Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUJICHEKESHA wakati UMEKASIRIKA labda ni DHAMBI!

>> Tuesday, November 01, 2011

 Kumbuka tu  kuwa ,...

.... ajichekeshaye kwa ALIOWAKASIRIKIA matokeo ya kitendo hicho  ni pamoja na KUKASIRIKIA WASIOHUSIKA ambao hawajamuudhi mtu ,...

...... na  ndio maana kuna wenye VISIRANI  na  wanafunzi  wenzao  wasiohusika MASHULENI  kisa  wameudhiwa na shoga  nyumbani na wala hawako  mwezini ,...

....na waudhiwao na wenye hasira kwa WAFANYAKAZI WENZAO wakati tatizo labda liko nyumbani ambalo labda ni mpaka lile la BABA WATOTO wao  kuwa na mchezo wakutaka kupewa bata  a.ka JICHO / unyumba wa sehemu zitoleazo haja kubwa  kitu wasichopenda na matokeo yao ni visirani  kwa wasiojua hata tatizo  ni nini MAKAZINI zaidi ya kuhisi mtu yuko ana VISIRANI vya KIUTU UBAYA na labda yuko kama yuko kwenye SIKU ZAKE  kila siku kitu kisicho kweli ,...

... na bila kuwasahau hata pia  wale WANAFAMILIA wajikutao wananyanyasika na VISIRANI vya WAZAZI  kisa wamekasirishwa makazini   na kujifanya wanachekelea na kuja kulipuka MAJUMBANI,...

.... yote tu  IKIWA ni kutokana na dhambi ya  MIJITU  kujichekelesha inapotakiwa KUKASIRIKA na na kutolea stimu za MIHASIRA YAO kusikohusika.:-(

Swali:
  • Si  shoga mpashe tu hukohuko aliko kukasirisha mihasira yako iishe BABU WEE na sio kutuletea visirani vyako tusiohusika na kutusuta hata kwa yasiyohitaji kusuta?
  • Kwani  unafikiri HASIRA za MUNGU kwa SHETANI anazielekezea kwa BINADAMU aliyezaliwa na kukuta maugomvi yao tayari DUNIANI?
  • Kwani unauhakika DHAMBI  ni nini na je MIPAKA ya dhambi ni ipi?


Ndio,...
..... tukiacha utani,...
.... labda hata wewe UNACHEKEA wasio stahili BATASAMU LAKO mwanana mara KEMKEM kitu kifanyacho kuwa labda kuna ukweli  MIASIRA YAKO  saa nyingine unaelekezea kwa vibonde wasiostahili!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(Au tu tubadili kwa kusikiliza  FELA KUTI na MICHAEL wakichanganywa kwenye -"Human Nature" vs "I No Get Eye For Back"Hebu  FELA aaanzishe upya tena kwa-Lets STARTSamahani ngojea tu FELA KUTI arudishe na - Sense WisenessHalafu Fela Kuti azime dozi kwa kulainisha tena kwa-Waka Waka


1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:05 pm  

Simon! hakika ulichosema ni kweli kabisa kilinipata wiki iliyopita rafiki mmoja alikuwa si yeye kabisa mihasira si mchezo...lakini alikutana na kapulya ...wengi wanasema mtu akikasirika mwache lakini pia ni vizuri kuongea naye kwani ndo atatapika/ongea kile kinachomsumbua ila usimwendea pupa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP