ALMASI na MCHANGA -bado LABDA ni MCHANGA ambao ni MUHIMU zaidi kwa BINADAMU hata kama kunawasiouona SPESHO!
>> Sunday, November 13, 2011
Na kitu SPESHO kuunganishwa na uchache wake ,...
.... labda ni tatizo tu lijengwalo na WATU kuoanisha WINGI na UKAWAIDA ,...
..... kitu kifanyacho kufanya watu kutafsiri kama kitu kina WATEJA WENGI wafanikiwao kukipata kugeuka mpaka zaidi ya KAWAIDA,...... KITU KIFANYACHO kama hicho kidude ni UKE basi ni ule wa MALAYA.:-(
LAKINI:
- Si umestukia kuna waoneao wivu vitu MAARUFU kwa kigezo cha kuwa hupendwa na WENGI?
- Kwani tofauti ya KUPENDWA na WENGI na KUGAWIA wengi kitu si hutegemea na tafsiri tu ili HASI igeuke CHANYA?
- Na si unakumbuka kuwa pia kutokupendwa na WENGI huweza kugeuza hicho kitu kisichopendwa kuwa SPESHO?
Katika DUNIA izidiyo kuona na kutambua MMOJA MMOJA na MOJAMOJA kama SPESHO,...
..... unaweza kushangaa vingi vilivyo kwa WINGI labda ndio kwa wengi ndio MUHIMU hata kama hawavitambui kwa wingi wake kuwa ni SPESHO.:-(
Swali:
- Kwani KIPENDWACHO au APENDWAYE na wengi kigezo kikuu ni umuhimu?
- Na si yasemekana ukichunguza waweza hitimisha KILA KITU na KILA MTU ni SPESHO kivyake?
Na VINGI kwa WINGI vinamchezo wa kurukwa kwa vigezo vya USPESHO,...
... ingawa kiumuhimu labda bado MCHANGA ulio MWINGI ndio MUHIMU kuliko ALMASI chache zibebazo sifa ya USPESHO machoni mwa watu,...
.. kitu ambacho kikijengewa hoja vizuri,...
.. hitimisho laweza kuwa MCHANGA kiumuhimu ndio SPESHO zaidi ya ALMASI.
NI wazo tu hili KINGUNGE!
Hebu MwanaFA aanzishe upya kwa -Bado NIPONIPO
Profesa J aingizie-Hapo SAWA
Au turudi tu KENYA ili CANIBAL na SHARAMA wazime kwa-KICHWA KIBOVU
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Duh! bonge la wazo:-) jumapili njema mkaka!!
@Yasinta: Jumapili njema kwako pia mtoto mzuri!
Post a Comment