....Wanasiasa wanachukuliwa kama VICHEKESHO na WACHEKESHAJI wanachukuliwa siriasi!:-(
Kama unaona nachoona na KUSIKIA NACHO SIKIA siku hizi,....
...... unaweza kudhani MWISHO WA DUNIA umefika mpaka usome HISTORIA na kustukia dhambi nyingi zistukiwazo ZILISHA ANDIKWA KUWA ZINAFANYIKA tokea kabla ya enzi za kina YESU na kuna waliodai dunia imefikia mwisho enzi hizohizo wakiwa tu vilevile siriasi.:-(
Swali:
Unafikiri akina FARAO wa MISRI nao hawakuwa na kitu wakiitacho SIKU HIZI?
Kuna uwezekano IDADI YA WATU imekuwa sana siku hizi,...
... na ukichanganya KITU HICHO na TEKINOLOJIA ZA HABARI zisababishavyo mpaka UDAKU KUPATIKANA kirahisi ,....
... labda kuna tunayoyasikia TU zaidi SIKU HIZI ingawa yalikuwepo tu hapa DUNIANI toka enzi za madanga chee.:-(
Swali watu wenye imani fulani :
Unadhani baada ya ADAMU na EVA kufanya dhambi ya kula tunda , dhambi yao iliyofuata ilikuwa ni nini?
Ushawahi kusikia msemo hakuna jipa chini ya anga na kama KITU hakijafanywa na MTU basi kimefanywa na angalau mjusi?
Ndio,....
.... kama unasikia nachosikia na KUONA NACHOONA,...
..... labda kibadilikacho hapa duniani ni staili tu LAKINI MAMBO NI YALEYALE,...
....kama tu salamu kubadilika KUTOKA ``Mambo dukinaa! ´´ kwenda ``Mambo POA!´´ na salamu YA KISASA kuwezakwenda mpaka kuwa ``Mambo Kukojolea dodoki!´´ - lakini zote zikimaanisha JIBU la salamu HIYO HIYO ya tokea enzi ya kuwa ``Mwenzetu hujambo lakini!´´.:-(
Ndio,....
.... kama unasikia na kuona nachoona,...
..... labda HATA udaku ni uleule kibadilishwacho ni MAHALI lugha tu itumikavyo au itumikayo.:-(
Na haki ya nani labda mambo ni kama SURUALI ,...
...iwe ni PEKOSI , kodrai au hata JEANS ya nailoni lakini vyote ni suruali na kupendeza au kutishwa na jinsi suruali imbinyavyo tako mtu HUKO KUKO tu machoni mwa mtazamaji na LABDA hakuna WATAZAMAJI wawili WAONAO na kuoanisha suruali na muonekano wa tako sawasawa.:-(
NI WAZO tu la GHAFLA MHESHIMIWA na wala usikonde kama unauwezo wa kula BAGIA !:-(
Namuachia SADIKI aendelee katika-Do You Hear What I Hear
Au tu Rick James abadili zaidi kwa ndude -Cold Blooded
.... yaweza KUSAHAULIKA kuna watu WASIOPENDA KULA pia DUNIANI.:-(
Na akisikilizwa KIDUME mpenda WANAWAKE,.....
.... kwa muda fulani UNAWEZA kusahau kuna wasenge pia DUNIANI.:-(
Swali:
SI unakumbuka katika kiwanja cha MPIRA WAMIGUU unaweza kusahau uwezekano wa kuwepo washabiki wa NETIBOLI hapo?
Ndio,...
.... kwa kuwa WATU WENGI wanaelekea upande wa kulia USIJE TU KUSAHAU kuwa kuna AMBAO kwa makusudi yao kabisaa wanaelekea KUSHOTO ndio maana wakati una sikiliza stori za waenda MSIKITINI au KANISANI usisahau kuna waendeao UCHAWI PIA duniani.:-(
Ndio ,....
... labda APENDAYE kula ndio anaweza stukia matatizo ya KUPIKA na kuosha vyombo na KIRUKA NJIA aliye chacha ndiye atakuwa anastukia matatizo ya gesti za migombani LAKINI na wachawi yawezekana pia wana matatizo yao tu kitu ambacho ni MCHAWI tu atastukia ni hali ya hewa gani kupaa kwa ungo ni shwari zaidi DUNIANI.:-(
Ndio,...
... labda wakati unasikia MALALAMIKO ya hili kumbuka uwezekano wa kuwa kuna MATATIZO YALALAMIKIWAYO ya lile lisilo kuhusu pia hapahapa DUNIANI.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(
Hebu Ray Barrettona Mongo Santamaria katika kubadili hali ya hewa kijiweni warudie - Congo Bongo
Kwa kuwa jamii ndio inaweka MIPAKA ya nini kisemwe,....
..... WAHESHIMIWA ndio wafao kisabuni kwa kuwa KIHESHIMA kiwakeracho wamejifunza kuwa huwa hakisemwi hadharani.:-(
Ili kisichozoeleka kisemwe,...
....yawezekana WAHESHIMIWA wajuaji inabidi waangalie upya ni nini HAKISEMWI ambacho KINAFANYIKA kwa kuwa tu jamii imeamua kiheshima hicho kitu kisiongelewe HADHARANI.:-(
Swali:
Si unajua kuna aliyepata mimba au UKIMWI kwa kuwa tu WAHESHIMIWA hawaongelei ngono kwa kuwa HAWATAKI KUDAKWA wakiongelea waaminicho sio tpiki ya kiheshima hadharani?
Hujawahi kuuonea wivu UHURU wa mtu apendaye kukusimulia ufikiriavyo ni vitu vya FARAGHA ambavyo wewe unavionea aibu mkiwa hadharani?
MIPAKA iwekwayo na HESHIMA,....
....kwa bahati mbaya inategemea mtu na mtu na ukiheshimucho kwa mtu mwingine wala HAKINA HESHIMA.:-(
Ndio ,...
.... kuna viheshimiwavyo kama tu TISHU CHOONI ambavyo hata TISHU IHESHIMIWEJE bado tumizi lake lisaidialo kuongezea heshima ya mtu hubakia ileile ya baada ya shughuli nzito TISHU ndio itakayogeuzwa kichambio.:-(
Swali:
Si unafahamu TISHU nayo inaheshima zake za kimakokoneo?
Hebu Erykah Badu abadili kwa kitu- Window Seat
Erykah Badu arudie ndude - Didn't Cha Know
Au tu Outkast na Slick Rick walete tena ndude- Da Art Of Storytellin Read more...
...kumbuka labda hicho KITU kimesha kupa uprofesa wa kuosha kitu chochote KILE.:-(
Swali:
AU?
Si unakumbuka CHOO KINUKACHO ni matunda ya kazi za uchi hata zifanywazo kiheshima na MHESHIMIWA?
Ndio,...
... sikubishii HASA kama umeshawahi kufikiria WAKATI ukipenga MAKAMASI ushikacho ni MAKAMASI.:-(
NAACHA MUELEKEO wa wazo nisije kugusia kugusia BURE mpaka nyanya za kachumbari uzipendazo zipendavyo kucheza na mbolea ilio oza kuliko kucheza na wewe.:-(
NI HILO tu na haki ya nani wazo hili la TARALILA halijafanyiwa utafiti wa kina na limeruka vyoo vinukiavyo vizuri bila kunyunyiziwa manukato .:-(
JUMATATU NJEMA MHESHIMIWA!
Hebu tubadili kwa kwenda YEMEN kuwasikiliza wanawake washabikiao kuoongezea shughuli kwa watoto katika ndude-The right to marry as a child
Au hebu Marijani RaajabnaFresh Jumbe waangushe ndude - Masudi
Ndio,...
... aliyeandika taralila yenye neno lisilo LAKIHESHIMA kwa baadhi ya waheshimiwa ni huyuhuyu mimi kama HUYU MIMI aonekanavyo kwenye picha zifuatazo akijitafutia matatizo na halafu akinunia MATATIZO baada yakustukia alivyojiongezea.:-(
TUKIMGEUZA PANZI KUWA nzige au tu BIN -adamu MKUBWA,...
..... labda kuna BINADAMU anaweza kukumbushwa kwa HII TARALILA kuwa MWANAMKE na MWANAUME sio UBINADAMU kwakuwa pia kuna MBWA MVULANA ingawa labda ni BINADAMU ambao inabidi waoshe UANAUME au UANAUKE kwa kuwa wanamchezo kuwa wasipojiswafi watanuka zaidi ya KIKWAPA.:-(
SWALI banangenge:
Unauhakika UKE ungekuwa rafiki ya UUME kama PANZI asinge ugeuza kuwa ni MATUMIZI?
Unafikiri CHAKULA kinaupenda MDOMO WA PANZI hata kabla ya kugundua hata kisichokuwa nia ya panzi ni kugeuza CHAKULA CHA PANZI mavi?
Ushawahi kufikiria kuuangalia UKE WA PANZI kwa kuwa hata PANZI DUME havai chupi?
NI WAZO tu lililopinda MHESHIMIWA na kama umenisoma mpaka hapa SHAURI YAKO miye simo!:-(
JUMAPILI NJEMA MHESHIMIWA !
Ngojea Teddy Pendergrass adai - It Don't Hurt Now
Au tu The Isley Brothers warudie - Contagious
DUH Makassy MASIKIONI ananilazimisha niachie pia TENA ndude-Mambo BADO
... ni kwamba hurahisisha mpaka LILE TATIZO ULIJUALO LINAMKERA MHESHIMIWA liwekwe pembeni kwa kuwa kuna FARAGHA na kufanya lile tatizo ambalo hujui mtu analo likawa ndilo LINAPEWA KIPAUMBELE ambalo ni la MHESHIMIWA kujiangalia uchi kila nafasi ikitokea kutokana na kukwazika kwake ambako HADHARANI hakujulikani,...
...kuwa MHESHIMIWA anajihisi ana uchi wenye sura mbaya kitu ambacho ndicho kimpacho MOTISHA NA nguvu ya kukivulia gwaguro ilia KUJICHUNGULIA kuliko ILE MOTISHA YA KUDAI HAKI YA MNYONGE Mheshimiwa AJULIKANAYO KUITETEA kwenye hutuba zake zisizo kuwa faragha.:-(
LAKINI uzuri wa FARAGHA,...
...ni kwamba inaweza kukufanya UTULIE na kufikiri VIZURI jinsi ya kutatua MATATIZO YAKO na hata YA DUNIA kwa kuwa haubughuziwi na WAKUDA hapo KWENYE faragha.:-(
Swali:
Kwani unabisha kuwa kuna watu FARAGHA ZAO huzitumia zaidi kufanya vitu vyenye undugu na KUNUSA chupi zao ili kujihakikishia ni kweli mkojo wao ukivunda haunuki vibaya sana kuliko WAFIKIRIAVYO watajiinuaje KIMAISHA wakati maisha mazuri yanapendelea MAFISADI?
Unauhakika aamuaye kuloga mtu huwa anawazia hilo FARAGHANI au katika kijiwe cha wachawi?
Unauhakika FARAGHA yako huwa unaitumia kufanya vya faragha au unaitumia ZAIDI kuwaza maswala yenye undugu zaidi na kitu kama kati ya KITUMBUA na MAANDAZI nini ni TAMU TAMU KAMA SUKARI zaidi?
FARAGHAAAA!
NI kweli mawazo YA MTU yasingekuwa YA FARAGHA labda tungestukia MHESHIMIWA sasa hivi umuaminiye kwa ufundi wa kusali,....
...SASA HIVI anafikiria kikojoleo na baada ya hapo wazo HILO ,...
....kitakacho hitimisha siku ni lile WAZO lake la kila siku la kufikiria UBWABWA na wala sio jinsi gani Tanzania itapata umeme wa kuaminika au wataunyimaje UKIMWI usinenepe kama ifikiriwavyo na wamheshimuo MHESHIMIWA wafikiriavyo ndivyo MHESHIMIWA anafikiria.:-(
HILI NI WAZO TU na halijafanyiwa utafiti wa kina kwa hiyo kifaraja unaweza kulitukania ZAIDI ya SHENZI.:-(
Hebu Matonya abadili kwa kuongelea-Spair Tairi
Diamond alainishe zaidi kwa ndude-Kamwambie
Hebu Isley Brothers waje live na kitu -Between the Sheets
Au nimuachie tu na Notorious B.I.G a sample Between the sheets na kuifanya kitu kiitwacho -Big Poppa
....KIBONGE cha mpinzani wake ni KUWA mtu mwingine NAYE anaweza kutoa madai hayohayo kuwa HAKI YAKE ni kukunyima.:-(
Na kwa bahati mbaya MWENYE haki anaeleweka,....
... asipoelewa ni kwanini katika HAKI YAKE YA KUTAKA kuwe na mtu mwingine mwenye haki pia ya KUNYIMA.:-(
Na haki NISHAI,....
.... ndio maana wakati kuna ateteaye matumizi ya kikojoleo na bado haja fikiria kuwa KINYEO NACHO NI TAKWA kuna adaie haki ya matumizi ya kinyeo ambayo hataki yawe kisheria katika kifungu cha kimlazimishacho kisheria hicho kipengele kwa wakitakacho katika burudani au mahusiano KUKINYIMA.
Swali:
Unauhakika wakati unanyimwa unamfikiria akunyimaye ni kwanini ananyima saa nyingine kinukacho kipengele?
Na HAKI nishai,....
....ndio maana kuna wateteao DINI watakuambia mpaka ni upotofu wa maadili kwa jinsi HAKI ZA WATU ZIDAIWAZO KUKUBALIWA SIKUHIZI KUWA WANAPOINTI zinavyotukania maadili ya dini kwa jinsi wafuasi wajaribuvyo kuzielewa dini zenye maelfu ya MIAKA kwa taratibu za uelewaji wa IMANI wa isemekanavyo ni kileo.:-(
Na haki NISHAI,...
.... kwa kuwa haki za wengine zisipofanana na ZAKO wewe zaweza KUKUUMIZA NANIHIII na na kukupa nyege hata ile ya kilio.:-(
Swali la marudio :
Umewahi kunyimwa HAKI YAKO wakati unataka?
Kikubwa cha KUJIFUNZA ni kwamba ,...
.....baadaye BAADA YA KUNYIMWA unaweza kugundua ndio ilikuwa BONGE LA BAHATI NA MSAADA KWAKO,....
... uliosaidia HUKUGAWIWA UKIMWI kwa kuwa ulinyimwa na ndio sababu baadaye ukafaidi tamu zaidi MBIVU zile.:-(
Swali:
Umeshawahi SIKIA mtu aliyelalamikia kukosa USAFIRI anavyosifia BAHATI YAKE baada ya kusikia GARI LILILOMNYIMA LIFTI limeata ajali na wasafiri wote wame ZE DEDI a.k.a wamekufa na KUFARIKI?
Labda KIKUBWA CHAKUJIFUNZA ni kwamba,...
.....ucheleweshwaji wa HAKI za mtu waweza kuwa na fundisho angalau la nini hasa ni haki kwa ANYIMWAYE.
Si utani,...
... HAKI ZA WANAWAKE zicheleweshwavyo LABDA kuna kizazi cha VITUKUU zitafikia kusifia hilo kama sababu wanawake wamezidi NGUVU na UBABE WA NANIHII kuliko wanaume .
Swali:
Umeshafanikiwa wewe binafsi kumnyima MWANAMKE haki yake ?
Unafikiri mwanamke hajawahi kukunyima haki yako wewe KIDUME?
Umewahi kunyimwa?
Haki ni nini?
DUH!
Nimeacha na NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na NI ruksa kulibishia!
Hebu Macka BnaDada Kofi wajiunge na makundi ya watu waliozoea kusifia kwa ndude - Proud Of Mandela
Hebu tupumzishwe kwa MANDELA ikisemekana akishabikia watu weupe wauawe
Au hebu Baby ChamnaCarl Thomas wabadili mkao kwa ndude- Oh No
Asante WADAU wote tuliokutana juzi fulani ya hivi karibuni ambao baadhi ni hawa katika picha zangu...
Tukiachana na kununa na kumuangalia MCHUMBA MWENYE SURA MBAYA TULIYEMPENDA KWA TABIA wakati KANUNA anavyotufanya TUJISIKIE ,...
... labda twaweza MPAKA kustukia ,...
.... kama una-HUZUNI jaribu kujichanganya na wenye FURAHA ili uambukizwe ANGALAU kuchekelea HATA kanyau bila sababu.:-(
Swali:
SI unajua FURAHA nayo huambukiza na ndiyo isababishayo HUWA UNASHUHUDIA hata baadhi ya uwajuao kwa busara nao wakichekelea pia ujinga kisa wako katika mazingira ambayo komedi babu kubwa ni MTU kajamba?
Umefanikiwa kununa leo?
Ndio,....
..... kama unafuraha unaweza kuambukizwa KUNUNA kisa kila LIMTU likuzungukalo limenuna utafikiri kama limebanwa HAJA-kubwa halafu aliyeko chooni anachelewa kutoka na kuachia wengine nao starehe.ya kupunguza uzito MSALANI..:-(
NI HILO TU MKUU na ni wazo tu!
SIKU NJEMA Mheshimiwa!
Au hebu tumsikilize mgomvi Winnie Mandela
Au tu wa mahaba SHAKILA arudie tu ndude -Moyo unalia macho yanacheka
... ndio maana ukichunguza utakuta MPAKA kuna mtu anapenda wimbo FULANI kwa kisa tu unaneno TAKO.:-(
Na avutiwavyo mtu na wimbo kila mtu staili yake,....
....na kuna wadaio WIMBO MZURI sio mirindimo wala maneno na ni jinsi uwakumbushavyo KITU au MTU na hata wakikuimbia huo wimbo hawafikirii maneno yanasema NINI na yana MAANA GANI na haiwaingii akilini labda huo wimbo ni matusi KWAKO.:-(
Swali:
Kwani kwako wataka kusema wimbo mzuri ni ule uuelewao maneno yake tu?
Ndio,...
... kuna ambao uzuri wa wimbo ni VIDEO yake.
Swali zaidi kidogo:
Huwa unafikiria LAKINI ni kwanini unaupenda wimbo fulani?
SI unajua ni kawaida maeneo fulani kusikia nyimbo za KANISANI kwenye baa na kuna wajipozao baada ya kuzini kwa kusikiliza nyimbo mpya za dini?
Ndio,...
.... labda unavyosikiliza wimbo unachosikia ni VIPENGELE VYA MAISHA katika MAISHA YAKO VIGUSANISHWAVYO na wimbo na wala huusikilizi wimbo kama idhaniwavyo kwa MIRINDIMO YAKE na MANENO YAKE kitu ambacho chaweza kuwa KIMESHASABABISHA umewahi kuukatikia kiuno wimbo wa msibani badala ya kuufanya ukusaidie kutoa BONGE LA mchozi.:-(
....kwa kawaida kunatofauti kati ya WEWE na kisemwacho kuhusu WEWE hasa kwa kuwa hakuna akujuaye kama unavyojijua WEWE.:-(
Jizoeshe kukumbuka,....
...kuwa kukwepa kusikia USICHOPENDA KUKISIKIA hakibadili kuwa kinaendelea kusemwa USICHOTAKA KUKISIKIA - na kwa kuwa hata sasa hivi kinavyosemwa hakikuathiri LABDA hakina ATHARI SANA KWAKO KISEMWACHO hata kama sasa hivi ungekisikia kwa masikio yako MWENYEWE kwa kuwa hata sasa hivi KINASEMWA na labda asiyekisikia tu ni WEWE.:-(
Swali:
Si unajua labda sasa hivi kuna anayekuwaza vibaya na kukusema vilevile ingawa wala hilo halikuathiri?
Tatizo lijitokezalo ukisikia USICHOTAKA KUKISIKIA ni kwamba SASA UMEKISIKIA ,...
... lakini mambo yako vilevile kama tu kabla hujasikia KWA AJIAMINIYE kwa kuwa ni KWELI HUWA UNASEMWA hata kama KWA uwezo wa binadamu mdogo BINADAMU HUATHIRIKA pale tu agunduapo ANASEMWA.:-(
Kumbuka kama umefanikiwa mpaka KUSIKIA,...
.... kibaya kuhusu WEWE ambacho mpaka umekisikia labda HICHO hakina nguvu ya kukuua ndio maana mpaka UMEKISIKIA WAKATI UKO HAI na kupata muda wa kukionea aibu au kukiruhusu kukuumiza tu moyo kisa eti umekisikia KIKISEMWA .:-(
Swali:
Hufikiri kwenda KANISANI au MSIKITINI ni moja ya mazoezi ya waumini ya kusikiliza WASICHOPENDA kusikia kuwa kuna DHAMBI WAKATAZWAZO bado wao wanazisiki tamu?
Huwa unafanya masoezi ya kuzoea kukosolewa au unafarijika na kumnunia au kumtukania uchi unayemsikia anakukosoa?
Ndio,....
.... inauma hasa usiyemtegemea kuwa NAYE anakusema vibaya kwa kuwa ni NDUGU au RAFIKI YAKO,...
....ukimsikia kwa sauti yake anakuteta au tu anatukania matege yako wakati ulifikiri anafikiri unabonge la usafiri.:-(
Ndio,....
...... yawezekana moja ya SIRI YA USHINDI KATIKA MAISHA YAKO ni kukabili usiyopenda KUSIKIA hata YASIYOKUHUSU WEWE KAMA MTU kwa mfano ya JINSI IDAIWAVYO KUWA tu Michael Jackson alidai Tanzania YAKO inanuka kwa kuwa labda kuumia tu roho hakutakusaidia kitu UKIFIKIRI.:-(
Swali:
Si unajua hutaathirika hata ukisikia likitajwa jina la kitendo wazazi wako walifanya mpaka ukazaliwa ingawa hupendi hilo KUSIKIA?
NAACHIA HAPA zoezi la kukuzoezesha kusoma maneno usiyotaka kuyasikia!.:-(
Twende kidogo Kenya tukajifunze ya kutoa mimba
Au tu Fally Ipupa abadili zaidi kwa ndude-Ko ko ko
...ni muhimu kujifunza kutoka kwa waliofanya HICHO KITU kabla yako.:-(
Ndio inasemekana,...
....unaweza kutopoteza MUDA kwa kuingilia BIASHARA ya chipsi mayai kwenye eneo kama UTAJIFUNZA kwa waliotangulia kuuza CHIPSI MAYAI kwenye eneo na kujua kuwa wateja hakuna na wapitao hapo huwa wana ulizia UGALI na sio CHIPSI MAYAI ambayo ndiyo biashara unaelekezea mtaji wako.:-(
Na inasemekana;...
....utatatua tatizo la KUTUNZA MUDA kwa kutegemea kujifunza kutoka katika MATATIZO YA WENGINE na kuepuka kufanya matatizo kama ya hao wengine yawepia ni YAKO.
Swali:
SI umesikia kuwa INASEMEKANA kuna msaada UNAOTOSHA FUNDISHO kwa kujifunza kuwa ukishika moto utaungua kutoka katika stori za wengine waliowahi kuungua kwa kushika moto kuliko weye mwenyewe kugusa moto ukaungua?
CHAKUKUMBUKA tu ni kwamba,...
....aliyetangulia kufanya KITU anaweza kuwa alikuwa MFUPI KULIKO WEWE na stori zake za ugumu wa kufikia KIDUDE unaweza ukawa uliongezewa ugumu kwa kuwa STORI YAKE KATIKA UGUMU ilijumlisha na KURUKIARUKIA KITU KUTOKANA NA UFUPI WAKE iliafikie KIDUDE kitu ambacho hakitakuathiri wewe ambaye NI MREFU VYAKUTOSHA na huhitaji kuhangaika na mihitaji ya msaada wa kigoda ili kujiongezea kimo UFIKIE kidude.:-(
Swali:
Si unakumbuka WEWE sio YULE kwa hiyo ingawa ngoma ya SINDIMBA ni ileile yawezekana kukata kiuno KWAKO ni rahisi zaidi kuliko YULE kwa kuwa wewe una kiuno kama NYIGU na ujazo wa MAKALI YAKO unatosha zaidi NAKUIFANYA SHUGHULI YA kuitingishia ngoma MAKALIO kwako kuwa rahisi zaidi kuliko wengine wenye kiono kama kabati na makalio chapati ?
Ndio,....
.... kuna stori za waliofanya UTAKACHO KUFANYA ambazo zaweza kukutisha kwa kuwa umeambiwa ni jinsi gani zilivyo washinda watu,....
.... lakini kumbuka labda walioshindwa SHUGHULI walishindwa kwa kuwa hawakuwa na kitu ulichonacho ambacho ni MTAJI WA PESA na wewe ukiingilia shughuli waliyoshindwa unachohitaji ZAIDI ni mtaji tofauti wa KUTUMIA AKILI ambao nao unao na SHUGHULI ZILIZOWASHINDA WENGINE ukiziingia kivyako mambo yatakuwa mswano.
Swali:
Hujastukia kujifunza kutoka kwa wengine NDIO MOJA YA SABABU watu wengi huhofu kujaribu wenyewe hata wawiwezavyo?
Unauhakika hakuna CHA MANUFAA ujifunzacho kizuri kwa kuungua mwenyewe NA MOTO ili kujua maumivu ya MOTO badala ya kuogopa moto kwa kusikiliza stori za wengine za makali ya moto?
Kwa kifupi ,...
... labda kunakitu ulichojifunza kwa KUSIKILIZA STORI NA UZOEFU WA WENGINE,...
... ambazo ulihitaji kujaribu mwenyewe ili kujikwamua katika tatizo lakoLA SASA hata LILE la kuogopa KUTONGOZA MTU kwa kuwa anasifa za kunyima watu KUTOKANA NA STORI ZA WALIOJARIBU WENGINE ,....
....kwa kuwa labda KWA STAILI yako na kwa kuwa WEWE sio WALE ungekaribishwa katika ufalme na utukufu wa ukitakacho hasa ambao uko kwa UMUOGOPAYE kumtongoza.:-(
Kwa kifupi,...
....kwa kuwa CHIPSI MAYAI yasemekana haziuziki katika eneo yawezekana ni kwakuwa sio WEWE uziuzaye,...
... na ungeanzisha biashara ya CHIPSI mayai wewe na KWA UKARIMU WAKO ,usafi wa mgahawa wako, BONGE LA BATASAMU LAKO, na jinsi tu uwafanyavyo wateja wanajisikia wako nyumbani , ungeweza kufanya mpaka WAPENDA NGUNA aka UGALI waanze kuja kula chipsi mayai mahali ambapo wengine wanadai hakuna wateja.:-(
Swali:
Umeshawahi kustukia KUJIFUNZA KUTOKA KWA WATU WENGINE haina maana ndio ujaribu KUWAIGA HAO MTUZ WENGINE?
Ndio,....
.....kujifunza katika MATATIZO YALIYO WAKUTA WENGINE,....
... labda isiwe ni KUJITISHA TU kuwa kwa kuwa wengine walipata matatizo basi na MTU MWINGINE atakutana na MATATIZO hasa ukizingatia labda wengine waliona NI TATIZO kwa kuwa ilibidi waonge mwili wakati KWA MWINGINE ASITAYE KWA KUTISHIKA NA STORI ZA WENGINE tayari ni MALAYA kwa hiyo hilo la kuhonga mwili ili atatue tatizo la kupanda cheo wala si TATIZO kwake.:-(
Ndio,...
... matatizo uyasikiayo YALIYOWAPATA wengine ,...
...yana UANDUNJE hasa kama HUYASTADI katika kunyambulisha yatakuathiri vipi hasa kwa kuwa WEWE sio WATU WENGINE na staili na rasilimali zako za kuanzia AKILI mpaka ujiandaavyo tu kwa kuwa na kondomu au tu polishi ya viatu kabla viatu havijachafuka yawezavyokutofautisha TATIZO LILELILE kwako kutofautiana na hilohilo tatizo KWAKE.:-(
Anachokiwaza MTU kingekuwa ndicho pekee kitambulishacho UTU wa mtu ,...
... labda wengine tusingeitwa WATU na WEWE.
Na ukisoma HISTORIA utastukia , HITLER aliamini mpaka WARUSI kuwa sio watu vizuri, WAJAPANI waliamini WACHINA SIO WATU, na bila kusahau AFRIKA KUSINI kuna waliohubiri mpaka makanisani kuwa WATU WEUSI sio WATU,....
.... na ukiwaza waweza kustukia ni jinsi gani misingi ya MAWAZO HAYO yawezavyo kuota mizizi ambayo chimbuko lake ni imani kuwa MIMI kwakuwa sifanani nawe basi sina uhusiano na WEWE.
Unachowaza ,...
... labda sicho WEWE.
Lakini unachowaza,....
..... kinaweza kuwa kinachangia ulivyo WEWE.:-(
Swali:
AU?
Kwa bahati mbaya NACHO -kuwaza,....
..... pamoja na yote nijuayo yana kuhusu wewe bado nikiwazacho sio WEWE.
Labda akiwazacho mtu wakati anawaza,...
... HICHO NI WAZO tu hata kama ndicho kifanyacho ufikirie unayekabiliana naye ni sio jini au MALAIKA na ni MTU kama WEWE.:-(
Swali:
Unafikiri katika tafsiri yako ya ni nini ni MTU ni asilimia ngapi inachukuliwa na ANACHOKIWAZA katika kukutambulisha kwako kuwa yeye ni MTU?
Unauhakika kionekanacho kama mtu hakitoshi kuitwa MTU?
UKIWAZA,...
... unaweza kuanza kuamini kuna watu uwajuao ambao wala SI WATU kwa kuwa labda wawazavyo na NGEDERE wawazavyo ni sawa.:-(
UKIWAZA,...
... waweza mpaka kuamini kuna BATA wanafikiria kama KUKU kama kipimo ni mwendo wao wakuvuka barabara wakati wanalikimbia gari lako kwa spidi sawa.:-(
Swali:
Unauhakika unachowaza sio kikufanyacho WEWE ni wewe au unafikiria ni sura lako zuri ndilo linauzito zaidi kuwa wewe ni WEWE?
Unafikiri SURA LAKO halinamchango fulani katika UNAVYOWAZA ?
Unauhakika sura yako haichangii unavyowazia MAHARAGE?
NIMEACHA na hili NI WAZO TU!
Hebu USTADHI Zakir Hussein atupigie-Tabla solo
Au tu turudi Msumbiji Mariza abadili kwa ndude-Barco Negro
Mariza alete pia - Oh gente da minha terra
Au tuamie tena Cape Verde ili LURA amwage kitu-Na ri NA
....ni wakumbukao walidanganya nini siku za JANA zilizopita.
Na labda mwenye AKILI ambaye anadanganya mtu LEO,...
....katika kusaidia kufanya uongo wake udumu vizuri anatakiwa kukumbuka ADANGANYACHO LEO na baada ya kumaliza kudanganya ADANGANYACHO LEO kuKIkumbuka ALICHODANGANYA LEO SIKU ZIJAZO kama anataka uongo huo WA LEO ubakie na sura ileile na asiugeuze kuwa NI UKWELI siku zijazo kwa BAADA YA KUDANGANYA kuchukulia alichodanganya KAMA NI kitu kilichopita.
Swali:
Unakumbuka mwaka jana muda kama huu ulijidanganya nini ambacho kinaathiri kitu maishani mwako ambacho kimaisha KAMA HUJIKUMBUSHI KUWA hicho ULIJIDANGANYA hutaweza kukipita?
Kwani hujui KUDANGANYA vizuri kudumuko ni kazi ya WENYE akili wakumbukao kuoanisha uongo wao wa leo na ULE wa siku zilizopita?
Unakumbuka labda leo kunakitu umedanganya na unakichukulia kitendo hicho kama kitu kilichopita?
Ndio,...
... labda KUSEMA KWELI hurahisisha mambo kama nia na madhumuni ya MTU ni kujulikana MKWELI,...
... na kama UNADANGANYA lakini ukiwa na lengo lilelile la kuonekana MKWELI wahitaji kutumia akili vizuri LABDA ZAIDI YA MSEMA KWELI na pia jaribu kutosahau uhusiano wa ya leo na ULIYODANGANYA yaliyopita.:-(
NIMEACHA !
Kumbuka hili ni wazo tu MHESHIMIWA ambaye angalau katika KUTONGOZA hudanganya mtu!:-(
Hebu kwa kuwa leo ni JUMATATU tujikumbushe JUMAPILI kwa kuwasikiliza Maroon 5 wakiongelea-SUNDAY MORNING
... mtu anaweza kusahaulika katika SHUKURANI kama msikilizaji ni yule aaminiye ashukuriwa ye ni MUNGU KWA YOTE hata kama ni mtu ambaye ndiye akumbushaye ya MUNGU .:-(
Swali:
Unafikiri wakati unashida ya chumvi JIRANI akikusaidia chumvi naye hastahili SHUKURANI kwa kuwa unaamini awezeshaye yote ni MUNGU?
Si unajua stori ya matatizo kwa atafutaye na afikiriaye MASHUJAA anaweza kuwa anasikia stori za kishujaa tu katika ZE HADITHI?
Ndio,...
... stori ya KAWAIDA YA UHANGAIKALO NALO,...
... unaweza kuigeuza kuwa ni YA MATATIZO ingawa uhangaikalo nalo na JINSI UHANGAIKAVYO NALO wengine huita HILO ni ``MAISHA TU`´hasa kama unaangalia uhangaikalo nalo kwa LENSI ya matatizo na sio kwa lensi YA MAISHA ambayo moja ya jinsi ya kusaidia jipu lipone NI KULIBINYA JIPU.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
Hebu turudi MALI ili Mama Toumani KONE arudie ndude - Niemogo
Au tu turudi TanzaniaOmar KOPA arudie ndude nzito iitwayo-UNYAGO
Au tu Omar Kopa aongee busara zilizo tafutiwa mpaka siku kwa WABONGO -Kitchen Party
Kuna waongeleao WALI ukiwapa nafasi ya kuongelea WALI ,...
... wakati wakifikiriacho kabla ya wewe KUSAIDIA UWEZEKANO WA WALI KUONGELEWA kilikuwa ni UGALI.:-(
Swali:
Unabisha?
Aongeacho mtu kuhusu WEWE kinawezekana hakikuhusu wewe na kinatokana tu na UZOEFU WA YASIYO KUHUSU YA AONGEAYE hasa ukizingatia hakuna amjuaye mtu mwingine vizuri UKIFIKIRIA ingawa ni rahisi hata kudhania kwa kuwa mtu ni ndugu yako basi kuna kitu anajua katika wako UBINADAMU.:-(
Swali:
Lakini wewe unajijua?
Unauhakika unawajua vizuri hata wazazi wako hasa ukifikiria hujui kwa uhakika walikutengeneza chumbani au migombani wakati wanatoka kwenye msiba wa jirani?
Lakini si unajua kwa kutojiamini na kujijua kwako kunaweza kuwa ndiko kusaidiako KUAMINI KWAKO kuwa labda kuna mtu mwingine zaidi yako ndiye anaye KUJUA zaidi?
Ndio,...
.... baadhi ya tafsiri ya MATATIZO MENGINE YA MTU hutokea kwa kuwa MTU HUYO MHESHIMIWA kajifunza na kufudhu kutegemea WATU WENGINE WANAFIKIRIA NINI KUHUSU YEYE mpaka wanafikia kuamini hata kitu kidogo ambacho wanakijua kwa kujiangalia kwenye KIOO kinategemea watu wengine waseme uzuri wa MIDOMO YAO KAMA BIRIKA ni mizuri namna gani au tu ni watu wazuri vipi kwa kuwa hawakosi kwenda msikitini.:-(
NIMEACHA!
Hebu tubadili kwa SANCHEZ kurudi ndude- FRENZY
Au Tanto Metro andDevonte warudie kitu-Gal say Wooee
Tanto MetronaDevonte warudie-Everyone Falls in Love
..... na waweza kujikuta unashabikia vijulikanavyo na wanao kujua kuwa huwa vinakutia KINYAA.:-(
Penda,....
.....na waweza kujikuta aibu zinakuisha na kukusababisha uonekawaida na kudhani ni moja ya kuonyeshwa penzi kuombwa kitengeneza watoto sehemu ambazo zilitengwa katika majengo ili bila BUGUDHA watu wajifungie na KUNYA.
Penda,...
.....na waweza kujikuta kwa mara ya kwanza KWA SAUTI UNABISHANA na wazazi wako ambao busara zao ulikuwa unazitegemea kama ndio misingi ya maamuzi yako ya hata ni kwanini wewe INJINIA SIKU HIZI wakati ungekuwa MPISHI MENYE FURAHA kama ungejisikiliza wewe mwenyewe kama ujisikilizavyo WEWE BINAFSI NA KUWA NA UHAKIKA NA BUSARA ZAKO KATIKA MAAMUZI YAKO kama hasa UJIAMINIVYO NA MAAMUZI YAKO katika kutiii ni muda gani ILIUSIJINYEE inabidi uende chooni KUNYA.:-(
Swali:
Unafikiri kama ungekuwa mtiifu kwa unaloliamini ni KWELI ,- kama ulivyokuwa MTIIFU KUHUSU YAKUHUSUYO WEWE BINAFSI kuwa iliusijikojolee ni muda gani inabidi uende kukojoa,... -unafikiri ni mangapi katika maisha yako yangefanana na wewe au picha yako ya dunia utakavyo iwe?
Ndio,...
... kuna uwezekano ukiongea na mgonjwa wa MAPENZI busara zako hazina maana kwa kuwa zinatetea kitu KWA KUTUMIA AKILI ZAIDI YA HISIA wakati uongeaye naye anatumia HISIA ZAIDI YA KUJADILI SWALA KIAKILI kitu ambacho labda ni aina ya UKICHAA.:-(
Na kwa bahati mbaya naweza kusema pia; `` NDIO´´,...
....UKICHAA uletwao na PENZI huweza kusababisha CHUNGU KIDOGO kuonekana tamu SANA na kwa hilo labda MAPENZI ni aina tu ya UKICHAA.:-(
NIMEACHA!
Kumbuka NI WAZO TU HILI Mheshimiwa na unaruhusiwa kulitukania!:-(
Hebu Ray Parker Jr abadili kwa kuwatetea wanaume katika ndude- I don't think MAN should sleep ALONE.
[Tahadhari: Katika wazo LILILOPINDA KWA WAVIVU WAKUFIKIRIA bado taralila ina neno CHUPI.:-(]
.......WAKATI kuna MPENDA KEKI alazimikaye KUGIDA MIHOGO wakati wengine kwa hiari yao WENYEWE hawaonji wagawiwazo KEKI kwakuwa wanasubiria MIHOGO,... ....yaweza kumtungishia MTU MIMBA ya swali;...
....``KWANINI?´´:-(
Swali:
AU?
Ndio ,...
...KWANINI ,...
....ni SWALI la kawaida la mtu!:-(
Swali:
Unabisha?
KWANINI katika taralila yaweza kuwa ,...
....katika chupi YA KITABIA ivaliwayo siku ya MTU kupania kumuonjesha MCHUMBA utupu kwa mara ya kwanza ,...
...chupi HUWA imepaniwa iwe SAFI ZAIDI ya siku ambayo MCHUMBA HATA ANGALAU kwa mbali hatapewa nafasi ya kukodolea uwezekano wa ``MPENZI hajavaa KIFICHA NYETI ´´ kistaarabu ,... na labda NDIYO kiashiriacho kuwa MSTAARABU HUTAKIWI KUJUA kunasiku mtoto mzuri UMJUAYE KWA USAFI labda chupi yake sio safi sana kama KIBANGA ALIYEMPIGA MKOLONI ,...
.... NA inaweza HILO kuwa ndilo SWALI la MTU!:-(
NA kwanini,......
....msibani AU HARUSINI kuna wahisio PILAU HUNUKIA vizuri zaidi kuliko KWA MAMA NTILIE YULEYULE ambaye ndiye aliyekuwa na TENDA MSIBANI na PIA ZILE HARUSI KADHAA ULIZO HUDHURIA ambazo ilibidi tu uende kwa kuwa hukuchangia pesa hata za kujionyesha tu KWA WAPAPARIKIAO WAJIONYESHAO kuwa wanapesa kweli kifisadi ,....
...na LABDA hilo pia NDILO ni SWALI la mtu!:-(
Kwanini,...
...HATA ambaye kwa kawaida ndiye MWENYE NYEGE YA DINI AAMINIZO ZINAPELEKA WASIO WAJANJA DUNIANI kule MBINGUNI wakati KUMBE sio kila wakati HUYO NDIYE anajiamini kama ATAMKIAVYO WASIOJIAMINI hasa wakati atulizavyo manyanga ILI MEZA itulie,...
....halafu ikitulia ndio mnastukia kumbe YEYE NDIYE yule mtu wa MIZOGA wakati anaokoa SIKU katika juhudi zake za wa ngono YA ufisadi,....
....ndio laweza kugeuka kuwa ndilo GUMU KINAMNA swali la MTU.:-(
Swali:
Kwa WATANZANIA unafikiri ni kwanini Mheshimiwa KIKWETE na sio Mheshimiwa PROFESA SARUNGI au Mheshimiwa RASHIDI KWAWAWA ndiye aliye tangulia kuwa MHESHIMIWA RAIS WA TANZANIA kabla ya Waziri mkuu MORINGE SOKOINE ?
Unauhakika kwanini YESU hakuwa MWANAMKE?
Umeshawahi kujiuliza NI KWANINI SIO kila lifanyikalo LIKUHUSULO HUWA UNAKUMBUKA kujiuliza KWANINI?
Ndio,...
....LABDA ni kweli ,....
....KWANINI ni KIBONGE LA SWALI ndio maana SIO rahisi KUJIULIZA
ni kwanini inasemekana kuna MWINGINE aliyevulia mtu chupi mara moja tu na akapata KITU CHENYE THAMANI YA UWAZIRI wakati kuna aliyevulia chupi ZAIDI YA WATU WANNE NA NUSU na kutopata angalau BILAURI MOJA ya UJI WA MUHOGO wa asubuhi moja.:-(
Ndio,...
...labda kuna sababu ,....
....KWANINI ,...
....ni SWALI la mtu.:-(
Swali:
KWANINI?
Tukiachana na UjingaBUSARA wa hiki KIJIWE huwa LAKINI unakumbuka kujiuliza KWANINI mara kwa mara MAISHANI?
DUH !
NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA lakini ni wazo tu HILI MKUU !:-(
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!
Hebu Hugh MASEKELA abadili tu kwa kutukumbusha SOUTH AFRICA katika JAZZ katika ndude- Strawberry
Tubaki tu Afrika Jimmy Dludlu aendelee TENA kujaribu kulainisha wajanja kwa ndude -Tote
Au tuhame tu na tupate ndude -Casanova kutoka katika unajisi wa shughuli wa - Levert
....kunauwezekano UFANYACHO NDANI YA MUDA baada ya kuonja UTAMU ndicho KIKUPONESHACHO kumbukumbu ZA jinsi ulivyowahi kuusikilizia UTAMU.:-(
Ndio,...
....kuna wasemao kwa ung'eng'e ``TIME HEALS´´ a.k.a ``MUDA UNAPONYA´´ ingawa mimi ningependa kukualika ukae mkao wa kufikiria uwezekano wa kuwa - ``IT IS WHAT YOU DO within that TIME that DOES THE TRICK´´ a.k.a kwa lugha ya wajanja-``NI UFANYACHO baada ya KUUMIZWA au KUSIKILIZISHWA UTAMU ndicho kinaweza kukusahaulisha na KUPONYA uyakumbukavyo MAUMIVU au tu ule wa lawalawa UTAMU´´.:-(
Swali:
Kwani ni kweli ulifikiria maumivu na WIVU wa mwenye MPENZI aliyestukia MPENZI wake aliyekuwa anafikiri ni wake peke yake tu anagawia na wengine UJANJA huwa yanaponeshwa na MUDA TU bila kwa hilo lijamaa aka HILO lililostukia linadokolewa penzi na wajanja kujishughulisha na kitulizo kingine ambacho labda ni KWA kujisomea KORANI na kumsikiliza mchungaji wa PENTEKOSTE?
Unafikiri ni MUDA TU na sio na michango ya vitu hovyo kama vile WALI , mikate na VIAZI ambao vitakusaidia kusahau UTAMU wa UGALI NA MAHARAGE hapo baadaye ukiamua kujisahaulisha tamu yake kwa kuwa inakukumbusha sana MBWA wako mpenzi alipozirahi na kufariki dunia?
Ndio,...
... labda MUDA haukuponyeshi UKUMBUKAVYO utamu wa MAKANDE YALIYO CHACHA kama ndani ya muda baada ya kula PURE a.k.a MAKANDE yaliyochacha hautashughulika na kitakacho KURUDISHIA kumbukumbu ya UTAMU HALISI wa yale matamu MAKANDE.:-(
Ndio,...
....ukifikiria LABDA utastukia ni KWELI kuna kitu umefanya katika muda na sio MUDA TU ndicho kilichofanya hukumbuki vizuri ulivyotishika na DHAMBI baada ya kufanikiwa kwa mara ya kwanza kuifanya MAKUSUDI ndio sababu LABDA siku hizi unarudia HIYO dhambi makusudi KIRAHISI bila kujisikia vibaya sana.:-(
Ndio,...
....MATUMIZI ya MUDA na labda WALA sio muda ndicho kisababishacho kuna aina ya UTAMU huisahau na kunaaina ya MAUMIVU labda unailenga makusudi ili kujikumbusha jambo FULANI ingawa bila kufikiria ndio maana kuna MPENZI husahau maringo yake.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na haki ya nani tena NIMELIACHA!
Hebu tubadili kwa kwenda kiduchu BRAZIL Sergio Mendes atuletee tena kitu-Magalenha
Au tu Sergio Mendes naThe Black Eyed Peas warudie ndude-Mas Que Nada
Basi bwana , tubaki tu na Black eyed Peas ya enzi ZILE katika kitu kitukumbushacho wikiendi bado haijafika kiitwacho-Weekends
[Tahadhari: Wazo linatapatapa katika TARALILA HII!]
NIA ya kumsemelea MTU kwa mtu,....
..... inaweza kutoa SIRI ya MTU WA TATU ASEMELEAYE MTU ya anawafikiriaje hao watu wawili ajitahidio kuwaunganisha kwa MSEMELEO.:-(
Kuna wadaio PIA kuwa ukisemelea mtu,...
.... nia yako ni kutaka tu UKWELI ujulikane na SIO KINGINE,...
...na ikitokea kama unayemsemelea AKIPATA KIBANO basi hiyo huwa ni BONASI tu kama kwenye CHIPSI dume ilivyo KACHUMBARI ,....
....NA NI BONASI tu PIA kama UTAPATA FARAJA SANA TU hasa ikitokea ukashuhudia matunda yale YAKUSEMELEA KWAKO - yale ya KUGOMBEZWA kwa MTU, kubinywa KWAKE makende, KUFINYWA au tu KUDHALILIKA kukifanikishwa kutokana na wako MSEMELEO.
ILA kwa bahati mbaya ukiangalia tabia za watu,...
.... utastukia KWA KAWAIDA afikiriwaye ni MNYONGE ndio HUSEMELEWA kwa MBABE ili ikiwezekana ishuhudiwe akigawiwa MKONG'OTO au angalau KUGOMBEZWA kidogo baada ya MSEMELEO.:-(
Swali:
Unafikiri KIINI cha KUWASHWA kwa mtu mpaka ASEMELEE KITU kwa MTU huwa ni kweli ni NIA UKWELI UWE WAZI watu tumjue anyaye pembeni ya choo na KUFUTIA UTAJIRI kwenye ukuta wa choo ni nani au nia ni KUJIFAJIRI kwa MSEMELEAJI kwa KITENDO CHA KUSEMELEA?
Unakumbuka mara ya mwisho uliposemelea MTU?
Unafikiri kwa kawaida Tanzania , BABA akisemelewa kwa MAMA ina -nguvu?
NABADILI kidogo;....
Ndio,....
..... kunauwezekano hata ukiisemelea SERIKALI YA TANZANIA kwa WANANCHI,...
..... wananchi hushindwa kufanya kitu ingawa ndio wenye NGUVU na matokeo yake wengi twashuhudia WASEMELEAO WANANCHI kwa SERIKALI kwa kuwa wanajua SERIKALI ina polisi na MAGEREZA- bila kusahau vyombo vya habari ivitawalavyo ambavyo vyaweza kustua watu NCHI NZIMA wasiona HATA NA mpango na WEWE kuwa umekaa uchi bila kificha nyeti UDHALILIKE kwenye jamii na kwa ALIYEKUSEMELEA.
NARUDI PALEPALE;.....
Ingawa kirahisi katika JAMII ya KITANZANIA inaweza kuaminika ``MAMA ntakusemelea kwa BABA´´ inanguvu zaidi ya ``BABA ntakusemelea kwa MAMA´´,...
.... ukweli wenyewe waweza kuwa uko kinyume kwa kuwa labda MAMA ndio mwenye nafasi nzuri ya kumuadhibu BABA kama adhabu aamuayo kuitumia NI ITUMIAYO AKILI ZAIDI na sio ile ioanishwayo na MIGUVU ya MISULI na PESA za BABA.:-(
Swali:
Si unakumbuka achangiaye kuonekana MWANAMKE ni dhaifu inawezekana ni MIMI na WEWE hasa weye mwenyewe MWANAMKE?
SI imekuwa kawaida kwa MWANANCHI kusemelewa kwa vyombo vya mabavu vya SERIKALI mpaka inasahauliwa ni WANANCHI HAOHAO WAOGOPAO SERIKALI ndio bila wao hakuna SERIKALI hata hiyo isiyowajali yaweza kujitutumua kwa MAGUVU?
Unauhakika lakini BABA mwenye MIGUVU na MAMA wakianzisha vita baada ya wewe kumsemelea BABA kwa MAMA hawezi kudedi MDINGI ambaye kazoea kupikiwa na MAMA MWENYA AKILI na kutarajia MINOFU YOTE MIKUBWAMIKUBWA ya BATA apewa yeye kwenye ZE MLO ambao watoto huambulia mchuzi na mabakimabaki ya chembechembe za mnofu wa BATA kabla BABA hajarudi usiku KALEWA?
Ndio,...
NIA ya kumsemelea MTU,....
..... inaweza ikawa ni kujisikia vizuri tu kwa ASEMELEAYE hasa kama anachokisemelea hakimuhusu ASEMELEAYE kuwa UNANANILIHIII ambacho hata KISIPONANILIWA hata afanyeje HATA KINANILII YEYE .:-(
Ndio,....
.... sibishi kuna ASEMELEAYE mtu,....
.... kwa nia ya kusawazisha kosa ili UNAYENANILII usijezoea tabia MBAYA ambayo itasababisha UNANILIWE hapo baadaye.:-(
NIMEACHA wazo MHESHIMIWA na kumbuka hili ni wazo tu ambalo ni RUKSA kutolielewa!:-(
BWANA na BIBI wasifiwe!
Tupoze basi kwa kumsikiliza tena Mheshimiwa IDD AMIN
Tuendelee kidogo na Mheshimiwa Idd AMIN
Na tumsikilize kidogo tena Mheshimiwa KIBAKI
Sasa twende kwenye KIPELE nikilengacho bila utani-Where Will We Find Tomorrow's Leaders?
[Tahadhari: Taralila hii KUNAUWEZEKANO ina wazo lililopinda!:-(]
BINADAMU katika anunuayo:....
....katika CHAKULA,...
....LABDA katika MAPUNGUFU hununua msosi akifikiria UTAMU badala ya VIRUTUBISHO VYA MWILI ambavyo kwa BINADMU ndivyo muhimu kiafya na UZIMA.:-(
Katika WACHUMBA ,....
.... labda hununua hata kwa mizawadi LIMTU ZIMA na MITABIA YAKE MIBOVU wakati labda wahitajicho katika mtu ni SEHEMU ZAKE TU BAADHI au tu zile za siri , - kitu kisababisha BINADAMU huendelea kujikuta CHUMBANI yuko na Limtu LIZIMA.:-(
Katika fulani DINI,....
....kwa sadaka na MWENENDO labda MTUZ hujinunulia STAILI YA MAISHA kama IHESHIMIWAVYO NA BINADAMU badala ya kustukia havinunuliki VIKUZA IMANI vile vilainishavyo woga wa MUNGU MWEMA lakini ACHOMAYE VIUMBE alivyoviumba KATIKA wabadaye UZIMA.:-(
Swali:
Unafikiri KIBINADAMU ni rahisi kununua samaki bila shombo yake?
Kwa BINADAMU unafikiri kuna anunuacho ambacho hakina makapi hasa ukifikiria hata katika chakula kitamu KILIWACHO ni asilimia ngapi huja na kile ambacho BAADAYE binadamu hukiita mavi?
Ndio,...
....LABDA katika UDHAIFU WA KIBINADAMU huwezi kununua SAMAKI bila MIBA yake.:-(
Na NDIO,...
....labda kila BINADAMU anunuacho lazima kiwe KIKUBWA zaidi ya ahitajicho na akinunua GARI basi amenunua na matatizo YA GARI LAKE na akinunua CHAKULA kitamu basi HICHO lazima kije na uzito utakaogeuka mavi yake. .:-(
Swali:
AU?
Ndio,...
...labda katika kila kitu anunuacho BINADAMU ni KIKUBWA kuliko MAHITAJI YAKE,....
....na labda hata chupi inunuliwayo NA KIGOLI imezidi UKUBWA kama inaziba tako zima KAMA nia ya asili ya UTUMISHI WA CHUPI ili kuwa ni ili izibe matundu mawili tu YA SIRI ya KIGOLI yaliyo mbele na SEHEMUSEHEMU ZILE fulani katika ramani YA YALE makalio YAKE.:-(
Swali:
AU?
Ndio ,....
...labda hata uendeayo SHULE ili ujisikie UMEELIMIKA yamezidi UKUBWA kuliko MAHITAJI YAKO ndio kisa katika MIA ya uyasomayo darasani labda ni moja KATIKA HAYO ambalo UKIKAA VIBAYA utakiona cha mtema kuni kikweli MAISHANI NA KUKIKUMBUKA UKIJUTIA kwa kuwa DARASANI hukuelewa hicho MAANA YAKE .:-(
.
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA !:-(
Au tu tumpate Ex Plantashun mwingine a.k.a 2FACE IDIBIA akija na Wyclef Jean katika ndude- Proud to be AFRICAN
Au tubaki tu hapahapa Nigeria Ex Plantashun Boiz 2FACE IDIBIA aje na R.Kelly waweke twist katika wimbo wa ya MAD COBRA katika -FLEX
Au tu MAD COBRA mwenyewe arudie classic -FLEX Read more...