Tuesday, June 30, 2009

Kwa mara nyingine na ni SIKU NYINGINE!

MATATIZO ni yale yale,...
.....ingawa SIKU ni NYINGINE.

KWA KUWA ni siku nyingine,...
....matatizo yaleyale hudhaniwa ni mapya ,...

.....kwa kuwa ni SIKU NYINGINE.


Kwa kuwa WEWE si WATU WENGINE,....
.... baadhi ya MATATIZO YALEYALE kwa wengine,...
.... WEWE waweza kudhani ni MAPYA kwa kuwa umeyagundua SIKU NYINGINE.


Na kama unajifunza KUTOKA KWA WENGINE,...
....matatizo YALEYALE ukiyafumbia macho HUJIFUNGUA MTOTO,...
... na siku moja unaweza ukaamka na tatizo JIPYA kweli kwakuwa ni SIKU NYINGINE.


Lakini MATATIZO ndio SIRI ya UFUMBUZI wa TATIZO,...
... na kushughulikia MATATIZO ndio SUKARI YA MAISHA kama ufumbuzi wa TATIZO,...
.... na hata kama ni kweli UTAFUMBUA FUMBO la kiini cha TATIZO siku nyingine.

Na leo ni SIKU NYINGINE,....
... na kama unadhani huna TATIZO basi wewe maisha yako yaliishia jana,...
... na hukufika leo SIKU NYINGINE.



Swali:
  • AU?
NI wazo tu KINGUNGE na NIMEACHA kukuzingua!:-(

Ngojea Scarface na 2PAC wakukumbushe-Smile


AU tu THE POLICE warudishe gurudumu nyuma zaidi katika ...- De Do Do Do De Da Da Da


Katika kuongelea BILA AIBU angalau UWEZEKANO wa kuwa MIMBA ya KUKU ni YAI!

Tukiachana na swala la KUKU MJAMZITO....
....... baada ya KUKU kufanya TENDO LA NDOA kama BATA,.....

.....tuongelee binadamu kiduchu basi!

Kwa BINADAMU kuna TAMADUNI, MILA na DESTURI zifanyazo tuamini KUWA NI ukweli kuwa swala la UJAUZITO ni la wakubwa,....
..... ndio maana binadamu akiwa mtoto hudanganyika kuwa watoto wananunuliwa duka fulani au kuna ndege anawaleta hata kama anayemsimulia BINADAMU MTOTO HUYO , ana MIMBA.:-(

Na ,...
.....kwa kuwa jamii inadai kuwa MASWALA YA UJAUZITO ni maswala ya faragha kuna ambao wamepata mimba kwa kutojua MASWALA YA mpigwa chini huvimba JUU.

NDIO!
Tamaduni zetu wengi zinatufanya tuepuke kuzungumzia mambo fulani:-(

Na ujuzi wa asilimia kubwa ya vijana siku hizi ,....
......ni wakujifunza wenyewe KUPEKECHA ingawa kuna washangaao kwanini RIJALI kila siku akiingia mtandaoni akilini akiona KIBONYEZO ''search ''hakawii kuandika mbele yake neno ''SEX''.

Ndio!
Asilimia kubwa ya WABONGO niwajuao wamejifunza maswala ya KITENDO CHA KUUJAZA ULIMWENGU wenyewe kwa kuwa ndugu na hausigeli hawakuviongelea kwa kuwa MILA na DESTURI ZIMEWAFUNGA mdomo hata WAZAZI.:-(


Na tatizo kubwa katika hili ni kwamba,....
..... kama huna MUONGOZO itabidi ujishughulishe mwenyewe KUPATIA na kwa bahati mbaya kwa kujifunza bila MUONGOZO waweza kujikuta USHAZOEA KUKOSEA matumizi ya NYETI.


Kumbuka,...
... apataye MIMBA wakati anapata MIMBA kunauwezekano MKUBWA alikuwa anafikiri anapata URODA tu a.k.a MIKASI na sio alikuwa ANAMIMBISHWA.:-(

Kumbuka,...
..... mara nyingi BEBERU LIKIPANDA huwa halifikirii matokeo yake ni kumpa mimba KIMWANA mbuzi.


Na kumbuka ,....
.... mwenye mimba anapendeza kwa kuwa unajua ana mimba LASIVYO ni kweli mwenye mimba huwa ana tumbo KUBWA a.k.a BOMBA LA TUMBO na HUWA anabadilika MWENDO.

Kwa hiyo,...
..... jihadhari kumuuliza MWENYE TUMBO KUBWA asiye na MIMBA maswala ya UJAUZITO kama hutaki kufyonzwa KABLA hujashushiwa bomba la TUSI lenye uzito wa KILO KADHAA lifuatwalo na bomba la KOFI .Na kama wewe mfupi JIHADHARI kwa kuwa labda pia utapewa bomba la konzi lenye KILO TATU na NUSU hivi kwa kukosea wa KUMDADISI.

Na ni kweli,....
..... ukikutana na mwanaume akukumbushaye MWANAMKE mjamzito, basi inasemekana huyo ANAKITAMBI kitu ambacho SI AFYA kama tu toto dogo lenye tumbo kama mimba linaweza kuwa lina KWASHAKOO , UTAPIAMLO ,nk.....
........ kitu ambacho SI AFYA!:-(



Na ni kweli,...
..... MIMBA ni KIBOKO ndio maana UMEZALIWA.:-(

Swali:
  • AU?

DUH!
NALIKATIZA wazo hili kabla ya KUONGELEA kuhusu MIMBA ya kuku bila KUOMBA ruhusa ya KUKU!
Swali:
  • Hivi kweli umesoma mpaka sentensi hii hapa katika SWALA HILI lenye uwezo wa kuwa ni la KIJINGA ?
  • Unafikiri lini katika ukuaji wako ulistukia MIMBA sio KITAMBI na KITAMBI sio MIMBA?
  • Unafikiri kungekuwa na uwezekano binadamu wasingehusudu KUTAGA kama kunguru ili kukwepa kuvaa MATENITE DRESI ingawa kasheshe lingekuwa ni zamu za hausigeli kuyatamia mayayi wakati bingwa YUKO kwenye KICHENI PATI?

Kumbuka ni wazo tu NA NIMELIKATIZA nikiwa nakutakia KILA la KHERI katika LAKO LIBENEKE!


Ngojea Kenny Roggers abadili hali ya hewa kwa kitu- You are so Beautiful



Au tu BONGO MAFFIN watukumbushe- MAKEBA

Monday, June 29, 2009

JINSI ya kumuibia MJANJA!

CHAMSINGI,...
...mfanye AAMINI unaamini kuwa yeye MJANJA!

Swali:

  • AU?
Kumbuka kutofautisha kuiba na KUPORA,....
...... na uwezekano wa kubwengwa ukidakwa kwa kukosea staili ya kumuibia MJANJA.


Nalikatizia hili WAZO hapa kwanza labda halikufundishi kitu kama wewe sio MWIZI!:-(

JUMATATU njema KIJEBA na ikiwezekana USIIBE nasikia ni DHAMBI!


Au turudi KENYA Safari SOUND BAND wakumbushe- MAMA LEA MTOTO WANGU..


Au tu GREGORY ISAACS abadili kwa -Love is OVERDUE..

Sunday, June 28, 2009

KATIKA kukumbuka TOTO zuri LIKUTISHALO ni kweli NALO bado linaenda HAJA KUBWA a.k.a KWA lugha ya kisasa -KUNYA!!:-(

Labda ni KWELI,...
...hakuna BINADAMU mjanja INGAWA kuna IDAIWAO ni WAJANJA.

Na kama kuna UJANJA,...
...basi MJANJA hajazaliwa:-(

Na kama unadhani WEWE ni mjanja,..
... jaribu kuhairisha KUNYA ukibanwa TUONE.[samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha!:-(]


Swali :

  • Unafikiri akutishaye anakutisha nini ikiwa kila BINADAMU unajua ni SPESHO?

NAACHA wazo na samahani kwa WAZO hili hapa MAWAZONI Bingwa, NA KATIKA HILO kumbuka hili ni wazo tu KIJEBA!:-(
Kwa mara nyingine JUMAPILI njema BINGWA!

Ngojea Jermaine JACKSON adai...-Do What You Do


Au tu Jermaine Jackson adai tena-Sweetest sweetest

STORI za JUMAPILI kama tu za JUMANANE za Kalumekenge!

KalumeKENGE aliamka,...
..... na kuachia bomba la M-hayo kabla ya kujinyosha na kujamba kidogo.

Ndio ,...
....ALIAMKA halafu baadaye siku ilipoisha AKALALA kama wewe TU!:-(


Ndio,..
.... labda kuna MUDA ndani ya SIKU kwa kuwa yuko hai alifanya jambo AFIKIRIALO ni KUBWA akilini mwake kabla hajaenda MSALANI kama wewe TU!:-(


DUH!

Swali:

  • AU?
  • Hivi kwani JUMAPILI inarangi tofauti na JUMANNE ,na ukisikia njaa, njaa ya JUMAPILI ni tofauti na ya ALHAMISI?

DUH!

Ngojea NIACHE wazo hili na labda ni la kijinga!:-(

JUMAPILI njema KIJEBA!


AU ngojea MR BEAN aboreke KANISANI kiduchu katika....-Church bore



Au tu tumchungulie MSENGE akishughulikiwa KANISANI na wajanja...-Church Rids Gay Demon....

Saturday, June 27, 2009

Ushawahi KUTHUBUTU?

Na,....
..... hapa siongelei swala la KUTHUBUTU kwako KUNYA,(samahani kwa lugha ya faragha), namaanisha kwenda HAJA KUBWA, kwa kuwa hata KUKOJOA(samahani tena kwa lugha ya matusi), namaanisha hata HAJA NDOGO unafanikisha ukiwa PEKE yako CHOBISI shwari.:-(


Ukitaka kujihakikishia una nguvu za KUTHUBUTU,...

.... jaribu KUTHUBUTU angalau KUJAMBA mbele za WAHESHIMIWA au WAGENI ambao HUJAWAZOEA kwa MAKUSUDI!:-(

Swali:

  • AU?

Kuna uwezekano LABDA kama UNGETHUBUTU sasa hivi usingekuwa unanisoma na ungesha JIUA zaaamaniiiii HATA kwa kula sana hata MAGIMBI au tu kwa kudai kama nidaivyo MAISHA MAGUMU!:-(

DUH!

Swali:
  • Au?

Thubutu lakini kama unataka kuwa WEWE na sio kuwa WATU wakufikiriavyo wewe kama tu MUUZA SURA kwakuwa una BOMBA la PUA ingawa MWANIWANE una MIAKILI MINONO na TABIA KIJEBA!:-(

Swali:
  • Unafikiri kama wajidanganyao KUWA NI wazuri wauzavyo sura , UNAFIKIRI wewe huuzi tabia INGAWA unamaaeneo mazuri KIFICHONI yenye TABIA MBAYA YAKITEKENYWA hata kama BADO yana nywelenywele NJOLINJO?
OK Bingwa nikiacha KUKUZINGUA na UJINGA;
SWALI:
  • Unauhakika umewahi kuthubutu na bado ukabakia MASIKINI?

NAACHA wazo BINGWA!:-(

Ngojea TUKAECHINI ili TUJIFUNZE watoto WADOGO wanasemaje kuhusu KULA KONI katika-Oral Sex the New Goodnight Kiss...


Au tu tusikilize utunzi wa Michael Jackson na Lionel Richie katika-WE ARE the WORLD..


KWA MARA nyingine ASANTENI WOTE! Mkiwemo hawa kwenye picha zangu za juzi ya MTONDOGOO....

Photobucket

Photobucket


Photobucket



Photobucket




Photobucket



Photobucket


Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket


Photobucket


Photobucket



Photobucket


Photobucket


Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket


Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket

Friday, June 26, 2009

R.I.P Michael JACKSON!

Kwaheri Mkuu na Asante kwa muziki kama HUKO ULIKO unanisikia BINGWA!

Mie bado wako Mshabiki.

Ciao!






Thursday, June 25, 2009

UKIWA na uhakika wa KULA njaa haiumi HARAKA!Lakini!:-(

Ukiwa na pesa za GARI,...
... mwenye gari hakuumizi KICHWA.


Ukiwa huna uhakika wa gari na unauhakika wa MKWECHE,....
....mwenye gari , ingawa ni mpaka uwe unataka gari ,ANATISHA!


Ukiwa na uhakika UTAFIKA,...
.... waliotangulia SI WAJANJA.


Ukiwa na wasiwasi na uwezo wako wa KUFIKA,....
..... unaweza mpaka kuanza kufikiri UTAFIA NJIANI na waliotangulia kwako WANATISHA.

Ukiwa na mke MZURI,....
....wenye wake hawakutishi kwa kuwa unaujua MKENGE waliouvaa.

Ukiwa na mke MBAYA,...
... wake wa wenzio wanavutia MNO kwa kukosa KASORO na jicho la ubongo WAKO litabunia MPAKA umbo lao hata la kabla hawajavaa.

Swali:

  • Hivi kweli kuna mke mbaya duniani?
Ukiwa na MUME MZURI au MBAYA mie sijui nini kinatokea na SAMAHANI kwa KUKOSA UTAALAMU wa HILO!

Ndio,...
.....Ukiwa na uhakika leo hata kuhusu ya kesho,....
... walionayo leo HAWAKUTISHI.

Tatizo ni;
...Ukiwa na uhakika leo, HUO NI UHAKIKA WA LEO,....
.....na labda kesho utagundua;
  • Pesa zako zikutiazo kiburi leo hazitoshi kesho kununulia hata mkweche.
  • Uhakika uliokuwanao leo kesho haupo, na ghafla huna uhakika wa hata kufika kesho kutwa ya KESHO.
  • Kakitu ambako katafanya MKE wako mzuri leo, USTUKIE kumbe tokea ZILIPENDWA alikuwa mbaya.


NA LABDA,....
....
Kibinadamu, ALAYE SASA HIVI ndiye mwenye uhakika ANAKULA,..
... na siye wengine HATUJAPANIKI TU kwakuwa TUNA MATUMAINI TU kuwa baadaye TUTAKULA.

Uzuri ni kwamba ,...
...BINADAMU huendeshwa na TUMAINI,......

.... ndio sababu ukiwa na kibano LEO unadhani labda utafaidi mbinguni WAKATI labda KIBANO CHAKO unachodhani ni KIBANO LEO ni KILE chakutamani unywe GONGO NA WASHIKAJI halafu usinyimwe TENDO LA NDOA a.k.a URODA a.k.a MIKASI a.k.a MATUSI a.k.a UASHERATI hapo baadaye CHOBISI , ingawa LABDA mambo yote HAYO umeshafundishwa na DINI YAKO kuwa MBINGUNI hayapo, NA kule mambo yote ni JUISI kwa MAZABIBU halafu KUIMBA kwa SANA TU na MALAIKA , halafu kwa bahati mbaya hakuna KUCHOKA.:-(

DUH samahani kama nakukwaza kwa kuwa unadhani nakufuru!:-(


LAKINI,...
....UBINADAMU ni NISHAI KWELI kwa kuwa kama wewe ni BINADAMU na SIO JINI, labda KWAKO hakuna lenye uhakika!

NAACHA wazo na KUMBUKA ni WAZO TU na nakutakia kila la kheri katika kukuza lako TUMAINI.
Damn , I am depressed now.(NA samahani kwa kuingizia ung'eng'e KIDUCHU!:-()

PEACE!

Tupitie Kenya kidogo Les Wanyika wadai - Dunia Kigeugeu



Au tubaki tu Kenya Salim Junior adai-Ni sorry Muno..

MAFISADI wa CHANGU changu na CHAKO changu!

Ukiwaangalia WANASIASA-mafisadi,...
... utastukia wanadhani CHAKO CHAO,....

..... KAMA HUJASTUKIA tayari KWENU wanadai ni KWAO.

Afadhali na MALAYA-mafisadi wa NGONO,.....
.....ambao CHAKO hukitakakiwe CHAO,....
....na ukiishiwa nakukistukia CHAKO ndio waweza kustukia hawakukuacha mtupu na kwa UKARIMU walikuachia angalau GONJWA LAO.


MAFISADI wa UNDUGU,....
.... ukifanikiwa wewe ndugu YAO,....
.... ila ngojea UCHACHE ndio ustukie wao si ndugu kwa KUSIKIA wadaivyo hawakujui na matatizo YAKO si YAO.



Na wale MAFISADI wa URAFIKI,...
....CHAO ni CHAO na CHAKO ni CHAO,.....
.... na unaweza usistukie mpaka usiwe na CHAKO.:-(


Swali:
  • Lakini kwanini ujilimbikizie CHAKO kwa kuwa ni CHAKO KIDUDE ili iwe nini kama HUKITUMII kidude?

  • Unakumbuka ukifa hata uwe na chupi ngapi labda ni moja tu utazikwa nayo halafu makorokocho yako yote mengine utayaacha?




NAACHA wazo!

Ngojea AEROSMITH wadai..-I don't wanna miss a thing

Au tu ALAINE abadili bila kubadili hali ya hewa...-Make me WEAK

Wednesday, June 24, 2009

SABABU za mlevi KUYUMBA!

NI kweli,....
.....Ujanja wa asimamaye au kutembea BILA KUYUMBA uko MASIKIONI na sio miguuni kama idhaniwavyo.


Ndio,...
...SIKIO kazi yake si KUSIKIA PEKEE kama unakumbuka HATA maswala ya balansi, bingwa ni SIKIO.

Hebu tujikumbushe BAOLOJI ya sikio kwa ndani katika NJONJOLINJO...

Semicircular canal















Exterior of labyrinth.














Inner ear illustration showing semicircular canal, hair cells, ampulla, cupula, vestibular nerve, & fluid


USITISHIKE,....
...... yote ni katika kukukumbusha kwa KUTEMBEA KWAKO KWA MARINGO kumbuka NI SIKIO linakusaidia kufanya hivyo NA SIO TAKO kama wewe kwa mwendo wako wa maringo huwa unatingisha tako!:-(


Halafu ni kweli,...
.... sababu kubwa ya Mlevi kuyumba ni kwamba KALEWA.

Swali:
  • AU?
  • Kwani wewe ulifikiri hadithi hii nitaisimulia kwa urefu gani?
  • Hivi sasa hivi sikio lako ukilichokonoa halina NTA ingawa sikioni mwako hakuna nyuki?

NAACHA wazo MKUU na NAKUTAKIA siku njema KINGUNGE katika libeneke!

LAKINI kama unamuda ngojea Waziri wa Utamaduni wa Brazili a.k.a Gilberto Gill atuburudishe tena kwa- Aquele Abraco

AU Ngojea tu tena Gilberto Gill adai -Waiting in Vain..

TAFADHALI usisome STORI HII ya SIRI za MHESHIMIWA aziongeleazo CHUMBANI na kujifanya kazinunia HADHARANI!:-(

ANAYEJIHESHIMU ,...
......huaminika kuwa HUWA ndiye asiyoyaongelea MAMBO kama hivyo HADHARANI,....

.....ndio maana kuna wasahauo WAITWAO WAHESHIMIWA wengi ndio wateteao ujinga HADHARANI.


MHESHIMIWA ,....
..... inasemekana HAVAI HIVYO hadharani,....
.... ndio maana ni bingwa zaidi ya WANAMAZINGAOMBWE kwa UTETEZI wa NGUO kwa MANENO hata wakati akiwa anawazia YALIYOUCHI fikirani HADHARANI.


Na ya MHESHIMIWA yako FARAGHANI,....
.... ndio maana WASIOFIKIRI HUKOSEA wakumuheshimu HADHARANNI.


UHESHIMIWA ni kama MADAWA ya KULEVYA,...
.... aliyenaswa na KUHESHIMIWA anajikuta anaung'ang'ania hata kwa kuomba kura za vyeo asivyovistahili HADHARANI.


Na kama unataka kulogwa na MHESHIMIWA,...
....baadaye kidogo baada ya KUWINI chuki za MHESHIMIWA,.....
... toa siri zake za CHUMBANI hadharani.


NAACHA na ni wazo tu MKULU!
Kumbuka kama umenisoma mpaka sentensi hii wewe si MTIIFU kwa kuwa nilikuomba kwenye KICHWA cha habari usisome STORI HII!:-)

Swali:
  • AU?

Ngojea basi tuliwaziwe na The VERVE katika - Bittersweet Symphony


Au ngojea tu Eminem, Jay-Z, Lil Wayne waharibu wimbo huo huo katika -Bittersweet Symphony Remix

Tuesday, June 23, 2009

Katika ULIMWENGU huu wa leo wa CHUNA BUZI , sijui bado BINTI Khalufani kwa KUNEMA hawezekani?

Siku hizi inasemekana,...
.... hata kama Binti Khalufani hawezekani kwa kunema, WANAUME hawawezi kustukia a.k.a KUJUA.

Lakini labda hata hapo zamani za miaka fulani iliyopita,..
... ujuzi wa Binti Khalufani au tu Binti Josef ulikuwa unapimwa kwa utiifu hata kama ni utiifu kwa mambo ya ajabu katika jamii ili mradi jamii inayaona ni DILI kama ya kukubali kutahiriwa KIDUDE na huko huko atahiriwako KUFUNZWA kuamini Mwanaume tu ndio USAHIHI WAKE ni SAHIHI.

Swali:

  • AU?
Ngojea nianze stori hii upya.......

Hadithi !Hadithi!

Nasikia enzi za ZILIPENDWA , ....
....VIMWANA walikuwa wanafunzwa kutii waume zao !:-)

Na nasikia pia ,...
....ilikuwa kama Mke wako akikushinda kwa HOJA kama tu aendeleavyo kukushinda hoja sasa hivi,.....
..... ilikuwa RUKSA kwa KIDUME kumchapa makofi halafu kabla hajamalizia kulia ilikuwa DILI kumshughulikia kunako apate MIMBA ili achunge adabu zake!
DUH !Kudadeki Walakhi!:-(


Kwa kifupi ,...
.....WANAWAKE na WANAUME enzi hizo ukitazama na kufikiria kwa jicho la kileo unaweza kugundua walikuwa hawajuani ila mmoja alikuwa anajitoa mhanga ili mwingine AFAIDI.

Swali kiduchu:
  • Hivi ni wewe ujitoaye muhanga mwenzio afaidi LEO HII au ni yeye ajinyimaye UMIMI ili wewe ufaidi halafu mahusiano YENU bado hayanogi?

Kwa bahati mbaya,...
... Bado naamini leo hii bado siye WANAUME tulio wengi hatulelewi kumuelewa au hata kumjua MWANAMKE. Halafu juu ya hilo, SI RUKSA KUMBWENGA Mwanamke wako hata pale katika klabu ya GONGO au Ulanzi kama tu pale kwa Bibi Kisebengo wauzapo DENGELUA siku hizi.

Kwa bahati mbaya,...
....naamini leo hii hata WANAWAKE walio wengi hawawaelewi WANAUME wanataka nini na kama unabisha WASIKILIZE waongeayo.:-(

Ukitaka kustukia kuwa hali si nzuri,....
  • Cheki jinsi gani Pochi lako likuzungumziavyo kuliko Roho yako katika maadili ya leo.
  • Sikiliza watu hata uhisio ni wenye busara wakizungumzia siri ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume hasa wakati unajua siri hizohizo wangapi zimewaharibia ndoa au kupoza penzi hata kama bado kidude wanapata.:-(
Swali:
  • Umestukia mpaka wafuata dini wamsukumiavyo Mwenyezi Mungu matatizo yao ya ndoa ambayo mengi yao yangetibika kwa wao kuongea tu a.k.a kuwasiliana/kusikilizana?
  • Unataka kusema hujawahi kusikia, hasa kama wewe ni MKRISTO, wakwepao kuongea moja kwa moja MPENZI na mpenzi kwa madai YA kupitia kwa Yesu na Biblia kitu ambacho huwatisha kuachana na kuendelea kuishi pamoja bila furaha kwa jina la Yesu?


Unaweza kunibishia lakini na LABDA miye siwezi kukubishia mwenzio KWA KUWA mwenzio hapa nawaza tu MKUU!:-(

Ndio ,..
....labda kati ya Mwanamme na MWANAMKE ukunaji wa kipele unaumuhimu wake ila labda ni muhimu kwanza kustukia uwepo wa KIPELE maeneo na kama ni busara kukibinya nasio kukikuna.

Na unaweza kubisha!

  • Leo hii tunavyoongea hapa bado WANAWAKE na mambo yao pamoja na KIDUDE chao yanaenda kivyao KAMA tu WANAUME na mambo yao ikiwa pamoja na UUME wao wanaenda kivyao.

Na asilimia kubwa ya wapenzi wenye tatizo la MAHUSIANO leo HII ukiwaweka vyumba tofauti na kuwauliza nini ni tatizo usishangae ukisikia hawana jibu linalofanana kama kwa mfano utakuta:
  • Mume adai tatizo hana pesa za kutosha, mwanamke akadai pesa si tatizo ila HAKUMBATIWI vya kutosha NA ndio tatizo!
  • Mwanamume akadai hapewi kidude vya kutosha , wakati MWANAMKE akadai KIDUME nyumbani haonekani na kidude hana muda nacho na katika KUGIDA anakila kwa uchovu ingawa daima NAMWANDALIA na manukato nanyunyizia.

  • Mwanamke akadai hasikilizwi wakati mwanamume akidai Mwanamke mashoga wamezidi na KIMWANA hapatikani ukitaka angalau KUMNG'ATA sikio.
  • Mwanamume akadai anatamani NA anafurahia KIMWANA akimfyonza, wakati MWANAMKE akadai alivyofunzwa kumfyonza mtu ni matusi na Kidume AMKOME BABU WEE nyooooooo!.:-(



Swali:
  • Unafikiri lakini Mwanamume gani siku hizi anauhakika Binti Khalufani kwa kunema hawezekani kabla ya kukutana na Binti Khalufani ki- MKUTANO?
  • Unafikiri jamii inavyobadilika ni kwanini MAFUNDISHO ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume ambayo ndio misingi ya BOMBA LA FAMILIA hayatiliwi MAANANI yabadilike kukidhi mabadiliko ya Limwanamume na Limwanamke wa leo wajengao JAMII ya LEO?
DUH nimekumbuka miye si mtaalamu wa Mahusiano YA WATU na NAACHA TOPIKI!
NIMEACHA na kumbuka hili ni wazo tu na NAKUTAKIA siku njema JEMADARI!



Ngojea niwaachie ARROW wabadili hali ya hewa kwa kitu-Hot Hot Hot





Au tu Arrow waongelee sabuni ya roho kamaitambuliwavyo na baadhi ya watu-
- money money



ASANTENI tena WADAU wote !
Asanteni hawapia ambao hamkunitenga siku za karibuni ambao baadhi ni hawa kwenye picha zangu.....

Photobucket


Photobucket







Photobucket



Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket








Photobucket








Photobucket



Photobucket

CCM OYEEE na chamoto TUNAKIONA!:-(

Hata utakekubisha,...
..... kama wewe ni Mtanzania unajua kuwa mpaka leo CCM inabomba la msuli ukilinganisha na UPINZANI.

Na kwa bahati mbaya,...
....
kwa muda wote huu chama hiki kinatawala kwa walio wengi hawajala KINGI.


Kwa bahati mbaya,...
..... hata wajanja kibao wanafikia kuamua kuwa WANACCM ili kuwa karibu na KINGI.

Swali:

  • Unabisha?

Kwa hiyo hata kama huipendi CCM,...
.... si vibaya kukiri kuwa kuna kitu wanapatia ndio maana katika STATISTIC zangu Mtakatifu Simon Kitururu ambazo sijazifanyia utafiti, ASILIMIA KUBWA YA WENYE nafuu TANZANIA ukichunguza ni WANACCM au wana uhusiano na CCM.

Swali :
  • Unabisha?


Kwa hiyo,....
.... utake usitake naweza kuwa sijakosea kwa kusema CCM OYEEE, ila zisidumu fikira za Mwenyekiti zenye mrengo wakutunyima KULA KINGI:-(


Swali:
  • Sijui Watanzania wote tujiunge na CCM kama ndio kwenye ulaji?(au unasemaje Bingwa!)
  • Kwani kuna sababu gani za kujiunga na CHAMA kingine kama ulaji uko CCM?
  • Hivi ni kweli unafikiri CCM ni CHAMA CHA MAPINDUZI?


Naacha, na kumbuka ni wazo tu KIBOSILE!
Haya basi VIVA CHADEMA!Viva CUF! Ila mnaulaji kwa wananchi wote CCM iwanyimao NANIHII?


Baadaye BASI!
Ngojea East African Melody wadai -UTAJIJU JIJI


Monday, June 22, 2009

JICHELEWESHEE huzuni kwa angalau kujaribu KUCHEKA mwanawane!

Labda kuna ukweli ,..
.... WACHEKESHAO ni wale wajuao SHIDA na kwa KUKUCHEKESHA wako tu katika kukwepa HUZUNI!:-(


Labda ni kweli,...
... kwa KUCHEKA unajicheleweshea HUZUNI.

Swali:

  • AU?

CHEKA BASI KINGUNGE ,....
.....kama UMESHAFANIKIWA KUSTUKIA au unakumbuka tu kuwa MATATIZO HAYATAISHA hata UKITUNUNIA.:-(


Kumbuka,...
.... hata kwa kujichekesha BINTI Khalufani alifanikiwa KUCHEKA na hilo laweza kukutokea wewe kama ukiacha KUJINUNISHA.:-)

Ni hilo tu na JUMATATU NJEMA Kingunge!

AU tu msikilize Chameleone aongelee - Shida za dunia

MATUSI!

Matusi ni vitendo,...
.....ingawa TUSI halihitaji VITENDO.

Matusi ni neno,....
..... ingawa bado unaweza kumtukana mtu kwa JICHO kama vile tu kwa KUMNG'ONG'A.

UMIVU la tusi hutegemea na UDHAIFU WAKO wakuoanisha UDHAIFU WAKO na tusi.

NA hakuna tusi duniani WEWE UKIAMUA,....
..... kama tu ILIVYOKUWA kuna uwezekano wa kila kitu kuwa tusi kama WEWE UKIAMUA.

Swali:

  • AU?
  • Unauhakika jina lako mtu akilitamka kwa staili fulani huwezi kuhisi ni TUSI kama tu kwa kilugha fulani Rais CHILUBA au neno GENGE ni tusi?


NAACHA halafu kumbuka ni wazo tu na wala labda halimuokoi MTU!:-(
Nakutakia LIBENEKE jema KINGUNGE!



Ngojea nimuachie Gerald Campbell ahubiriye wenye matusi kichwani....


Cat Stevens a.k.a Yusuf Islam aongelee-A is for Allah


Au tu Snoop DOGG ,Dr.Dre na Dangelo waendelee kutukana huku wakilipwa :-( katika-Imagine..
..

UNAKUMBUKA swala LA KWENDA kupima UKIMWI?

Ni hilo tu nataka kukukumbushia,...
..... kama unahisi hili swala na weye LINAKUHUSU kama tu YULE au MIMI!


Swali:

  • Kwani swala hili linahitaji maelezo zaidi?
NIMEACHA ingawa LABDA HILI swala linahitaji maelezo ZAIDI!:-(


Ngojea TENDER MAVUDLA
ambaye anaishi na MDUDU atukumbushe jambo fulani tena...

Sunday, June 21, 2009

HADITHI hii nimefundishwa na MALAYA!:-(

KATIKA fundisho kumbe ni kweli,.....
.....UNAWEZA kulipia kupewa hata GONO kama tu ununuavyo viazi VITAMU.:-(

Na,...
...
mpaka konokono wanafanya ngono na kama wewe unafanya matusi/MAPENZI kwa mwingine hiyo ni NGONO tu:-(

Na ,...
.....MALAYA ni mtoto wa mtu na inawezekana ni ndugu yako au ni mtoto wa mheshimiwa kama wazazi wako kama SIO MTOTO WAKO na labda uwepo wake duniani ni matokeo ya NGONO tu.:-(

Na,...
..... si lazima ujilazimishe kupata dhambi ingawa unafanya dhambi nyingine kwa kuwa unajua ni dhambi na NONO.:-(

Na,...
..... MALAYA ni kwa wengine kama kwako unaamini ni wako na UKO NAYE na PIA ni MNONO.

Swali:

  • AU?

DUH !
Naacha wazo MHESHIMIWA na samahani kwa kukupotezea MUDA kwa kunisoma NA labda badala ya kunisoma sasa hivi HAPA ungekuwa uko chooni UKIFANIKISHA!:-(

Swali:
  • AU?
  • Unauhakika malaya ni malaya na sio ni FIKIRA ZAKO TU kwa kuwa UNASHINDWA KUTOFAUTISHA ugawaji wake MALAYA na HURUMA au unauchanganya TU na kuwa kwake na roho NZURI ya KUGAWA nanihii?


NAACHA!

Hebu tupitie tena MALAWI tukutane na Fuggie Kasipa + Njati Njedede walete za - Ukanene



Au tupitie tu tena ZAMBIA Angela Nyirenda aburudishe kwa - Ngoma

Saturday, June 20, 2009

Labda kuna TITI kama CHUCHU au KIPELE kama JIPU , na hiyo LABDA sio STORI katika HADITHI hii !:-(

KUMBUKA,...
...ujanja wa KANISANI sio UJANJA wa MSIKITINI ingawa zote ni IMANI:-(


Kumbuka,...
....UJANJA wa kanisani labda niwa SADAKA!:-(


Kumbuka,...
..... Ujanja wa MSIKITINI aujuavyo SIO wewe na ni SHEKHE ajuaye ndio maana akiamua UTABINUKA kwa IMANI na ukibinuka kwa kweli hiyo ni staili ya SALA na yote ni IMANI!


Kumbuka,....
...LABDA kanisani AU msikitini kama ungekuwa MJANJA ungestukia kuna WATU wanatibu hukohuko MPAKA ya UCHI kama tu CHUMBANI kama wewe ni mjanja chumbani na unajua mpaka ujanja wa MIGOMBANI na UNAKIBURI katika KUNG'ANG'ANIA nanihii hata kama hiyo haina KISHIKILIO!:-(



Swali:

  • AU?

Halafu NI KWELI,....
.... labda ujanja wa TITI ni CHUCHU la sivyo hakuna KINYONYEO!:-(

Na stori hii haina uhusiano na TITI wala CHUCHU na bado hili si kielelezo cha naongea nini.:-(

Swali:
  • AU?

Ok ngojea niache KUONGEA !
Mtaalamu samahani kama NAKUKWAZA !:-(


Au ngojea tena BURNING SPEAR aongelee UZOEFU katika- This Experience:-(




Au turudi tena TU AFRIKA KUSINI Arthur MAFOKATE agune katika - OYI OYI...

Friday, June 19, 2009

KU-mamaye/KU-dadaye Walakhi! BINGWA miye KAMA weye NIMENYIMWA kuonewa mpaka HURUMA!:-(

Ni tusi kuonewa huruma,...
.....
kama wewe katika SIGIDA kwa kuwa una SIGIDA ndio UNADHANI unatakiwa kuwaonea huruma wasio na SIGIDA kwa kuwa HAWASUGUI sebule ya kichwa kwa KUSALI mpaka wakaota SIGIDA!:-(



Na KUONEWA HURUMA ,...
......ni siri ya UMASIKINI kama wakuoneao huruma wanakitumbua na wamefikia kukunyima KITUMBUA na huna uhakika na uwezo wako wa KUTIMBUA.:-(


Na si siri,...
.... kuna kitu nimenyimwa LEO kama MWAKA JANA kama WEWE TU ,....

.... ambacho kwa kunyimwa nakifanyia kazi na nahisi nitakibugia BAADAYE kwa juhudi.:-(


Swali:
  • Unafikiri juhudi ni nini na ni lini uliJUHUDIKA na kwa kujuhudika unaweza kuapia HUKUWEZA kufanikisha KULA?



SAMAHANI kama KU-mamaye ni TU-si kwa mheshimiwa kama MHESHIMIWA huwa anafikiria KU-dadaye ni NINI!:-/


Nakatiza wazo KINGUNGE na labda wazo hili ni UJINGA ingawa kumbuka ni WAZO TU na sio USENGWILI!:-(

ASANTENI WOTE na ukiwamo WEWE, lakini kama wewe ni MHESHIMIWA kama WEWE halafu umejikuta UMESOMA mpaka sentensi hii ambayo labda ni UJINGA, samahani!:-(


NAACHA!
Swali KIDUCHU:
  • Unahisi au UNAFIKIRI ni HAKI ya MUNGU au YAKO kuonewa HURUMA na wenye HURUMA wale?
Na hivi KU-shangaziye WALAKHI kwako si tusi,....
.... KAMA utaniahidi kufikiria tena kwako TUSI ni NINI?:-(

Samahani BINGWA!
Niko MAWAZONI tu mwenzio!:-( :-( :-(




Ngojea MAXWELL aongelee MAISHA katika MNONONEKO uitwao....-LIFETIME




.....AU tu MAXWELL aendeleee kutuboa kwa kibao...-REUNION..



Wednesday, June 17, 2009

Kuhusu MARUDIO ya HAMU!

Kwa KURUDIA kuwa na HAMU ya KITU si lazima safari hii UTAKIDHI HAMU.

Na huwezi kujilazimisha uwe na HAMU na ni kweli kuna hamu hazijirudii kama tu ile hamu ya KUCHOMWA na MIIBA , kuumwa na SIAFU au ile ya maumivu ya LIMTU ulipendalo kukuacha SOLEMBA na Limtu jingine!:-(



Binadamu ni MWEPESI kusahau na kumbuka hilo ukiisahau HAMU,...
....NA ndio maana ALIYEKUWA ANALIA JANA unaweza kukutananaye LEO anacheka ile balaa ingawa ni kweli ana meno kama NGIRI.

Na usidanganyike kwa kuwa labda umeshiba sasa hivi ukafikiri UMETIBU hamu ya KULA hapo baadaye .:-(

Kumbuka,...
.... HAMU ni MALAYA na ukiwa na WALI na MAHARAGE sasa HIVI kunauwezekano unajitengenezea mazingira ya kuwa na HAMU YA UGALI kwa CHUNGA.

Swali:

  • AU?
NI moja ya wazo tu Kingunge na NIMEACHA!


Hebu twende tena Reunion tupate Afrofusion kutoka kwa Granmoun Lele aongelee - Soleye


Au tu Jamie Foxx na Timbaland wabadili hali ya hewa katika -I don't need it

Kama kuna FAIDA za KUISHI na KINYONGO!

Kinyongo kama tu KULAANIWA,...
.... Laana haimtesi ALIYELAANIWA na KIMPACHO laana MTU ni KUISHI NA LAANA.:-(

Ni kweli,...
.... KUISHI NA KITU ndio KASHESHE na kukifanya kitu ni rahisi hasa kama hufikirii kuwa itabidi uendelee kuishi UKIJUA ni kweli ULIFANYA KITU naKATIKA KUFANYA kumbuka WENGINE wafanyacho ni KUUA!:-(

Kama unakinyongo na mtu ,...
.... wewe unateseka na KINYONGO na wala sio huyo MTU.

Na kama unakinyongo na MTU,...
..... na unataka USITESEKE na KINYONGO, basi usiishi na KINYONGO.

Swali:

  • AU?
KUMBUKA hili NI wazo tu Kingunge!

Ngojea Barbara Kanam aongelee ya - Teti


Au tupitie tena Cape Verde Talina alete - Pour Te Revoir

Tuesday, June 16, 2009

BINADAMU katika kuusingizia MOYO ya KICHWA!

Ukweli ni kwamba YA MOYONI yako KICHWANI,...
...ingawa kuna WADAIO kukupenda kwa MOYO WOTE!


Ya kichwani bila aibu HUSINGIZIWA hata ROHO,...
.... na YAAMULIWAYO na KICHWA huhukumiwa hata roho kwa roho kusingiziwa eti ni ROHO MBAYA.


Na WOGA wa MAAMUZI ya KICHWA,...
... kuna adaie kuna wasio na MOYO kwa KISA cha kushindwa kutekeleza yaliyo MUKICHWA.


NDIO!
Kustukia MAUMIVU au hata UTAMU ni kazi ya UBONGO mukichwa na hakuna kitu kiitwacho MOYO UNAUMA.


Na kwa kutumia KICHWA ,...
....YA MOYONI kama vile PENZI na IMANI yanaweza YASIELEWEKE na YASIYOELEWEKA kichwa huyasakizia au kuusingizia MOYO.


NDIO!
Ujinga wa YA MOYONI bado ni UJINGA wa ya KICHWA!


Na daima ni KICHWA kiusingiziao MOYO ya KICHWA!:-(

Na ni kichwa kiamuacho lini moyo uache KUDUNDA, na ukiacha kudunda hakuna TENA ya KICHWA!:-(


Ni wazo tu KINGUNGE na NINEACHA!

Swali:
  • Unafikiri ROHO inaishi wapi ndani yako?
Ngojea IMAGINATION wadai-JUST AN ILLUSION


Au tu nimuachie JAMES BROWN

Monday, June 15, 2009

Ufasaha na UMAHIRI wa MTOTO MZURI mwenye SURA MBAYA na LABDA kavaa kama tu alivyoanzishiwa KUVALISHWA chupi nzuri HALAFU SAFI!

KATIKA dunia HII yenye WAPENDA SURA NZURI ,...
.... wenye SURA MBAYA wengi hutambuliwa kwa zao JUHUDI za vitu vyenye SURA NZURI.

Swali:

  • Unauhakika ni nani mwenye sura nzuri?
  • Ni kweli unataka mpaka kujua ukweli kuwa ni UKWELI hata kuna KINYEO chenye sura mbaya kwa mtazamaji?

Kwa juhudi unaweza usistukiwe kuwa sehemu zako za siri zina SURA MBAYA kwa kuwa kwa juhudi zako wewe ni TAJIRI na katika utajiri wako baadhi ya MATUNDA YA LA KIJINGA likufanikishalo ULE KINGI , ni lile UFANYALO lisababishalo JUHUDI ZAKO zitambulike kwa HATA WASIO WAJINGA , ...
....na labda likutambulishalo NI JINSI UJUAVYO KUHONGA hasa KWA BILA , ....
......bila kujulikana unahonga kwa wakupao KIKOJOLEO,nyuma ya kikojoleo , chuchu ,NA labda hata MAANDAZI PIA kabla hujapewa KIDUDE maeneo!:-(


Na LABDA ni kweli,....
... INASEMEKANA kuwa ni KWELI kama unatafuta waishio kwa kutegemea SURA ZAO, ...
...JAMII IITAZO NZURI na unataka USITAFUTE, ....
... tembelea shule za waliofeli au tafuta sehemu rahisi zipendelewazo na WASIOFIKIRI au TU pale uhisipo kuna WAJINGA a.k.a WAVIVU wa MHANGAIKO kwa kuwa sura inauzika hata kwa HEDIMASTA.:-(
Swali:
  • AU?

Na kumbuka,...
.... JIHAMI na MTOTO MZURI uaminiye ANAAKILI kwa kuwa kwa kumuangalia huoni kasoro ZAKE ,....
.....na hujui hata UMAHIRI wake wa kutumia NYETI na kinakufikirisha kwanini huoni kasoro ZAKE kwa kuwa labda HUONI KASORO KWA KUWA MJANJA labda HUJUI KASORO ZAKE KWA KUWA anakunya KITANDANI na wewe ni ALEJIKI na MAVI na hata SEBULENI KWAKE HUJAWAHI alikwa!:-(

NDIO!
........INASEMEKANA kirahisi JAMII iwaaminio ni wazuri bado HAO na wao husamehewa hata kama WANAKOJOA KITANDANI!:-(

Na,...
....INASEMEKANA kirahisi JAMII IWAAMINIO NI WAZURI huwapandisha hata CHEO ofisini kama tu KITANDANI , huwaSIKILIZA hata kwa yasioeleweka kama vile yao ya KUGUNA, na pia ni kweli wanaweza kusifiwa kwa USAFI WA CHOO ingawa choo chao bado KINANUKA na ungejua,...
..... labda ni kweli WANAKOSEA hata KUNYA!:-(

NDIO ,..
....ni kweli ukiamini kuna MTU MZURI ,...
....huyo anakuchezea MAZINGAOMBWE na ABRA kaDAbra YAKE labda inakufanya uweze kujikuta umeoa mpaka MTU anukaye UVUNGUNI kwa mnukio ufananao na MAITI YA SAMAKI kwa sana tu ,...
...kisa NI KWAMBATU huwa akikuchekea PUA yako HUZIBA ingawa unajua hata YEYE michezo ya BABA na MAMA yeye ni MTOTO MZURI na bado KATIKA SHUGHULI yeye ni MTOTO!:-(


Na ,...
.....LABDA inahitajika kuamini KUWA kama unaamini una SURA mbaya ni muhimu kwako kucheza mazingaombwe ya JUHUDI kwa kuwa KUWASAHAULISHA WATU yako NI sura MBAYA KWA IMANI,...
..... huhitaji JUHUDI kwa kuonyesha UBINGWA WAKO kwa kitu kingine hata ikiwa ni kwa TAALUMA yako ya KULAMBA PEREMENDE ili kusahaulisha WATU matumizi yako YASIYO MAHIRI katika ya KUSHUGHULIKA na PIPI KIJITI katika PIPI iliyo na LIJITI na yote ni ili UPENDEKE tu na ukweli ni kwamba HUPENDI PEREMENDE.:-(
Swali:
  • Unafikiri mtoto mzuri ukimzoea HUWA unakumbuka kuwa mwanzoni ulidhani uzuri wa MTOTO MZURI wake KWAKO MWANZONI ulikuwa ni SPESHO?


Nakatisha WAZO na kama nimekukwaza SAMAHANI KIBINDA NKOLE, Kadoda au weye Binti Khalufani!

Ngojea Shania Twain aongee katika-That don't IMPRESS ME MUCH


Au turudi tu TANZANIA Dr REMMY amzungumzie - Karola


UNAKUMBUKA katika yote uliyowahi KUJIFUNZA moja wapo ni JINSI ya KUVAA CHUPI a.k.a KIFICHA NYETI?

Na ni kweli,...
...... HUTUKANI kama HUKUJIFUNZA tusi NI NINI!:-(

Na,..
...kuna MENGI unayoendelea KUJIFUNZA SASA HIVI ambayo hatuyajui na labda HUYAJUI kwa kuwa hayo si maarufu LEO kwa BINADAMU na yake bin-adamu ya KUJIFUNZA maeneo na jinsi ya kutumia ENEO!:-(


NDIO,...
...huhitaji KUJIFUNZA KUNYA ingawa ni kweli KUNYA huhitaji TAALUMA kama unataka KUNYA VIZURI .

Na....
.... ni kweli kama unahisi unapatia KITU ,...

...LABDA kuna KITU unafananisha nacho ambacho kwako ni MAFANIKIO ndio MAANA kwako hilo ni fanikio na kama hujui,...
....kumbuka hata KWA hilo ULIJIFUNZA!:-(


NA NI KWELI kwa bahati MBAYA,..
...hata UJITAHIDI VIPI,...
.... bado utakufa huku kuna KITU HUJUI!:-(


Samahani NAKATIZA wazo!:-(

Ngojea turudi ANGOLA SAVIMBI aongee nisichoelewa na nisikufiche napenda Kipochugali mpaka nishadeti Wabrazili kadhaa kwa kisa CHA kunogewa tu na WAONGEAVYO Kipochugali.:-(


Na ni kweli sijawahi deti Mpochugali wa Pochugali:-(
SAMAHANI kwa kujielezea kubwa kuliko katika swala la faragha na lisilo na UJUMBE mzuri hata kwa KIFARANGA.:-(

Huyu basi Savimbi adanganye wananchi kidogo kama afanyavyo KIKWETE kama naye hakujifunza kwa NYERERE....


Au tu LEADBELLY atusaidie kubadili hali ya hewa kwa ambacho bado sikielewi ingawa naelewa LUGHA katika...-Goodnight Irene



ASANTENI wadau WOTE na hasa ambao hamnitengi kama hawa waliopo kwenye picha zangu za JUUUUZZZZZI ya JAANA!:-(


Photobucket


Photobucket


Photobucket



Photobucket





Photobucket


Photobucket


Photobucket












Photobucket



Photobucket






Photobucket





Photobucket






Photobucket


Photobucket

Sunday, June 14, 2009

Historia ya MAJINA ya SIKU ZA WIKI na uhusiano wake na SHENZI!

Ukifuatilia majina ya siku kwa Kiingereza ,Kiroma au Kispanish hukawii kustukia uhusiano wake na majina ya MIUNGU ya wahusika!

Na ukifuatilia majina haya kwa Kiswahili hukawii kujikuta shughuli zako zinachelewa kuanzwa au zinaanzia siku ya TATU a.k.a JUMATATU halafu unashangaa kwanini umezidiwa ujanja na waliokutangulia siku MBILI.



Swali:

  • Unafikiri ni kwa nini siku ya PILI a.k.a JUMAPILI ndio iwe ya mapumziko kwa WASWAHILI waongeao Kiswahili?


Ndio!

Kama majina ya siku na shughuli zioanishwazo na majina ya siku hazikuchanganyi basi labda hujawahi kujiuliza aliyetafsi majina haya kwa kiswahili kuwa labda hajachangia WASWAHILI kuchelewa kufanikiwa.

Swali:
  • Kwani wewe kama mswahili hujawahi kujiuliza kwanini shughuli za Mtanzania zinatarajiwa kuanzwa JUMATATU na sio JUMAMOSI na siku ya pili a.k.a JUMAPILI Mtanzania hata kama ni MUISLAMU hutarajiwa kupumzika?
OK,..
... na ni kweli SHENZI ni KIJERUMANI ukifuatilia historia!


Na,...
.....LABDA siku uanzayo shughuli si MUHIMU kama ni kweli unaanza shughuli!

Swali:
  • LAKINI Unauhakika umeshaanza shughuli?
  • Ushawahi kufuatilia historia ya kwa nini JUMATATU haiitwi IJUMAA kwa kiswahili?

NAACHA wazo na JUMAPILI NJEMA Kingunge!

Ngojea Fu-Schnickens wakumbushie- WHATS UP DOC can we ROCK

Au tu Barry White alainishe kwa kukiri - Can't get enough of Ur love Babe

Kama unafuata DINI kunauwezekano UMEJIPONZA!

Ni kweli,...
...KAMA unafuata DINI fulani unaweza ukajikuta unajua mpaka JEHANAMU!

Na kwa kujua ,....
...KWA BAHATI mbaya UNAWEZA UKAWA UMESHAJUA MPAKA labda huwezi TENA kukana hujui DONDOO zilizopo katika STAILI yako ikuzidishiavyo KUPAMBA staili yako itakayo KUPELEKA jehanamu usipoangalia huku unaangalia.:-(

NA,...
... KWA BAHATI MBAYA ni weye mwenyewe hata sasa hivi ujuaye staili yako ikupelekayo JEHANAMU usipobadilika na hakuna WAKUMSINGIZIA.:-(



Na LABDA,...
... kama hujui auUSINGEJUA,.....

......KUNA UWEZEKANO kwako hakuna au kusingekuwa na JEHANAMU na wala stori za MBINGUNI zisingekuvutia kama tu CHOO CHA STENDI.


Na kama unajua,...
.....KAZI KWAKO!:-(

NAACHA MAHUBIRI na nimeacha WAZO!

Hebu twende ANGOLA Carlos Burity adai - Ojala Yeva

Au tubaki tu ANGOLA Miss S adai-I GIVE U MY WORLD

Kwa BAHATI MBAYA ni KWELI upumbavu UNAVUTIA!

Unaweza kubisha,..
... LAKINI asilimia kubwa ya WATU huvutiwa zaidi na UPUMBAVU!

Kinamna fulani ,...
... asilimia kubwa ya watu hufikiria UPUMBAVU ni rahisi KUUELEWA kuliko KINYUME cha UPUMBAVU!


Na hata kwa wadaio wanajua KUSOMA,...
... asilimia kubwa watakiri hupendelea kusoma UPUMBAVU kuliko kidaichwacho kuleta MAANA.

Swali:

  • Kwani hujawahi kustukia asilimia kubwa ya wajuao kusoma hupendelea kusoma udaku na sio Korani au BIBLIA?

Cha ajabu ni KWELI wengi wadaiwao kuwa ni wenye BUSARA bado hawana jibu ni kwanini BINADAMU wenye akili hawatumii akili!

Na kwa bahati MBAYA ni kweli,..
... BINADAMU WENYE akili wakitumia AKILI wanaweza KUSTUKIA kuwa wanaweza kujifunza kutoka katika UPUMBAVU kama wanastukia ni UPUMBAVU!

Na ni kweli,...
.... USIPOUSTUKIA upumbavu unaweza kujikuta umekuwa PUMBAFU!:-(

Na ni KWELI,...
....UPUMBAVU ni MTAMU na ni ADDICTIVE kama wadaivyo wanao bonga UNG'ENG'E!:-(
Swali:
  • Kwani ni KWELI upumbavu hauleti maana?

Ngojea NILIKATISHE wazo!


Au ngojea NYERERE aongee ambacho kuna anayeweza kumbishia kwa swala hilo hilo aongelealo...



AU tujikumbushe kuhusu IDI AMINI kwa mtazamo wa watu fulani ambao kwa bahati mbaya hawezi tena KUJITETEA...

Saturday, June 13, 2009

MTOTO MZURI unayehisi ananoga kama TUSI , mkileana MIGOMBANI kama huna CHUMBA!

Katika kuendelea kuongelea yasiyoeleweka ,...
.. moja ya lisiloeleweka ni KULEA ndio maana kila MTU analijua TOTO tukutu mtaani na hilo ni kama hujabarikiwa kuwanalo NYUMBANI.

Na ni kweli,...
.... kingine kisichoeleweka kwa BINADAMU ni TUSI na ndio maana unaweza kumtukana mtu akafikiri UNAMSIFIA.:-(

Na chumba inawezekana hakipatikani pekee ndani ya jengo ndio maana katika neno CHUMBA ukiongezea ''M'' kuna watakaoelewa uongeleacho ni limtu lijulikanalo kwa jina '' MCHUMBA''.

Swali:

  • Hivi Migombani ni wapi, na mtoto mdogo haleleweki migombani?
  • Unafikiri ni binadamu wangapi wanajua MGOMBA ni nini?
Tukiachana na hilo.....

Kuna waongeleao na kuna WAFANYAO inayo-ONGELEWA na ni kweli IKILAZIMIKA waongelewao wanaweza KUFANYA hata matusi na ifanywayo kama mawazo yako yamepinda , KIDUDE ni MATUSI.

Na wafanyao , ...
....hata kama wanajua SALA inahitaji kupigiwa magoti wanajua kuwa hata kwa kubinuka nahuna UJANJA unaweza kutubu ndani ya SARAKASI.:-(



Tatizo ni,...
...HATA mahiri wa hata wa shughuli au UMATI udhaniao ndiye AFANYAYE,....
... afanyacho ni kweli kwa ukweli KINAWEZA kisimfaulishe hata SHULE ya vidudu kama wewe ndio MKAGUA MTIHANI kwakuwa ukweli ni kwamba anakiongelea zaidi ya KUKIFANYA!:-(

Ndio!
Kuna waongeleao na ukiwapa mtihani utajua kuwa hawajui kuisubiria BAGIA, kuigeuzageuza iive, kuipakua kwenye sinia,..... hata kabla ya kuila HAWAKUSTUKIA STAILI YA kuionja!:-(

Ndio!
Kuna waongeleao ya SEBULENI hata KIJIWENI kabla hawajawahi KUCHUNGULIA sebule, VARANDA au DIRISHA kama sio TUNDU lililo karibu ya JICHO kwa kuwa walikuwa MUDA WOTE wanawazia kilicho UVUNGUNI.


NA ndio ni kweli ,...
....MARA nyingi si kweli mtoto anaanzia kutambaa chumbani, na labda mbele ya wageni sebuleni ndio aliaanza kutambaa na kusimama.

Ndio !
Kama umechoka,...
...... MIGOMBANI kama tu CHOONI ni chumba cha kulala au kuleana!
Swali:
  • AU?
  • Nimefanikiwa kukuzingua kwa niandikacho ambacho labda HAKIELEWEKI ingawa umenisoma mpaka sentensi hii?


NIMEACHA wazo na NINAACHA kukuzingua!:-(
KUMBUKA HUHITAJI KUNIELEWA naongea nini hapa KINGUNGE!
Nawaza tu hapa kijiweni BINGWA na saa nyingine wazo hupinda!
:-(



Swali
  • AU?

Ngojea SEAL abadilishe hali ya hewa kwa wa heshimiwa..akisema - This COULD be HEAVEN




Au tu BOB MARLEY aongelee dunia inavyochanganya katika- MIX UP MIX UP..

Tatizo la WATAKAO KUELEWA!

Watakao kuelewa mara nyingi husahau wakielewa wanaweza kukosa raha!:-(

Na,..
... WATAFUTAO kuelewa ni kweli WAMEJIONGEZEA TATIZO la kuelewa KAMA kwa kuelewa wamegundua kuwa wao ni BINADAMU na kuna mambo ukiwa MTU uwezacho vizuri ni kusononeka kwa kuwa hapa duniani na yakidunia MJANJA ni SHETANI na kama unabisha MUULIZE YEsu atakuambia jinsi gani kwa ya kidunia kama unaamini MUngu jinsi SHETANI aijuliavyo dunia.

Swali:

  • UNABISHA?

NAACHA, au ngojea niseme kwa kisauti..



Samahani nilikosea ujumbe ngojea niseme tena...

Inaumiza UKINYIMWA uliyotegemea.:-(

Inaumiza roho UKITEGEMEA halafu USIPEWE!:-(


Na,...
... INAUMIZA kama ADHABU ,....

............ingawa HIYOHIYO adhabu ikiitwa ZOEZI kuna wengi watakaoifanya kwa furaha na wengine mpaka wataota- SIKSIPAKI juu ya mavuzi.:-(

Na labda WATAKAOUMIA ZAIDI ni kama wale,...
.... wadhaniao INAUMA au KUJILAUMU zaidi kwa kufikiria kama WAFIKIRIAO wataenda MBINGUNI halafu labda baadaye kidogo baada ya kufa wakajikuta JEHANAMU.:-(





LAKINI labda Ni kweli,...
... inaumiza KAMA KUBWA kama tu IUMIZAVYO roho , moyo na mwili ,kwa juhudi IKIPWAYA kwa UKUBWA.

Ni kweli labda,...
......INAUMIZA!

Swali:
  • Kama wewe ni muombaji MUNGU hujawahi kuhisi kunyimwa na MUNGU hata baada ya bomba la sala?
NAACHA wazo na kama nakukwaza niombee au TUBU kivyako chobisi uende PEPONI!

Ngojea Lenny Kravitz anisaidie wimbo uitwao- Many Rivers to Cross

Au to nimuachie aliye utunga wimbo JIMMY CLIFF arudie wimbo- Many Rivers to Cross..

Thursday, June 11, 2009

Kwa JUUJUU!

Kwa JUUJUU bado sio NDANI na haijaingia.:-(


Kwa JUUJUU,...
.... amuonaye anayecheka hudhania achekaye moyoni anafuraha!

Kwa JUU JUU ,....
.....aliaye anaweza dhaniwa halii kwa furaha!


Kwa JUUJUU ni ngozi ,...
......na kuna BINADAMU weupe na weusi wasahauo kuwa wote WAFANANA kwa ndani!:-(


Kwa JUUJUU ,....
.....akaaye kimya wanadhani KASAHAU!

Kwa JUUJUU,....
..... unaweza kutomstukia atakaye hata kukupiga JUJU!

Kama unajua JUU JUU ,...
.....weye hujui undani wa KITU au MTU na ujuacho ni kwa JUUJUU na labda ni kweli udhaniaye mlevi hajalewa!


Na,...
... kwa JUUJUU labda nilichoandika ni UJINGA!:-(

----------------------------------------------------_______________----------------



NI wazo tu MKUU na NIMEACHA!

Swali:
  • Unadhani kuna umjuaye kiundani?
  • Unadhani ni mara ngapi unajaji kitu bilakukijua kiundani?
Nakutakia siku KIBONGE na mafanikio JEMADARI!

Namuacha Mr FOX adai-Yo No Tengo La Voz


Au tu YONDO SISTER alete-Mbuta Mutu

Wednesday, June 10, 2009

Kwa BINGWA muanzisha UCHOCHORO!

Twajua DUNIANI asilimia kubwa ni WAFUTA zilizosha-tengenezwa NJIA,...
.....VICHAKANI kwao hakupitiki ,kwao vichakani HAKUNA NJIA!

NA WATASIFIANA kwa ubingwa wakuwahi kufika kwa umahiri WAKUFUATA NJIA,...
......HUKU WAKIMTUKANA aliyeanzisha hiyo njia KWA KUSAHAU nani alianzisha NJIA!


NA aanzishaye UCHOCHORO si MAARUFU kwa wadhaniao wanajua njia kwa kufuata NJIA,...
.....WAKATI labda UCHOCHORO badaaye ndio utakuwa NJIA!


NA asiyejali HUMDHARAU aanzishaye UCHOCHORO baada ya kumsahau hata ALIYEANZISHA NJIA.....
....MPAKA agunduapo UCHOCHORO ni njia ya MKATO kuliko njia.

ASANTE Bingwa muanzisha UCHOCHORO na yako naamini ndio NJIA!

Swali:
  • Wewe ni mfuata njia kwa kuwa umeambiwa hiyo ndio njia?
  • Unakumbuka labda ukichoshwa na makali ya njia labda ndio wewe mwenye uwezo wakuanzisha nyingine njia?


NAWAZA tu MKUU!
Ngojea twende New York SHY CHILD watupe- Drop the Phone



Au turudi tena Kameruni TOM YOMS na MAREHEMU CHARLOTTE Mbango waendeleze..-SENGAT TO

Kama kuna JINSI ya KUIZOELESHA jamii kuwa UMEMUACHA MKE WAKO AMBAYE BADO unaishinaye na unamendea HAUSIGELI!

Katika jamii inasemekana HAUSIGELI ni msaidizi wa nyumbani kama vile mke hasaidii nyumbani!

Na labda kuna mke anaogopa jamii itamfikiriaje akimuacha mume na kumchumbia HAUSIBOI asaidiaye nyumbani na ya UNYUMBA kuliko LIMUME vivu!:-(

Na jamii ilivyo KIBOKO,..
... ikiuzoea UNYANYASAJI huwa ina mchezo wa KUUKALIA KIMYA!:-(

Na jamii ikikutambua kama wewe ni HAUSIBOI au HAUSIGELI inamchezo wa kukusamehe hata kama hujui kuandika na kwa jicho la jamii weye shule hustahili ukijumlisha na bado ukinyanyasika kwa unavyonyanyaswa jamii ni KIPOFU!:-(


Na unaweza kubisha,...
... lakini MKE ateswaye na MUME au Mume ateswaye na MKE hu- hurumiwa zaidi kwa teso hilo hilo ambalo ukiitwa Hausiboi au Hausigeli linafumbiwa macho.

Swali:

  • Hivi Hausigeli hawezi kuwa Mke wa Mtu au Hausiboi hawezi kuwa Mme wa mtu?
  • Hivi Hausiboi hawezi akawa ni msenge wa baba wa nyumba na Hausigeli ni msagaji wa mama wa nyumba?[samahani kwa wazo la faragha!:-(]

Ndio ,...
... inasemekana kuna WAPENZI wapendezao zaidi GIZANI au kabla WAGENI HAWAJAJA ,lakini mpenzi ni mpenzi ikiwa mpenzi wako NI MTU na si mbwa au kuku mrembo.NA kama unaficha ufanyacho ni UNAFIKI!

Jinsi jamii inavyojali statasi za watu unaweza kukuta Limwanamke lenye uwezo wa kuishi na Hausiboi limpendalo linanyanyasika kwa kung'ang'ania Limme lisilompenda wakati limme lake linashindwa hata kufikiria kazi kazini kwa kumuwaza Hausigeli mpendwa na jinsi litakavyo jaribu kumchungulia upaja jioni akipika, HAUSIGELi ambaye linahofia likionyesha pendo jamii itakuja juu halafu litadharauliwa.

Ndio!
Jamii ni kichaa na usipoangalia utaishi kama MNAFIKI kwa kuwa jamii kuna mambo HATA ya kawaida kama KUJIFIA kwa MTU a.k.a KUPENDA, huyachukulia kama ni vitendo vya aibu kama jamii ikidhani umekosea kulilenga Limtu BOMBA!:-(

Na tunasikia kuna aliyemuacha MME wake akafuata MDUNDIKO , na inashangaza kwa watu wengi waliosikia msemo huo kutoendelea kufikiria kwani huko kwenye mdundiko kuna akinanani wanogeshao MDUNDIKO!:-(

Swali:
  • Kwani unafikiri jamii itakumbuka kwa muda gani uliacha mke wako ukafuata Hausigeli?



NIMEACHA na kumbuka tu ni moja ya wazo tu MKULU!
PS :
-Mimi Simon sina Hausigeli bado na natafuta kimwana cha kuchukua chotechote na kama wewe ni hausigeli, bomba TU nistue tuangalie ule mpango VIPI!

Hebu turudi Rwanda tukasikilize wimbo wa mapenzi. Tupate Somi-Ingele


Au turudi Tanzania kwa Saida Karoli adai-Nkaba Ningya




ASANTENI wadau wote mkiwemo baadhi ambao nilikutananao juzi ya jana kama muonekanavyo katika picha zangu za juzi ya jana!


Photobucket


Photobucket

Photobucket



Photobucket







Photobucket



Photobucket



Photobucket







Photobucket



Photobucket


Photobucket




Photobucket


Photobucket



Photobucket

UKISEMA huu ni UTAMADUNI WETU WAAFRIKA, unamaanisha NINI?

AFRIKA bado sio moja ,....
.....ingawa unaweza kunibishia!
Afrika labda haitaweza kuwa moja ,...
....ingawa unaweza kuendelea KUNIBISHIA!
AFRIKA sio moja LABDA na HILI NDILO MOJA ya sababu za WAAFRIKA kuwa wakali katika FANI YA KUBWENGANA WAO kwa WAO a.k.a VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE.

Na labda HAKUNA kitu kiwezacho kuitwa ''WENYEWE kwa WENYEWE'' wakati hata ''WEWE unaamini kuwa wewe sio ''MIMI''.
Swali:

  • Kwani wanaoongelea ''SISI WAAFRIKA'' kwa neno''SISI'' huwa wanamaanisha sisi ''WAHANZABE au WANGONI'', na sio sisi ''WAMISRI na WAXHOSA''?
  • Unakumbuka katika matumizi ya neno ''SISI'' hata katika kudai sisi WATANZANIA tulimpigia MKAPA kura awe Rais, ina maana unawasingizia watu lukuki na kuwaingiza katika swala la kura za Rais Mkapa wakati mpaka leo wanaamini Rais wao alikuwa ni Lyatonga MREMA?

Tukumbuke tu kuwa neno ''SISI'' ni neno KIRAHISISHI na wengi watumiao neno ''SISI '' humaanisha -''MIMI''.

Nachomaanisha ,...
... kwa wacheza MDUNDIKO Tanzania , huwa wakizungumzia Utamaduni wa Tanzania huunganishia mdundiko pia, wakati kwa Wamasai mambo yote ni KURUKA na Sindimba kwao haipandi kama tu MDUNDIKO usivyo kuwa wao Utamaduni!:-(

Swali:
  • Au?

Au nijaribu kusema tena,...
Kumbuka ndani ya TANZANIA tu na UAFRIKA WAKE,
  • Kuna wenye mila na desturi /tamaduni za kulia MSIBANI na wale wachezao disko MSIBANI.i.e Ushahudhuria msiba wa Kijaluo au ule wa Kimasai?
  • Kuna walao Mbwa na watoshekao na Panya.
  • Kuna watahirio wanaume na kuna watoshekao na mpaka kumtahiri KIDUDE mwanamke.
  • Kuna wenye utamaduni wakucheza ngoma kwa kutikisa tako huku chuchu nje na waimbao tu na kuruka bila kujali matumizi ya chupi.
Nachomaanisha ni,...
... SISI wa AFRIKA tupo wenye tabia za KIARABU na TUPO PIA tufuatao tabia za Kizungu za kuweka majaji watusaidie kuamua ni MISS gani anatembea vizuri nusu uchi au kwa chupi ya kuogelea yenye kuonyesha kidogo kiburungutu cha nywele za nyeti chini kidogo ya kitovu ili ashinde U-MISS KIBAHA!


Na ni kweli ,....
..... BISHA usibishe UKIZUNGUMZIA sisi WAAFRIKA, usisahau Wamoroko wanadai ni Waarabu na Dr Leakey wa Kenya anadai ni Muafrika!

Sasa swali:
  • Ukisema HUU NI UTAMADUNI WETU WAAFRIKA unamaanisha nini?
Ni wazo tu KINGUNGE na labda wazo lako ni sahihi kuwa ni KWELI Afrika ni moja !
NIMEACHA!

ngojea turudi South Africa ARTHUR MAFOKATE atukumbushe -Oyi, Oyi

Au tuendelee kubaki South Afrika watu fulani wapewe soseji katika-VOROSO

Busara za MWENDO wa kwendea CHOONI kabla HUJABANWA vizuri na HAJA NJONJOLINJO!

Ukijiandaa vizuri,...
.... hata kwenda chooni unaweza kutembea kwa maringo!

Tatizo la kusubiri mpaka ubanwe unaweza ukajikuta mwisho wa mwezi pesa za kodi ya nyumba ulisahau kuzitunza au tu unastukia jinsi ulivyokuwa mahiri wa kumkwepa anaye kudai!:-(

Na wakati unaenda chooni wakati hujabanwa vizuri,....
... una lakshari ya kuwaza kitu kingine wakati unausogelea mlango wa maliwato na uliwazalo likawa halina uhusiano na HAJA namba moja au ile NAMBA MBILI!

Swali:

  • Kwani nani anabisha wajiandaao vizuri mara nyingi ndio watuliao kwenye mtihani?
  • Unakumbuka kukuru -kakara usiku wa mtihani ghafla ukistukia labda hujajiandaa vizuri?
  • Unakumbuka wakati unaenda chooni huku umebanwa huwa HUPEI-ATENSHENI unavyotembea na kukanyaga mavi ya mbwa wakati uko katika safari hiyo ya chooni wakati umebanwa wala hakukufanyi upumzike ILI kusafisha kiatu?
Lakini tusisahau kuwa,...
.... ni muhimu pia kupitia mwendo wa kwenda chooni huku umebanwa ili uelewe starehe ya kutobanwa, KWA KUWA unaweza ukastukia ukibanwa tafakuri zako zinabobea kwenye haja mpaka hata HARUFU ya kinyesi cha aliyekutangulia chooni HUWA hukisikii!

Tatizo tu la kuwa choooni kwa kuwa umebanwa na unahangaikia haja bila kustukia harufu ikuzungukayo,...
..... ndio KISA utashangaa JAMAA limeingia OFISINI halifikirii UFISADI na likitoka LINANUKA UFISADI.

Swali:
  • Kwani unafikiri wapokea rushwa wengi waliingia ofisini wakiwa na nia ya kupokea rushwa?

Nachojaribu kusema,...
..... ukiingia chooni na kibano , unaweza ukatoka chooni unanuka harufu ya MAVI bila kujua!

Na kwa maana nyingine,...
...kama hujajiandaa na ukafaulu basi hiyo ni bahati tu na unaweza ukawa unaitwa Profesa wa NANIHII kwa kuwa umefaulu lakini ukweli ukawa ni Profesa waNANIHII asiyeJIAMINI!

Swali:
  • AU?

  • SI binadamu anaweza kupanga katika siku ni saa ngapi anaenda haja kubwa?
Kumbuka tu,...
.... ukijiandaa utajua kuwa hata kinyesi chako chooni hukunukia weye kwa dakika kadhaa tu wakati unaanza kukishughulikia ndio maana baada ya dakika kadhaa unaweza mpaka kuanza kusoma gazeti huko huko chooni kwa kuwa umeshazoea harufu ya kinyesi chako na atakaye ingia chooni baada yako ndio atabana pua.
Swali:
  • Unauhakika naongelea nini?

NIMEACHA!
Ngojea Ziggy Marley alete- Goodtime Accoustic



Au to Sting na Ziggy Marley walete- One World

Sunday, June 07, 2009

MCHANGO wa WAHUNI kwa TAIFA!

Pamoja na WAHUNI kuwasaidia WENYE TABIA NZURI, Walokole, Ustadhi na.... WAHUNI kuna wawaDHARAUO!

Wahuni ni bomba mpaka wanaweza kukukumbusha kuwa wewe si MHUNI!:-(

Labda hata sababu zako za kujisikia vizuri leo ni msaada walioBUSTI wahuni mpaka unafikiri hujapotea halafu umepatia ingawa bado kicheko chako cha jana na usipoangalia labda hata cha leo ni cha KINAFIKI kwa kuwa MPAKA LEO unayemchekea hakuchekeshi lakini ukijichekesha we SI MHUNI kama ni tafsiri ya MAENEO.:-(


NA kuna UWEZEKANO mpaka MCHANGO wa PROFESA kama uliwahi kukutananaye ukawa UNAZIDISHA kukufanya uzidi kuwa BINGWA wa KUKARIRI bila KUELEWA wala kujua KUFIKIRIA kisa unataka jamii ikujue wewe si MHUNI na labda ukimbishia PROFESA kuna anayeweza kuhisi ufanyacho ni UHUNI!:-(



Na ni kweli kama wewe si MHUNI unaweza ukashangaa MCHANGO wa SHEKHE, ASKOFU, BABA na labda DADA YA SHANGAZI yule aliye tajiri kumzidi MAMA , inasemekana kuwabishia ni tabia mbaya na inawezekana kuwa watu wakaamini kwa hilo WEYE MHUNI!:-(

Kumbuka lakini kuwa,...
... UHUNI ni tafsiri BINAFSI kutokana na ulivyofundishwa au kujifundisha nini ni UHUNI!:-(

Nachojaribu ni kusema,..
... fikiria tena mchango wa uhisiye ni mhuni kama ukiruka kipengele kikufanyacho ufikirie UHUNI?
SWALI:

  • Umesahau kwa tafsiri fulani Rais KIKWETE na Auntie MUDI wote ni WAHUNI kama wanafiti kwa yako tafsiri?
  • Kwani kwako UHUNI ni NINI?
NI HILO tu kwa leo!

NAACHA na kumbuka ni moja tu ya WAZO hapa MAWAZONI!:-(

Nakutakia siku KIBONGE na MAFANIKIO JEMADARI!...

AU tu ni muache Marehemu aliyetutoka juzi ya jana kutoka Kameruni nizimiaye shughuli zake aitwaye CHARLOTTE MBANGO alete-KONKAI...

JINSI nimuheshimuvyo UNAYEMDHARAU!

Kuna watu unawaheshimu halafu ukashangaa wao WANAMUHESHIMU unayefikiri anafaa KUDHARAULIWA!:-(


DHARAU ni bomba la udhaifu ndio maana hujafikiri kuwadharau UDHANIAO ni BOMBA:-(



NDIO,..

...LABDA kila mtu ana sababu zake KWA NINI anadhani MIMI au lile JINGA!:-(


Ila USAHIHI wa SABABU ukijulikana INAWEZEKANA asilimia KUBWA ya WANADAMU wanakosea WAKUMDHARAU!

Swali:

  • Una uhakika na sababu zako zisababishazo kuna CHAUPELE una mdharau ?
  • Una uhakika CHAUPELE akipona UPELE hutatamani kumpa kikojoleo kama isingekuwa dhambi?



NI hilo tu na NIMEACHA WAZO!:-(


Ngojea SHABBA RANKS aongelee -Trailer LOAD of GIRLS...


Au tu BILLY PAUL aongelee mapenzi ya MKE wa mtu katika-MIMI na mke wa JONES

Kama MUNGU akibadili MAWAZO!:-(

Labda,....
.... MUNGU ghafla anaweza kuamua kuzimia VIUMBE VYAKE vyenye juhudi za kufanya dhambi kwa kuwa wadaio hawafanyi dhambi katika fani zao zakutofanya dhambi ni VUGUVUGU .


Katika juhudi za wafanyao dhambi,...
.... WAFANYAO wanajuhudi kweli na DHAMBI mpaka SAA NYINGINE HUWA wanaivulia MPAKA kificha NYETI !:-(

Swali:

  • SI ya MUNGU bado anaamua MUNGU na bado anayojua MUNGU ajuaye ni MUNGU MWENYEWE?



NI kweli lakini,...
... inasemekana asilimia kubwa ya wajaribuo kutofanya dhambi kama wewe ni VUGUVUGU na kuna kidhambi kina wini kishenzi kama kile chako CHA kudhani wengine wana DHAMBI ZAIDI!:-(



Ni hilo tu NILITAKA KUSEMA!:-(

NIMEAACHA!:-(
BAADAYE basi MKULILA!

Hebu basi twende tena Namibia Tate BUTI aongee tena - Efenge

Friday, June 05, 2009

Kuhusu JITIHADA za KUACHANA na MAWAZO YALIYOPINDA na YASHUKIWAYO kuwa yana KASORO KIDUUUUCHU!

Kama weye ni mdadisi basi kuna mengi unajiuliza na kuwaza ila kwa sababu zako kuna MENGINE unafanya yawe kwetu SIRI!


Na ,...
......huwezi kuchagua uwaze nini!:-(

Na,...
....
huwezi kujikataza kurudia kuliwaza jambo kwa kuwa ulishaliwaza juzi!

Na,....
...
haki yanani TENA ungejua kila akuangaliaye unamkuna kivipi KIMAWAZO, kuna uwachekeao UNGEWANUNIA na uwaheshimuo ungewadharau!

Na,..
...kwa bahati mbaya kila mwisho wa siku ni maelfu ya mawazo ambayo huwa unayasahau ingawa kuna uwezekano kuna wazo moja la kijinga unaweza ukalikumbuka hata mwaka kesho.

Kumbuka tu kuwa,....

.... kila MWEREVU au MWENYEBUSARA umjuaye ,....
.... HAMALIZI SIKU bila mawazo kadhaa kumpitia kichwani ambayo ni ya KIJINGA.
Swali:
  • AU?
  • Au unafikiri MANDELA,OBAMA, Liyatonga Mrema na PAPA BANEDICTO wao ni tofauti ?
Nachojaribu kusema ni,....
..... kama wewe ni muwazaji, KILA SIKU kuna WAZO LAKO ambalo labda ni SIRI na ni kweli LABDA kwa wengine LIMEPINDA na lina kasoro KIDUUUCHU!:-(

Endelea kuwaza lakini ,....
...... ingawa sio lazima utuambie kila siku au kusema ovyo kama Mtakatifu Simon Kitururu kama lile wazo lako LA labda kila ukimuona mtu kavaa kanzu moja ya wazo likupitialo MUKICHWA ni kwamba labda hajavaa chupi.

NI HILO tu KWA leo!


Asanteni kwa wote wanaoendelea KUNITEMBELEA na KUSOMA MAWAZO yangu YALIYOPINDA katika huu mtiririko naouita UjingaBUSARA.

Samahani KWA AMBAO nawakwaza kwa kuandika mawazo mawili matatu mara kadhaa ambayo kwao yana KASORO KIDUUUCHU na KUWAKWAZA!:-(

Ijumaa na WIKIenDI njEMA / AMANI KUBWA KULIKO iwe nanyi MILELE AMINA!
Naanza KIVYANGU hivyo , PEACE!


Unaweza tulia Billy Ocean aongee.....


Au tu Billy Ocean azungumzie-Suddenly

Thursday, June 04, 2009

ETI inasemekana KUBWA ZIMA linaweza KUHARIBIKIA UKUBWANI!:-(

Mambo mengi hayatokei au kuharibika GHAFLA TU kama walalamikaji wanavyofikiri!:-(

Kama unabisha iangalie Tanzania!

Swali:

  • Au?

Labda ni kweli kuna MAKUBWA kubwa zima inabidi lianze kuyaonjea UKUBWANI!

Lakini mengi kubwa zima yalinogeyalo KUYAGIDA ukubwani,.....
..... hamu za kuyaonja hata kwa staili ya NANIHII haikuanza ghafla UKUBWANI.

Ni kweli,...
... wengi huongelea MATOKEO ingawa DALILI zilikuwepo UTOTONI ndio maana wanashangaa hata ya KUBWA JINGA.

Na ni kweli,....
..... UKISHUHUDIA kitu leo mara nyingi misingi ya TOKEO ilikuwepo tu muda mrefu na washangaao TOKEO ni wachelewao KUSTUKIA DALILI ndio maana labda leo kwao LIJAMAA ni kubwa zima bado kuendelea KUCHEZA MDAKO au kupora watoto KUMBIKUMBI kama tu kuwa BOMBA LA MALAYA halafu upatikanaji wake BEI CHEE kwa kushindwa kupandisha bei!



Na kunauwezekano mpaka leo kuna TOTO huliangalii TU vizuri na ndio maana kwa kutoliangalia kwako katika mwenendo wake wakati bado KINDA a.k.a TOTO , baadaye utadhani NI KUBWA ZIMA halafu limeharibika GHAFLA ukubwani!:-(

Swali:
  • Kubwa zima unalodhani limeharibikia UKUBWANI unauhakika unalikumbuka au ulikuwa unalijua UTOTONI?

  • Unauhakika kuna KUBWA LILILOHARIBIKA na sio tu NI TAFSIRI yako ya JAMBO na ya KUHARIBIKA ni NINI inayokuponza kudhania BINADAMU anaweza kuharibika?
Ndio kuna vitu vipo TU !

Labda ndio maana huhitaji kuwafunza dume na jike staili za kutamaniana na labda wenyewe tu hata ukiwaacha pekeyao wakati bado wadogo msituni , WAKIKUA ukirudi unaweza kushangaa walizaa watoto kwa ubunifu wa MAKUBWA UKUBWANI bila MWALIMU.

Lakini kama uliwachunguza wadogo LABDA utastukia tu mwelekeo wa mtu kuweza kupewa MIMBA hapo baadaye labda kwa kustukia hawa wadogo walianza mapema kuonyesha dalili za mtu kuwezapewa ujauzito kwa kuonyesha HATA dalili za kupendana na hiyo ni kabla hawajagundua kwa kupendana kuna wavulianao nguo katika moja ya hatua za penzi.:-(



Nachojaribu kusema ni;
...unauhakika aliyeharibika kwa kuwa ni mkubwa basi maana yake kaharibikia UKUBWANI kwa kuwa umemstukia JUZI wakati MKUBWA?
NAACHA wazo!

Hebu tubadili hali ya hewa kwa kwenda Minesota tukashuhudie WAKUBWA WAKIPIGANA KANISANI!


Au ngojea tu mke wa Rais wa France a.k.a Carla Bruni alainishe ukubwa kwa-- Tout le monde

Binadamu na matumizi yake ya Mungu!

Tukiachana na swala la MUNGU wanani ni sahihi,....
......kwa mwenye udhaifu wa kibinadamu kuna SIKU au KITU utakwama na litokeapo hilo nikikusimulia hata ya kuhusu Mungu wa Kimandengereko anavyosaidia unaweza kuchukua muda kunisikiliza wakati kwa kawaida ulikuwa unamjali na kumuabudu Mungu wa Kihindu.

Na usipoangalia,....
..... labda kuna mambo unakosea mwenyewe halafu UNAMSINGIZIA MWENYEZI!


UKITAKAKUJUA ni kwanini Mungu ni muhimu,...
....fikiria jinsi ilivyorahisi hasa BINADAMU akikwama apatavyofaraja hata kwa kudai HATA KIBANO ni mipango ya MWENYEZI MUNGU!


Binadamu wengi wakati wanajisikia kufakufa ghafla na imani inakua.

Jinsi kibano cha udhaifu wa KIBINADAMU ulivyomkali,...
.....kuna ambao mpaka wanaokoka au kustukia imani za kuabudu Mbuyu hata kwa KIBANO cha KUCHACHA.

Ukweli ni kwamba,....
.....KWA ASILIMIA kubwa ya BINADAMU, ni FARAJA wapatazo kwa kuamini kitu chenye uwezo na NGUVU kuliko wote kinakutunza na KUKULINDA.

Swali:

  • Unakumbuka enzi zako za utoto za kufikiria Baba Yako anaweza yote na haanguki?
  • Unakumbuka filingi ya kuzidiwa nguvu hata wakati jamaulilofikiri unalizidi nguvu halafu ghafla ukastukia linakubwenga kisawasawa kisha ukamstukia mtu mtetezi anakuja ?


Kwa imani inasemekana yote yanawezekana,...
.....lakini kama weye mchunguzi utastukia asilimia kubwa ya waombewao dua hata kama ni za ugonjwa huwa hawaponi.:-(


Kikubwa ni FARAJA uipatayo!

Unaweza kubisha ,...
.....lakini asilimia kubwa ya waombao Mungu , MUNGU wao huwa hawajibu na ni imani tu inayoendelea kuwafanya wasikufuru kwa faraja kuwa kuna sababu ajuazo MUNGU wao kwanini umeomba weee halafu mpaka leo HUJAPATA na wapatao ni wezi na baadhi uliwapigia kura.

Na aaminiye hata ajuapo anakufa kinachoweza kumfanya afe kwa amani ni kwamba anafaraja tu.

Na wamuombeao mtu hata yule mgonjwa asipopona muhimu kwao ni FARAJA kuwa anaenda Mbinguni au kwa waaminio dini fulanifulani labda hufarijika kuwa anarudi Kigoma na mzimu wake utaendelea kuwalinda.

Swali:
  • AU?

JIANDAE kinamna kivyako na Mungu wako kwa kuwa Mungu usiyemuamini unaweza usiwe na uhakika naye mpaka dakika za mwisho na utakacho kosa ni kupoza roho ya na kuanza huku huna FARAJA!

Swali:

  • AU?


Naacha na kumbuka hili ni moja ya wazo tu USITISHIKE!

Lakini kama umekwazika niombee au tubu kivywako kama katika imani yako ukitubu maswala ya PARADISO yatakuwa MSWANO!


DUH!

Ngojea tupumzike kwa kuangalia talanta za Mwenyezi....


Au tu ngojea tutulie na King Boogaloo Tut -Smooth poppin'..

Wednesday, June 03, 2009

Data za leo za CIA kuhusu Tanzania bado zinanizingua!


HIV/AIDS - people living with HIV/AIDS:

  • 1.4 million (2007 est.)
Hivi ni kweli idadi ya hata Tanzania inawatu wangapi inajulikana kikweli?


Religions:
  • Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim

Hivi hii ya 35% indigenous beliefs Rais wao atatokea lini wakati kilasiku kwenye siasa tuna wasikia wakristo na waislamu tu wakilumbana? Hawa wenye indigenous belief wako wapi katika kuchangamkia maswala hapa TZ?

Literacy:
  • : age 15 and over can read and write Kiswahili (Swahili), English, or Arabic
total population: 69.4%
male: 77.5%
female: 62.2% (2002 census)
Hivi hawa asilimia zisomazo na kuandika huwa zinahusudu kusoma nini?


Government type:

  • republic
Capital:

  • name: Dar es Salaam
geographic coordinates: 6 48 S, 39 17 E
time difference: UTC+3 (8 hours ahead of Washington, DC during Standard Time)
note: legislative offices have been transferred to Dodoma, which is planned as the new national capital; the National Assembly now meets there on a regular basis
Hivi kumbe makao makuu sio Dodoma tena?

Internet users:

  • 400,000 tu(2007)
Kazi ipo!

Age structure:

  • 0-14 years: 43% (male 8,853,529/female 8,805,810)
Hapa inaonyesha kuna watu watakosa mke hapo baadaye.

ENDELEA kivyako kama unamuda mie NAACHA kwa kukongoli CIA -Theworld FACTBOOK

Ngojea nimuachie Lukazi Sambatree atupe -Tanzania National Anthem

Tuesday, June 02, 2009

UJINGA!

UJINGA MAARUFU ni ule ufanywao na WATUMIA AKILI!
Swali:

  • AU?


NA CHA AJABU ni kwamba,...
......wale wajulikanao kwa MIAKILI ndio kuna ujinga hawaustukii hasa katika sehemu wasizotaka kustukia hili kwa kuwa wanaamii lile kama vile NANIHII ziitwazo DINI.


Haki ya nani tena ,....
....... ni wenye akili ambao HUANZISHA KUABUDU hata KUKU kisa ni KUKU ZERUZERU.:-(




UJINGAAA!



Tatizo la UJINGA MAARUFU ,...
.... kama ukiustukia kuna watakaodhani au kuwa na uhakika UNACHEMSHA.

Swali:
  • AU?


NAACHA!

UMAARUFU wa asiye MAARUFU wakati anadhani ni MAARUFU, na hata ukimsikiliza labda kanogewa kabisaaa na adhaniavyo ni MAARUFU:-(

Wadhaniao ni maarufu labda kuna mtu KAWASIFIA!

Na ni kweli baadhi ya sifa watu wakusifiavyo ni UONGO.:-(

Na ni kweli kuna watu wanapenda sifa kwahio ukiwasifia kuhusu titi wanasahau kuwa kabla hujagundua ukubwa wa titi LABDA uligundua mtoto mzuri HUYOHUYO tako lake moja limekonda:-(

Na ni kweli MTU asifiwaye kirahisi anaweza kuanza kuamini MAKENGEZA ni KUREMBUA.


Swali

  • AU?
NAACHA wazo!:-(
Au tu Sade anisaidie kupitisha siku kwa kuongelea mwiko -Sweetest Taboo



Au tu KASSAV waendelee kunisaidia katika-Zouk La Ce Sel Medicament Nou Ni

JINSI ya kuendelea KUVUMILIA UTAMU!

UTAMU ni MAUMIVU!

Na LABDA kama unanogeawa na utamu KUNAUWEZEKANO unajua MAUMIVU.



Swali:

  • Hivi wakati unasikilizia utamu ushawahi kujiuliza ni kwanini UNADHANI ni TAMU?


Na labda wakati unasikia utamu hujiulizi kwa nini utamu wa sukari na kikojoleo ingawa unajua hivyo vyote ni tofauti ila bado vyote ukifaidi unadhani au unauhakika vyote ni vitamu.
Swali:
  • AU?
  • Lakini si unajua ukizidisha sukari hata chai hainogi kwa kuwa sukari imezidi na chai imezidi utamu?


Na ni kweli kuwa hata kikojoleo kinaweza kukusaidia kusikilizia utamu lakini labda ukikinusa wakati kinakusaidia kuonja utamu BADO labda KINANUKA.:-(


DUH!
Naacha WAZO na kumbuka hili ni moja la wazo tu!:-(
AU ngojea Kofi Olomide amuongelee - SYLVIE


Au tu tu Frankie Paul arudie kuongelea - SHUB IN

Monday, June 01, 2009

USHAWAHI kumuangalia MHESHIMIWA halafu WAKATI UNAMUANGALIA ukafikiria SURA YA MHESHIMIWA umuangaliaye wakati ana KUNYA?

Kuna MAMBO afadhali usiyafikirie!:-(



Na wakati una nguvu za kufikiria kuna uwezekano WEWE UMEKULA!

Nafikiri unakumbuka NI VIGUMU kweli kufikiria vizuri kuhusu hili wakati unanjaa ya LILE!


Na ni vigumu kweli kufikiria wakati UNA NJAA!:
Swali

  • AU?


Lakini unaweza kunibishia kuhusu maswala ya MHESHIMIWA kunya kwa heshima HUWA kuna tofauti sana na MHESHIMIWA akitafuta KUHESHIMIWA.:-(


SIBISHI kwa kuwa labda kuna kitu unajua halafu kwa kujua kitu unadhani naongea UPUMBAVU !:-(

NAACHA wazo na NIMEACHA wazo!:-(

Ngojea WERRASON aendeleze ANASA katika -DANCE MANIA




Au tu marehemu DENIS BROWN aendelee kuzungumzia -The EXIT











Photobucket
NIpo LAKINI kama hivi....



Photobucket


Photobucket



Photobucket




Photobucket





Photobucket






Photobucket




Photobucket