Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kinachotembea kama bata na kulia kama bata, SIO LAZIMA NI BATA!:-(

>> Tuesday, September 08, 2009

Unaweza kunibishia!


Lakini maisha ya binadamu siku hizi yalivyojaa UNAFIKI mpaka hata MALAYA wanamapozi MPAKA ya KILOKOLE!:-(


Na waitwao WAHESHIMIWA mpaka hata kwa wizi hawawezekani!:-(

Na wakuhubiriao dini wanachosahau tu ni kwambia fanya nayosema lakini sio nayofanya kwakuwa wafanyayo waweza kukuta ni bomba la dhambi mpaka neno dhambi linaonekana kama ni uji wakati kiongelewacho ni ugali mgumu wa Kisukuma .



DUH!
Nimeacha WAZO!


Ngojea OPRAH aongelee tena ya Nabiii Issa....katika-Oprah Denies Christ


Au tu ngojea Marilyn Manson abalansi kwa kitu-Beautiful People

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:02 am  

Au hujui siku hizi ni unafiki hadi kwenye utoaji misaada? Hujui kuna watu wanamwaga misaada ya mamilioni huku mtoto wa dada yake amerudishwa shule kisa kakosa ada ya 20000 tu!

Simon Kitururu 10:35 am  

@Askofu Fadhy: Si utani!:-(

Umenikumbusha mpaka ya nchi kama Marekani ambayo inaweza kuwa na pesa za kwenda Mwezini wakati kuna walalao na njaa mtaani hapo hapo Marekani na washindwao gharama za matibabu idaio haina pesa kwenye bajeti ya nchi ya kuwasaidia.
. Inaweza ikakukomalia kuhusu misaada ukatishika mpaka usikie ukubwa wa deni lake yenyewe idaiwayo na CHina!


:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP