Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

VIVA KAMANDA LOWASSA

>> Saturday, November 26, 2011
 LOWASSA KUANZA KUANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND KWA KWELI NAONA ANAFANYA KILE NILICHOWAHI KUTABIRI KWENYE MAKALA YANGU YA "LOWASSA SEMA NENO MOJA TU"

...NIMEAMUA KUMTUNGIA SHAIRI HILO HAPO CHINI...

Kalamu yangu nashika, shairi nakutungia
Kamanda umeongea, kiwingu umeondoa
Hukutaka kusinzia,makosa kuyarudia
Jibu umetupatia, viva kamanda LowassaMwananchi nimesoma, la jana nilinunua
Machoya yakatuama, dukuduku umetoa
Uliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutia
Jibu umetupatia, viva kamanda LowassaRichmond kupasua, mapema uligundua
Kikwete ukamwambia, mkataba kuondoa
Rais akakataa, nini alitegemea?
Jibu umetupatia, viva kamanda LowassaNape akashikilia, lile asilolijua
Mikoani kaambaa, uzushi kang’ang’ania
Jinalo kulichafua, wewe ukavumilia
Jibu umetupatia, viva kamanda LowassaMapema nilitabiri, falsafa nikapinga
Magamba sikukariri, kuvuana sikuunga
Ukweli niliukiri, mantiki iso kunga
Jibu umetupatia, viva kamanda LowassaBeti sita nakomea, kalamu naweka chini
Mengi nimeongelea, soma tena kwa makini
Yatazidi kutokea,kusini kaskazini
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.


Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,
Tanzania, East Africa
Jumamosi, November 26, 2011

Nimetumiwa hii nanihii na:
Nova Kambota

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP