Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika HAMU ya VIJISENTI!

>> Friday, November 04, 2011

Ndio,..
.... yasemekana hakuna BINADAMU aliyezaliwa FISADI,...
... na yoyote yule anaweza kuwa FISADI  kitu kiwekwacho uzito na ukweli kuwa karibu MAFISADI wote uwajuao wenye VIJISENTI vya WIZI au hata tu ambao wanalia ofisini  huku bado hawajastukia kuwa waliavyo ofisini ni WIZI;...

... bado ukweli uko palepale kuwa WAINGIAO OFISINI ambazo zina FWEDHA,...
...huwa yasemekana hujistukia HUMOHUMO  ofisini  kuwa wanapenda VIJISENTI na kama KIUHASIBU wamestukia hawatastukiwa WAKIDOKOA  ,...

....hujichukulia vyao MAPEMA huku wengine wakiahidi WATAENDA KUTUBU  makanisani  au tu kwa MIUNGU YAO baadaye!:-(

Swali:
  • Unauhakika hutaki VIJISENTI?
  • Unauhakika VIJISENTI vikigalagala mbele zako  hutadokoa kama hatutajua?
  • Lakini si unakumbuka pia  hata yaliyowazi kama TITI  na MWANA  kuwa sio kila mtoto azaliwaye hupenda TITI la MAMA na ili ale kikunyonyeshwa ni bonge la shughuli kwa MAMA mnyonyeshaji?Ndio,..
... labda kumbuka tu tena kuwa,...
...karibu  asilimia  mia ya mafisadi hawakuzaliwa MAFISADI,...
... na hustukia tu kuwa wamegeuka MAFISADI baada ya kuanza kuitwa MAFISADI,...
.....LAAAKIIIINIIII!!:-(NDIO ni  wazo tu hili NGULI!
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Mheshimiwa!

Hebu COSTULETA aanzishe upya  kwa - Do Milindro


COSTULETA apenyeze kachumbari zaidi tena na - LADJUM
Costuleta apandishe mita za dozi  zaidi kiujazo kwa - Tchiriri


Au tu tusiende mbali Dj Anjo Negro aingilie kati na kuzima kwa miondoko hiihii ya KUDURO kwa ndude pana kikishimo ile -Chuco Chuco


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

maisha ni mikikimikiki 1:59 pm  

Hata hivyo,wale ambao wameazimia kuwa matajiri huanguka katika jaribu na mtego na tamaa nyingi za kijinga na zenye kudhuru, ambazo hutumbukiza watu katika maangamizi na uharibifu. Kwa maana kupenda pesa ni chanzo cha mambo mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo wengine wamepotoshwa kutoka kwenye imani nao wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi._Timotheo 6:9,10.

maisha ni mikikimikiki 2:08 pm  

Wikiendi hii iwe njema sana kwa mtani wangu Simeon na wadau wengine wote.
=====================================
"UBAYA HAUNA KWAO LAKINI WEMA HAUOZI"
====================================

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP