Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NYOLINYOLI! Wewe UNACHO kidude, mie sina!:-(

>> Sunday, September 13, 2009

[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]

Wenyenacho,...
.... huwa na mchezo wa kufikiri kwa kuwa wanacho basi WANAKIHITAJI!

Na kama kwao ni muhimu walichonacho,...
... wanafikiri na kwako ni muhimu na ni HITAJI.


Na AKUNYOLISHAYE kwa kuwa nacho,...
.... huyo anafikiri tu akunyolishacho UNAKIHITAJI.

Lakini KUTOKUWA nacho,...
..mara nyingi ni nafuu kuliko kuwa nacho kidude kama dira ni tu umuhimu wa MAHITAJI.

Fikiria tena UTAKACHO kuwanacho,...
...waweza KUGUNDUA chupi mbili zinatosha kama nia ya kuwa na chupi ni tumizi tu la chupi HATA ukiunganisha mpaka UMUHIMU WA KUBADILI CHUPI wakati MOJA CHUPI UMEFUA baada ya kitunza nyeti kuchafuka baada ya kutimiza zamu yake ya HATA kujambiwa hata kama HILO sio la chupi tumizi muhimu au HITAJI.

Ndio KIDUDE unacho,...
...lakini baada ya kufikisha CHUPI YA TATU na ZAIDI, ingawa unaweza kunibishia, hapo UTATUACHO KWA CHUPI YA TATU NA ZAIDI sio tena kile kile cha tumizi la chupi kama MGAMBO WA ZA SIRI NYETI ndio ulengacho kama HITAJI.

Na inawezekana ikawa ushajitungia umuhimu MPAKA WA KUREMBESHA ulichonacho,...
.... na labda kidude hutaki kionwe ghafla KILIVYONUNA baada ya kukivulia gauni au bichikoma NA KWA HILO wafikiri kificha nyeti a.k.a CHUPI kikipendeza kwa usafi au KWA KUWA NA MAUA YA rangi ya SAMAWATI , basi cha sahaulisha watu KUWA kilengwacho KUONJWA hutumika pia kutoa MWILINI MWA LIMTU uchafu HASA kama MOJA TU YA la muhimu kwa binadamu la nyeti tumizi la nyeti HITAJI.:-(

Na wafikiriao wanacho,...
....na inaweza ikawa MPAKA hata ni dini ZAO WALIZONAZO wadaizo za wapeleka mbinguniziwafanyazo HATA KAMA WEWE HUAMINI WAAMINICHO, wanaweza fikiria kuwa wanahitaji kukuokoa kwa vile wanafikiri kwa kuwa wao wanataka kwenda mbinguni basi na wewe lazima unataka kwenda mbinguni ingawa wewe mwenyewe mlevi na dini zao ZENYEWE haziendekezi ulevi hata mbinguni KWAO na wanafikiri bado kwako kwenda mbinguni kwao WADAIKO ni kwenye juisi na kuimba sana lazima kwako ni MUHIMU kama kwao WAKATI wewe MWENYEWE hupendi kuimba hata kama ni kuimba na malaika na JUISI KWAKO haipandi na HUIHITAJI.:-(

Swali:
  • Ushastukia mara karibu zote ni wafikiriao wanacho hata usichohitajindio waKUnyolishao?
  • UNafikiri ukistukia una MDUDU utatunyolisha kwa kuwa unao?
  • Ushawahi KUMNYOLISHA MTU/kumringishia mtu kwa kutokuwa na kitu?

NIMEACHA WAZO HILI Mheshimiwa Banangenge NA kumbuka ni WAZO tu USIKONDE!!:-(

Na kutakia JUMAPILI zaidi ya UGALI KWA MAHARAGE kama hupendi UGALI KWA MAHARAGWE Kijeba au weye Mdada OSHKOSH!





Ngojea nimuachie HITLER a rap-



Au ngojea Sizzla adai-Rise to the Occasion

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 7:58 am  

Ukiwa nayo moja ndo kazi yake ni kuwa mgambo wa nyeti. Lakini zikishaanza kujaa kabati na madoido mbali mbali pale zinakuwa virembesho vya eneo wakati wa kumnyolisha fundi bomba anapokuwa katika maombi ya kazi ya kuunga mabomba ya majitaka.

Simon Kitururu 9:17 am  

@Papaa Fadhy: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP