Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo katika wa wanawake uchokozi: Eti WANAWAKE waliosoma sana huogopwa na NJEMBAZ!:-(

>> Thursday, December 16, 2010

Nimesikia kuna wanaume LUKUKI,...
....moja ya  kitu kifanyacho waamue MTOTO MZURI hafai kuoa,...
... ni  kiwango chake kikubwa cha  SHULE yake.:-(

Ndio,...
...inasemekana wanawake walioenda shule sana NI WASUMBUFU hasa kwa kujifanya MACHINOO aka wanajifanya wanajua KILA KITU kitu kifanyacho kisa KIGOLI ana PHD ya KEMIA  mwanaume anaweza akajikuta anabishiwa na kufanywa mjinga katika kuongelea hata  JIOGRAFIA ya tako  kama tu abishiwavyo ile JIOGRAFIA ya nchi.:-(

Ndio,...
...inasemekana WANAWAKE walioenda sana SHULE ndio wabishi  zaidi  KUITWA CHUMBANI hata katika maswala ya kutoa CHAKULA CHA USIKU ghafla kisiri kabla watoto hawajalala na KWA BAHATI MBAYA  sio kwa kama ufikiriacho ni MAADILI ndio kizuizi kwa kuwa WATOTO HAWAJALALA - ila ni kwa kuwa tu  wanadai MWANAUME hawezi kuwageuza KIFAA cha STAREHE  a.k.a kiburudisho murua wakati wao wasomi na baada ya siku ndefu kazini  HAWATAKI BUGHUDHA kwa kuwa wameshafanya kazi ofisini zile muhimu sana za kujenga nchi!.:-(

Ndio,...
...inasemekana wanawake wasomi sana MATAKWA YA MUME huwa hayana kipaumbele kama matakwa ya OFISI  au tu nchi!:-(

Swali la kizushi:
  • Kama ni kweli kwanini WANAUME wasikwepe  WANAWAKE wa namna hii ikiwa wale waliofundwa kuhudumia  MWANAMUME kwanza au wale wategemeao tu kila kitu kuletewa na BABA WATOTO wapo na wanaadabu HATA KAMA HAWAJAENDA SHULE na wakitekenywa tu wanakubali hata kama kwa kutoandaliwa vizuri itauma na michubuko SEHEMU SEHEMU inaweza ikatokea?
Na inasemekana JAMII ya siku hizi iliyoenda shule,...
....inasahau kitu kwa kutotetea SHULE za MAADILI  ya zamani yaliyofunzwa na shule za elimu DUNIA ya WATU  waliojua mazingira na maadili yafaayo WATANZANIA ,..
...kwa kuwa tu eti WATU katika  JAMII WANAKWENDA shule hizi za kisasa zilizoletwa na MKOLONI siku hizi,....


.....ambazo pamoja na mazuri yote ziletazo ila bado HURUKA  kitu ambacho WATANZANIA wenyewe walitakiwa wakiboreshe kutoka katika elimu za jadi ambacho kilikuwa NA MAZURI YAKE ambayo misingi yake inge neemeshwa yangetatua matatizo YANAYOENDELEA kujitokeza au tu KUIKUMBA JAMII kisa jamii inaiga yote kutoka nje SIKU HIZI  kutoka katika elimu za NJE  au tu mambo ya jamii za NJE na KUJARIBU kuacha hata yale mazuri YA JADI  kisa yanaonekana ni ya JADI zaidi kwa hiyo ni ya KISHAMBA  ambayo LABDA ni ya MSINGI kwa JAMII ya KITANZANIA  na yangeboreshwa na sio KUACHWA KABISA yangesaidia sana tu MWANAMUME na MWANAMKE wa KITANZANIA  sebuleni , chooni ,..... mpaka CHUMBANI katika MAISHA yazidiyo kupoteza MAADILI na yageuzayo mtu awe na tabia kama za MBWA malaya.:-(


Swali zaidi la uchokozi:

  • Kwani nani hapendi URAHISI WA MAMBO katika DUNIA HII yenye maisha magumu halafu ,HALAFU  twafa?
Ndio,...
....nasikia WANAWAKE waliosoma sana ,...
...kuna NJEMBA zinawakimbia,...
...na nasikia kuwa LABDA sababu zao labda ni za MSINGI kinamna.:-(

Ndio,....
.....kunawezekana kuna kikubwa WAKIKOSACHO hawa njembaz,...
...kwa kukimbia WATOTO WAZURI wasomi wajuao kuongea mpaka YESYES NO mai milk is stending,....
...kitu kifanyacho JAMII nzima kupungukiwa na kitu.:-(




Na ni ndio,...

....hili NI WAZO tu la KICHOKOZI TU  mwaya NA wala usikonde MWANAKWETU na kuanza kunisuta bure NIKALIA!:-(



Tubadili wazo basi  kwa kuwapata De la Soul   katika mdinyo-BABY PHAT





Au tu De la SOUL na CHAKA KHAN warudie-ALL GOOD



Au tu badili tu kabisaaa na kurudisha AFRO BEAT uwanjani kwa FELA KUTI akirudia-Lets Start

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 5:08 pm  

Ni vigumu kwa mafahari wawili kuishi zizi moja!

Simon Kitururu 5:17 pm  

Si utani Mkuu Malkiory!

Yasinta Ngonyani 6:54 pm  

Kaazi kwelikweli:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP