Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kujitahidi SANA kuna wafikiao KUCHUNGULIA mpaka ambavyo WANGEANGALIA tu kwa kuwa DUKA la MZUNGU li WAZI!

>> Thursday, November 17, 2011

Yasemekana,...
....UKIJITAHIDI SANA,...

.... mara lukuki yawezafikia kuwa JUHUDI  SANA ziko katika KUJITAHIDI SANA  kuliko hata  katika ni nini kwa KUJITAHIDI UNAFANYA.:-(

Na yasemekana,..
... tuko wengi tu  ambao  kwa KUJITAHIDI SANA mpaka tunapofuka na kufikia  KUCHUNGULIA mpaka zile IHANA,...
...ambazo labda  tungeziangalia tu  na  KUSHUHUDIA mpaka ya firigisi na kitumbua makunyanzi  na kiponzacho ni JUHUDI!

Swali:
  • Unafikiri  wakati unajuhudi na HIKI hilo sio kikwazo  kwako kifanyacho huoni KILE?

Ndio ,...
.... LABDA,...
..... au tu ni LABDA saa nyingine LABDA,...
...... kifanyacho MTU au tu hata WEWE  hustukii mengine,...
.....ni JITIHADA ZAKO  na JUHUDI  zako  kwenye VITU  ambavyo labda sio hicho KITU kiwezacho kuwa ni muhimu KABISAAA kwako !:-(

SWali:
  • Unabisha?


Ndio,...
... ukijitahidi,...
.......LABDA saa nyingine labda UNAJITAHIDI SANA mpaka  hata katika YAFANYIKAYO KIVIVU weye wayafanyia JUHUDI  mpaka yanaanza kuonekana ni MAGUMU  hata kwa wasio WAVIVU wa kufanya.:-(


Ni wazo tu hili NGULI!:-(


Hebu Inner Circle  wabadili kwa - Games People Play


Inner Circle wachokoze  zaidi mpaka wale WAKRISTO wa siku mojamoja kalika WIKI hata kama hiyo ni JUMAPILI na sio JUMAMOSi katika mtuno- One Day ChristianHalafu  tu INNER CIRCLE wazime kwa -BAD BOYZ

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 10:52 am  

NAKUNUKUU:

"Unafikiri wakati unajuhudi na HIKI hilo sio kikwazo kwako kifanyacho huoni KILE?" MWISHO WA KUNUKUUJuhudi zote zinatoka katika akili ya mtu. Tendo na wazo lolote lile la mtu ni mchango MZURI katika akili yake hata tendo hilo likiwa zuri au baya; hata endo au wazo likiwa ni lenye kusifiwa au kulaaniwa; hata likiwa lenye ujinga au busara.Juhudi zote ni nzuri tu kwako ili mradi hisia zako zinakutuma, na utapoteza nguvu na msukumo wakuwajibika ikiwa juhudi zako wewe wataka ziwe zinasahihishwa na jamii kabla ya kutenda!


Akili ni mfereji wa maji; na chochote unachokimwagilia mule kwa vyovyote lazima kitatiririka na mfereji mzima tu. Na mfereji mwenye kitu, hata kikiwa sumu, ni bora kuliko mfereji mkavu; kwani mfereji mkavu hauna maana na waliojenga mfereji mkavu ni wajinga tu.

Binadamu asiyekuwa na juhudi, hata ikiwa juhudi mbaya, ni kama laana kwa Muumba wake!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP