TISHA TISHA ina MIPAKA na LABDA ndio maana HATA utishie UKIMWI ,ngono hatuachi NG'OOO!:-(
>> Thursday, November 10, 2011
Funzo kutoka kwenye TAHADHARI za hatari za UVUTAJI SIGARA ziwekwazo kwenye PAKETI za SIGARA , sigara yenyewe au hata kwenye MATANGAZO ya SIGARA zaonyesha kuwa ,...
......WATAKAO KUVUTA SIGARA asilimia za kutosha TU,...
... watavuta tu SIGARA hata kama wanajua na WAMETAHADHARIWA kuwa uvutaji wao SIGARA utawapatia SARATANI ya MAPAFU.:-(
Swali:
- Kwani unafikiri WAVUTA BANGI wangapi huacha kuvuta bangi kwa tahadhari wapewazo kuwa BANGI huleta KICHAA?
- SI walevi wanajua POMBE si CHAI?
- Na kwani unafikiri swala la NGONO PUMBAVU kuwa chanzo cha uenezaji UKIMWI latisha wahusudu NGONO asilimia ngapi ambao wanafanya kazi katika N.G.O . za ``TISHATISHA UKIMWI UNAUA´´ ambao kazi yao ni kinyume na NGONO pumbavu waendekezazo wakati wako katika ZIARA za kikazi ya KUELIMISHA watu watishike na UKIMWI?
Ndio,...
.... na labda TISHATISHA inamipaka yake KIMAFANIKIO,...
... kwa kuwa kwanza WATU TWATISHIKA kwa vitu tofauti kitu kifanyacho hata UCHOCHORO ukutishao ule wenye GIZA kwa mwingine ndio mahali pazuri pakujibanza BILA WASIWASI kiofisi ya kazi maalumu kwake ya UPORAJI waogopao HUO uchochoro.:-(
Swali:
- AU?
Ndio,...
... TISHATISHA ina MIPAKA katika KUTISHIA kitu mtu,...
... kwa kuwa labda pia kwa baadhi kilengwacho kutumika kama TISHIO ilikusitishwa ,...
... hichohicho ndicho kifanyacho MAISHA ya MLENGWA kuleta MAANA.:-(Swali zaidi:
- Na si wakati mmoja anatishia mtu atakufa labda kuna ambaye ALENGWAYE NA KUTISHIWA KIFO ambaye kufa ndio kitu kiletacho maana KWAKE na ni poa kwa kuwa NAAMINI ndio staili ya kwenda mbinguni kiaina?
Ndio,...
.... ukikosea WAKULENGA na ulengacho kama TISHIO ,...
....... KITISHO CHAKO chaweza kuwa ni KICHEKESHO kwa kuwa UTISHACHO NACHO kwake hukitambua kama Ze COMEDY.:-( Hebu DJ JESUS aanzishe kwa-Homem Casado
Tuga Agressiva na Titica waongezee dozi ya pambio kwa - MOTO
Halafu Gata Agressiva wazime kwa - Fula Mupepi
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
mmmhhh!!
Post a Comment