Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ya KINYAA CHA MTU kisa katika STORI na PICHANI bata kaharisha!

>> Thursday, November 10, 2011

 KINYESI kwenye  PICHA itiayo KINYAA mtu ,..
.... kama tu kwenye STORI za WATU zitiazo KINYAA mtu ,...
.....huwa HAKINUKI ingawa kwa kuwa kuna wenye KINYAA,.....
.... hata stori za USHUZI  TU  kuna wakunjao  USO  utafikiri wamenusa harufu MBAYA,...
....eti WANAKINYAA.:-(


Swali:
  • SI  umestukia harufu nyingi ni za KUFIKIRIKA kutokana na MAZOEA tu  yafanyayo  watu  hata KISAIKOLOJIA  WANUSE na  kufananisha na wajuavyo VYATIA KINYAA kitu kifanyacho wafanikiwe kusikia KINYAA?
  • Na  si umestukia YA PICHANI bado  KIAINA labda  yako  kwenye hiyo PICHA  TU kama  ya SIMULIZI yawezavyo kuwa kwenye SIMULIZI TU  na kihalihalisi kwako hayapo na hutakutananayo?


Ndio,...
....KIAINA,...
... ya SIMULIZI kama tu  yalivyo kwenye  TV/LUNINGA,...
.... ayapayo MAISHA na kuyafanya yawe HALIHALISI / YA KWELI hata kwa KIKUHUZUNISHA kama sio KIKUTIA KINYAA,...
.... labda ni WEWE mwenyewe kwa jinsi uyaoanishavyo na HALI HALISI itiayo KINYAA.:-(

Swali:
  • Si ili  hata utishike na SINEMA ya KUTISHA labda yahitaji uoanishaji  wako  wa UONACHO na KUSIKIA na ujuacho KINATISHA kwenye UBONGO WAKO?


Na ndio,...
.....LABDA  kinyesi  kisipooanishwa na mavi na MKULIMA ,...
....kwa MKULIMA hicho hugeuka MBOLEA NZURI tu  na wala isiyotia kinyaa na itafutwayo kwa juhudi KABISAAA  BILA KINYAA kwa ajili ya bustani ya NYANYA  za KACHUMBARI uipendayo!:-(


Ni wazo tu hili MKUU!

Meiway hebu aanzishe upya kwa - Les Genies Vous Parlent


Halafu hebu tu Vusi Mahlasela arudie-When You Come Back/Ndakupenda Sana


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP