Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BONDIA ALLAN KAMOTE KUMVAA MKENYA JUMAPILI

>> Thursday, November 03, 2011Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania , Yasin Abdallah , amesema  novemba 6 mwaka huu bondia machachali kutoka Tanga Allan Kamote atapambana na bondia Fredrick Nyakesa kutoka kenya katika mpambano wa kimataifa wa kirafiki utakaofanyika katika ukumbi wa Ridoch mkoa wa Tanga na mabondia hawo watapambana katika pambano la raundi 8 la uzito wa kilogram 61.2 light weigth yasin alisema kutakua na mapambano ya utangulizi mengine yatakayowakutanisha mabondia kutoka tanga na Dar es salaam

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D

--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam TanzaniaNimetumiwa na :
SUPER D

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP