Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hakuna kitu ``KISWAHILI FASAHA/sahihi DUNIANI´´.

>> Tuesday, November 01, 2011

 Ndio,...
... labda  kuna wapendelewao tu kuwa waongeavyo KISWAHILI ndio sahihi kisa LAFUDHI zao TAMU kwa BAADHI  hata wasipokuwa wanatongoza kwa kuwa:

  • Kiswahili  kama LUGHA YOYOTE ILE  ile , ni LUGHA  ambayo haijaganda na  lisilosahihi LEO katika LUGHA yoyote ile jamii  ikibadilika kwa kuwa nayo haijaganda kimatumizi ya lugha -labda KESHO laweza kuwa SAHIHI kifasaha kabisa.
  • Kiswahili kama sio LUGHA  iliyoganda (STATIC) inamaana kuna maneno tayari ambayo yashakufa hata kama yaliwahiitwa ni KISWAHILI na matumizi yake leo-  labda yatumie tu kama hutaki kueleweka uongeacho ni KISWAHILI
  • Na pia UFASAHA wa kitu  ni kitu kitegemeacho  mtumia lugha  anaamini ni  nini FASAHA -kwa kuwa UFASAHA wa wataalamu wa LUGHA yawezekana kabisa UFASAHA wao unaleta maana tu wakiwa na wataaalamu wenzao wa LUGHA waaminio  wakabilicho ni FASAHA kwa vigezo vyao ambavyo labda sio vile vya ufasaha uliopo kwenye jamii itumiayo KISWAHILI siku hadi siku kwetu KIGOMA.

Tukiachana na hilo:
  • Na kwani  si LAFUDHI  za watu ndio kwa wengine hufanya eti WAPWANI ya AFRIKA MASHARIKI waonekane  KISWAHILI CHAO ni sahihi zaidi  kuliko  kile tuongeacho sisi WAPARE kule kijijini kwetu MBAGA ,MANKA -au tu kile cha KIHAYA kuliko hata vigezo vingine ambavyo hata kitaalamu hugeuza lugha kuwa SAHIHI?
  • Na KISWAHILI si ni LILUGHA lenye kuanzia KIRENO, KIARABU  mpaka KIMASAI ambazo ni LUGHA  zisizo za KIBANTU kama KISWAHILI kisingiziwavyo misingi yake- misingi ambayo ndio siri ya UTAJIRI wa KISWAHILI?
  • Na kwani unafahamu  hata MTU MMOJA DUNIANI  aongeaye kwa asilimia MIA  KISWAHILI fasaha?


Ndio,...
... ukichunguza utastukia,...
... hata NYERERE alikuwa akiongea  maranyingine kwa kutumia maneno ya KIZANAKI  wakati anaongea KISWAHILI  - kitu kilichofanya kuwe  na mchezo wa kugeuza maneno hayo kuwa ni ya KISWAHILI na hapo ni bila kuruka  ukweli kuwa ukimsikiliza  hata huyo NYERERE aliyesifiwa kwa kujali KISWAHILI kwenye hotuba zake za KISWAHILI,...

... utastukia dalili zote za  fulu KISWANGLISH.:-(

Swali la KIZUSHI:
  • Kwani hufikiri  labda matumizi ya BABA wa TAIFA Mwalimu NYERERE  ya KISWAHILI yalikuwa na misingi yake kwenye SIASA zaidi ya kupenda LUGHA?

Ndio,...
... ni uchokozi tu huu MHESHIMIWA,...
...usikonde,..
.... ingawa labda ni kweli kuwa hakuna KISWAHILI SAHIHI  au FASAHA DUNINANI ,...
....ila kuna KISWAHILI kitamu  na KIZURI  na kama unaelewa liongelewalo LUGHA ilikuwa imetanua vyakutosha LAWALAWA kilugha!

Hebu tubadili WAZO kwa kumuachia tena Pachanga alete tena ndude- Calienta



Don Omar aongezee - Danza Kuduro



Halafu tu tena Daddy Yankee azime hapahapa Puerto Rico kwa- Gasolina

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 6:53 pm  

Ahsante sana kwa somo tamu Mtakatifu!!

Rachel Siwa 10:28 pm  

kaka Simon umenena Yakheee!!!vipi hapo mtu wangu?duhh kila nikiandika naona sio sahihi, jee ok HAKUNA KISWAHILI FASAHA/SAHII!!!!!UBARIKIWE MPARE WEWE.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP