Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SI muda mrefu uliopita TANZANIA ilikuwa ni UHUNI kwa WANAWAKE kuwa WANAMUZIKI !

>> Thursday, November 03, 2011

SI unakumbuka sio MUDA mrefu ni WANAUME tu TANZANIA walioimba kama WANAWAKE kwa kuwa MUZIKI wa DANSI waimbaji wakike hawakuwa LUKUKI na kiaina JAMII ilikuwa inaona ni MAMBO DUKINAA?

Ndio ,...
... si muda mrefu ulio pita kuwa LADY JAYDEE au tu RAY C ,...
......ilikuwa ni kutojiheshimu kwa MWANAMKE

Hebu tusikilize mwanamume katika  Orchestra Makassy  katika ndude -Mume wangu
DDC Mlimani Park Orchestra waingizie ~ Mume Wangu Jerry
Au na hebu Maquis du Zaire nao warudie - KarubandikaSwali:
  • Si nasikia mpaka sasa hivi kuna wengi waaminino  ni UHUNI kwa WANAWAKE kuwa wanamuziki au tu hata wasanii wa maonyesho?
  • Si nasikia pia siku hizi DUME ZIMA  likiimba kihivi(KUWAKILISHA WANAWAKE kistahili hiii ya kulilia wanaume ) kuna watakaofikiria KIDUME anananiliwa kisenge?
  • Hivi kwani uanamuziki sio UHUNI katika jamii ya KITANZANIA siku hizi hata kama mtu unakojoa na kishikikacho huku umesimama?

DUH!
MUDA KIBOKO!

Ya kawaida leo huweza kuwa tofauti sana katika mtazamo wa watu si MUDA MREFU UJAO  kama tu jinsi ilivyokuwa katika hili sasa ambavyo VIGOLI kwenye fani ni LUKUKI kiheshima tu KUIMBA kwenye vilabu hata vya sebule zetu majumbani!

NI HILO TU KAMANDA!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP