwa MASUPA MODO wengi wasifiwao sana kwa UZURI ni WEUPE au kule KISUMU KISIMANI ambako Binti ya Mheshimiwa Othrong'ong'o anateka maji ,....
...DEMU  mzuri anaye windwa zaidi kuliko wote  kwa kudhaniwa ni MZURI huwa anakuwa ni YULE MWEUPE  angalau kiuweupe wa KIMAJIYAKUNDE.:-(

Swali:
  • Na si umewahi kusikia karibu asilimia 90% za picha zote za MALAIKA WATAKATIFU duniani kwa kawaida huonyesha MALAIKA WAZURI sio wale WEUSI?

  • Na si umewahi kusikia kwa kuwa WENGI wajulikanao kuwa na akili sana DUNIANI  huwa ni WAZUNGU na WAASIA kitu hicho kimefanya  watu wengi wasio WEUSI kudhani WATU weusi ni HAMNAZO Mkichwa kwa kukosa tu  WENYE akili WEUSI wakufananisha ambao wanasifa DUNIANI?
  • Si inasemekana hata kisa cha VIONGOZI  WABAYA kujirudia rudia  AFRIKA ni kutokana na kuwa MIFANO MINGI ya wafananao na viongozi wapiya AFRIKA huwa ni wale waliotangulia ambao NI WABAYA   kama ndani ya choo cha shimo cha STENDI?



Ndio,...
.... KWA KUTOONA mtu anaye FANANAFANANA na weye katika MAZURI,....
.... inaweza kusababisha mpaka WEWE MZURI kutojiamini kuwa ni KWELI MZURI, weye MWENYE MIAKILI kedekede kuanza kudhania ni angalau kwa mbaaali kuwa ni MJINGA kisa unafanana na watu wenye kujulikana NI WAJINGA , yule MJINGA KIKWELI kama uharisho kudhania ANAMIAKILI KOCHOKOCHO  kisa anafananafanana  TU na akina Albert Einstein au tu angalau Rais Julius Kambarage Nyerere wajulikanao kwa MIAKILI,...
...na HAO KENGE WAKUBWA kujiamini kweli kuwa WANAMIAKILI korokocho.:-(

Swali:
  • Lakini unafikiri Rais Nyerere kiakili alikuwa MKALI kweli wa HESABU kama alivyokuwa bingwa wa KUTOA HOTUBA?

  • Na je unafikiri Albert Einsein angekuwa GWIJI wa ngeli za KISWAHILI Kijiniasi?

Ndio,....
.... labda wafananao na wewe WANAHITAJI mfano wako ili wajiamini kuwa wanaweza KAMA WEWE,...


... kama tuonavyo MAFISADI wajulikanao TANZANIA waonyeshavyo mfano KWA KUPATA WAFUASI HARAKA SANA wenye UFANISI katika KUFISADI,...


...na kutoa funzo kuwa hata katika  WIZI unawezekana KUFANYWA kwa ufanisi  UKIPATA MFANO IMARA wa AFANANAYE NAWE bila kujali KABILA la mtu kwa hiyo wewe kama hutoki kabila la WATANI ZANGU WACHAGA jua kuwa ukitafuta MAROLI MODO wa kuiga katika kabila hata lako tukiondoa wale ufananao nao ,...
...waweza ibuka tu BONGE LA MWIZI kiunadhifu kabisa hata TANZANIA.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na IJUMAA na wikiendi njema MKUU!

Hebu MAD ICE alainishe mpaka kwa KISWAHILI mfukuto wenye jina -Te AMO





Au tu STING ajaribu tena KUUJAZZIFAI wimbo wa NGULI Bill WITHERS uitwao- Ain't No Sunshine When She's Gone



Au tu BUJU BANTON aingie ghafla na kubadili mchezo kwa ndude-African PRIDE

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 5:25 pm  

Mkuu, weekend njema

Simon Kitururu 10:37 pm  

Wewe pia Mkuu! Asante kwa kunikumbuka mtu wangu!

Yasinta Ngonyani 9:51 pm  

haya bwana! wikiend njema MT.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP