Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika TAFAKURI za wafikiriao KUISHI MIAKA MINGI ni KUFAIDI MENGI kiaina!

>> Thursday, November 10, 2011

Ndio,...
... kuna WAHURUMIWAO pia na KUHUZUNIKIWA kwa kuwa,...
... hawakula CHUMVI nyingi  kabla ya  kuanza kivyao kwa  staili ile ya  KUDEDI.:-(

Swali :
  • Si  kuishi MIAKA MINGI kwa WENGINE  maana yake ni``JAMAA LILIFAIDI LILE ?´´
  • Katika HAMU YA KUISHI miaka MINGI umewahi CHUNGUZA matatizo  ya WALA CHUMVI NYINGI?
  • Lakini  si KUISHI  miaka MINGI  maana yake  pia ni KUZEEKA sana kitu ambacho kuna WASIOPENDA?
  • Si kwa kula chumvi nyingi kuna warudiao NEPI tena?

Na labda,...
.... kuna WASAHAUO kuwa KUISHI  KUREFU labda  wala sio TIJA  na FARAJA kwa  AISHIYE MAISHA MAREFU  hasa kama AFYA na HALIHALISI ya KIMAISHA ndio HIVYO TENA  kitu kifanyacho labda KUISHI KUREFU kukawa maana yake ni KUTESEKA  kwa muda MREFU kiaina.:-(

Swali KIAINA:
  • Unakumbuka kufaidi VIWEZEKANAVYO sasa hivi hasa UKIZINGATIA miaka izidivyo labda VIWEZEKANAVYO  SASA uviwezavyo kuvipindia mgongo yawezekana ikawa ni tatizo  kuwezananavyo baadaye kisa UMRI wafanya mgongo unauma?

Ndio,...
.... kuishi kwingi  ni KUONA mengi,...
..... kitu ambacho  pia LABDA ni kuongezea muda wa KUJUTIA URUKAVYO kufanya sasa hivi UVIWEZAVYO SASA HIVI  ambavyo havitawezekana siku UKILA CHUMVI NYINGI.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!





Hebu Baaba Maal abadili wazo na aanzishe upya kwa - Miyaabele




Baaba Maal azime - Three Little Birds


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP