Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Na ni mstari mwembamba kati ya KUFAULU na KUFELI!

>> Tuesday, November 22, 2011

Na  kama UMEFAULU,...
.....labda  kumbuka kufeli kupo tu  ,...

.... na kuna uwezekano  ALIYEFAULU  hajisikii kafeli kwa kuwa kaegemeza mitazamo yake mbali na YALE  aliyofeli.


Na kama  MTU anajisikia KAFELI,...
.... akumbuke tu  KUFAULU kupo tu,...
.... .... na kiendeleacho  ni labda kabobea katika kuangalia zaidi ayatambuayo kama KUFELI.

Swali:

  • Si  katika  MTU alilofaulu  akijichunguza bado MAISHANI anaweza kustukia nini alichofeli na ndio maana hata mtu ajulikanaye kwa kufaulu KISIASA kama NELSON MANDELA  bado anakiri wakati anafanikiwa KISIASA , kifamilia ALIKUWA anafeli  kitu kilichofanya ndoa zake mbili kufa na watoto kulelewa bila BABA?


  • Na si unakumbuka hata MOTHER TERESA yasemekana alikuwa anaona wale WALIOONEKANA na JAMII kuwa ndio waliofeli kimaisha  na kuwa masiki kupindukia ndio ambao KIIMANI  walionyesha kufaulu zaidi kuwa karibu na MUNGU?
  • Na si nasikia hata katika LIFAULIWALO/Lifaulwuo moja ya siri ya wafauluo HILO  ni kufeli katika hilo  bila kukata tamaa nakulifanyia kazi  hata kama ni  kimazoezi mara kwa mara  kitu kisahauliwacho na washabikiao  KUFAULU tu ?

Ndio,...
... labda tukumbuke  hakuna AFELIYE au KUFAULU  kila kitu,...
.... na  ni tabia tu zawatu  kuruka baadhi ya mambo kufanyacho  hapa DUNIANI kuna wenye lebo za kuwa wao WAMEFAULU,...
.... autu ni wale WALIOFELI:-(



Ni wazo tu hili MKUU!


Hebu BONEY M warudie-MALAIKA



Au tu Anjelique KIDJO naye arudie-MALAIKA


Halafu tu tena BONEY M wazime kwa-JAMBO BWANA/Hakuna MATATA


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Rachel Siwa 8:46 pm  

Hakika neno limenigusa mtu wangu!

Goodman Manyanya Phiri 10:46 pm  

Kusema ukweli hamna mtu anayefeili duniani, bali mtihani mwenyewe unashindwa kumwuliza maswali ya kumfaa ili aonyeshe werevu wake....


Ama walietunga mtihani walitunga masuali na huku labda wamelewa.... si uliwahi kumuona hata yule muliemtegemea anazo akili sana ndie awe wakwanza kufeili...?


Ama mwalimu mwaka mzima "bishoo" tu...

Ama mwanafunzi mwenyewe "kenge" tu. Na kama angekuwa huyo kenge, basi hata kuja chuoni asingekuja hata kuja.


Q.E.D.
Mwanafunzi hana hatia wala udhaifu wowote ule HATA KIDOGO KATIKA HILI LAKUFEILI. Hata wale waliofeili katika ndoa zao kama babu... mie nawafariji sasa... waliishia kwa kupata dogodogo zaidi, Wasema Nini Mkuu Simon?

Simon Kitururu 11:51 am  

@Rachel: Tuko Pamoja!

@Mkuu Goodman:Ndio Haaapoo!

Lakini bado kuna wapimao kwa kuangalia kuwa kama tuna mwalimu mmoja , tuko darasa moja, kitabu kimoja basi yastahili tuwe na maksi moja.

Rachel Siwa 8:03 pm  

Hahahaha kaka zangu nyie mna Maneno haswaaa kama sijapata kuwasoma siku haiendi sawa!!!Ninge kuwa mtunzi wa Hadithi ninyi mngekuwa wa kwanza!! Tena kaka Manyanya unafaa kuwa Mshenga wa kaka Kitururu,Kwani nitaanza kampeni si muda mrefu ya KITURU NA KUOA!Pamoja sana tUU.

Simon Kitururu 8:46 am  

@Rachel: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP