Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

R.I.P Elvis Musiba!

>> Sunday, October 31, 2010


Nakiri ni stori za Willy Gamba zilizonitambulisha huyu Mheshimiwa!

Kwa kujua zaidi habari zake soma HAPA
.
.

Au soma hapa kwa Lukwangule Entertainment.
.


Poleni Wafiwa!
R.I.P Elvis A. Musiba!

Read more...

LEO nawatakieni UCHAGUZI Mwema !

Wiki hii nimejikuta nikisikikiza malumbano ya UCHAGUZI kutoka kwa marafiki watokao BRAZIL, Ivory COAST na Tanzania ambao wote LEO ni siku ya kupiga kura katika NCHI ZAO.



Kila la kheri WABRAZIL,...
......WaIVORY COAST na WATANZANIA mpigao kura leo!

Katika kuilenga TANZANIA:
Tuombee AMANI na uchaguzi huu uende SHWARI! 
MUNGU IBARIKI TANZANIA!

NI HILO TU!



Hebu Ze comedy wabadili kwa -Muziki mnene huu


Ze comedy katika - Kurudisha chenji muhimu



Au tu ngojea Lágbájá na abadili tu na- Bling Bling Panda



AU tu Lágbájá ambaye ni msanii nimuheshimuye labda kuliko wote Nigeria sasa hivi arudie-Gra gra

Read more...

Aliyeandika kuhusu swala la TITI labda sio HASA ni yule MTAALAMU wa MATITI!:-(

>> Saturday, October 30, 2010

Wakati unakula MLENDA,....

....kumbuka TU  kuna WATAALAMU WALIOKUBUHU KATIKA KUJUA ambao wako kimya,...
....wasiopata nafasi ya kuandika KIUTAALAMU WAO kuhusu MLENDA,....
...au wasiojua tu jinsi ya kusimulia KIMAANDISHI jinsi ya kupika MLENDA wakati unasikiliza AU UNAWASOMA waongeleao MLENDA.:-(



Na umsomapo Simon Kitururu akiongelea  kipengele cha mwili kitumikacho sana MSALANI,....
..... kumbuka tu  kuwa kuna wataalamu ZAIDI wa jinsi ya kubana matumizi ya muda na umadhubuti wa utumiavyo kipengele huko MSALANI ambao wako kimya kwa sababu mbaimbali  zikiwemo za kawaida  kama zile za HESHIMA kwa kudhani  wakiongelea kipengele anuai  wataonekana kama SIMON kuwa si WAHESHIMIWA .

Swali:
  • SI unajua labda SHEKHE YAHYA  pamoja na kutoongelea zaidi BIBLIA kama aongeleavyo utabiri labda anaijua BIBLIA kuliko hata ASKOFU kadhaa za KILUTHERI  katika mpekecho wa BIBLIA?
  • Si umestukia kuwa labda kunauwezekano ingawa  ni wanawake ndio wenye titi lenye ujazo NA UTAALAMU WA JINSI YA KUISHI NA TITI NONO  wa kutosha lakini labda kuna mwanaume  ndio muongeleaji titi zaidi?


Nawaza tu MKUU!

Hebu ARRESTED DEVELOPMENT warudishe ustaarabu kwa-Revolution



Walete- Tennessee



Arrested Development warudie-Mr Wendal



Au tu ARRESTED DEVELOPMENT wamalizie na-People Everyday

Read more...

Binadamu WAKIZOEA KITU hupenda kuendeleza kutenda walivyozoea HATA kama walivyovizoea havifanyi kazi tena hata katika jinsi viamshavyo PENZI kama MCHUMBA ageukapo MKE!:-(

Binadamu wakizoea hata kuliambia limtu ``I LOVE U!´´,....

.....wanaweza kujikuta WANAENDELEA TU KULIAMBIA limtu ``I love U´´,....
....hata kama siku hizi hawalipendi hilo LIMTU ki ``I LOVE U!´´,....
..... kisa kisa wamezoea tu na mazoea yamegeuka TABIA nyumbani wakati siku hizi ni HAUSIGELI apendwaye kuliko MKE hasa tokea HAUSIGELI ajulie KUJISOPUSOPU na kuzibua uzuri wake uliokuwa umejificha kwa KIDUME aka MME wa MTU chini ya miguu yenye MAGAGA, bonge la kikwapa na kadhalika nyingine kadhaa zilizokuwa hazina mvuto kwa kidume mwanzoni kutokana na familia KIFISADI ilivyo zoea kutafuta mahausigeli kutoka katika famili zisizojiweza ili wa MDHULUMU mfanyakazi wa ndani kwa kumpa mshahara mdogo kabla hajastuka.:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,....
.... watu wakizoea kuweka mbolea ya chumvi chumvi kwenye shamba lao,....
..... kirahisi wataendelea kutumia mbolea ya chumvi chumvi hata wakiambiwa inaharibu udongo wa shamba lao kama tu waliozoea kupiga kavukavu wakataavyo kondomu hata wakisimuliwa stori za UKIMWI.:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
..... binadamu hupenda kuendeleza walivyozoea hata kama walivyozoea havifanyi kazi tena,...
.... na labda ndio maana bado ndoa yako imedumu ukizingatia labda ulichuja utamu zamani tu ,...
.... kitunzacho uhusiano wako na MWENZI WAKO ni mazoea tu ya kuendeleza tu VILIVYOZOELEKA.:-(

Niwazo tu hili MHESHIMIWA !:-(
Jumamosi NJEMA!



Hebu Snoop DOGG abadili kwa kitu-Sixx Minutes

Read more...

Wakati MOHAMMED ndio jina maarufu wapewalo WATOTO Uingereza na FINLAND!

Taka usitake kunakitu chaweza kukuingia akilini KITAFAKURI,....

..... kama utatafakari kuwa nchi kama FINLAND ambayo ni ya KIKRISTO mpaka SEREKALI ndiyo itozayo watu sadaka za KANISA kwa kukata watu  mshahara  kama kodi ya KANISA kwa ajili ya KANISA hasa la KILUTHERI ,....

.....katika data unakuta watoto wengi wapya wakiume MOHAMMED ni moja ya jinalitawalalo,....


.....pia nchi kama UINGEREZA ambayo kihistoria ni ya KIKRISTO  ukisikia pia ni jina hilohilo MOHAMMED ndio linatawala.

Hebu deku watu wanasemaje kuhusu hilo UK...




Swali:

  • Wakristo MPO ?
  • Au ndio nyie mliozidisha kugeuza kipengele cha kutengenezea mtoto kuwa ni KIBURUDISHO MURUA tu KWA KUWA TAMU na mitoto hamzai kwa kuwa kuilea mitoto ni kibano kama kupanga foleni RTC kununua UNGA WA YANGA enzi za NYERERE baada ya vita na Mheshimiwa Idd AMIN?


NAWAZA TU MKUU usikonde!



Hebu Gilberto Gil abadili mkao wa wazo kwa kurudia -Aquele Abraço




Au hebu tubakie Brazil  ELIS REGINA  anisaidie kuendelea kubadili hali ya hewa hapa kijiweni kwa ndude -Madalena


Read more...

Ngojea RUMMY mutoto ya KARIAKOO aendelee... na ALIKO MWAKANJUKI aage!!

>> Friday, October 29, 2010

Photobucket







Nimemkumbuka tu mtoto wa kariakoo   RUMMY aka Mr B aka Rumpunch  kwa kuwa sijamuona siku nyingi!

















Nafikiri mara ya mwisho ambao ni muda kitambo kidogo nilivyomuona  ni tulivyopiga picha hiii...

Photobucket


Hebu aendeleze na bendi yake Mighty 44....

THIS love!


Abandike pia....

PUSH IT



Rummy nakusabahi Mkuu!
Pamoja sana MKUU!



Halafu watu MLIOKO au mtakao weza kufika HELSINKI,....

ALIKO Mwakanjuki aka DJ ALTUNEZ ambaye ni huyu hapa.....

Photobucket






AU huyu hapa na mimi....
Photobucket



Anaaaga marafiki waliokuwa naye mitaa ya ULAYA  kwa kuwa anahamia bara jingine siku ya tarehe 13.11.2010 kama tangazo linong'onezavyo.....


Huyu namchagulia jiwe SHUB IN la FRANKIE PAUL


Pamoja sana MKUU!

Read more...

Sikiliza LABDA unaweza kuelewa, SIKILIZIA , na labda KWA HILO utapata OGAZIMU!:-(

[Tahadhari: Wazo katika TARALILA HII limepinda na linamapengo!:-(]


Tatizo moja LA WATU ni kuwa WANAPAPARA na,....
..... ndio maana  wwanaweza kunogewa kwa papara kama WATANZANIA wawezavyo kunonogewa kwa papara na Waziri  LIYATONGA MREMA kuliko,...
......Waziri MKUU MORINGE Sokoine.:-(


Swali:
  • AU?
  • Samahani kama huzijui siasa za Tanzania na kama hilo linakusaidia kutojua SIASA ya Liyatonga Mrema na Moringe Sokoine si nasikia sikuizi kunakitu kina itwa GOOGLE ambacho ukigoogle unaweza kujua kuwa Profesa Lipumba ni PROFESA kweli?

Kama HUNIELEWI,....


....tulia,....
...na wakati umetulia UKIKUNWA sikilizia,....
..... na akiguna SIKILIZA pia,....

...na labda KISIKILIZWACHO bila PAPARA  katika MAISHA kinaweza mpaka kukuwekea wazi  UDHAIFU WA DINI YAKO PIA katika tu kukuelewesha MACHACHE utakayo ELEWA au tu utakayo kuwa na moyo wa kukubali kuwa umeelewa na hayako kama uyafuatavyo kisa PAPA BENEDIKTI kasema usitumie KONDOMU,...


... hata kwa kisingizio kuna kitu unajua sasa kuliko BABU YAKO kama wanasiasa wa CCM walivyojua hata kabla NYERERE hajafa kuwa kuna kitu  alikuwa anawaficha kwa kuwa yeye IKULU alikuwa anaangalia BBC kwenye TV  tokea enzi TANZANIA kunaaminika hakuna TV wakati wewe TANZANIA BARA  KUWA NA VIDEO ilikuwa noma.:-(


SWALI:
  • SI unajua ni RUKSA kutoelewa TARARILA HII inalenga hasa nini?
Ndio,...
.....sikiliza LABDA unaweza kuelewa, SIKILIZIA  , na labda  KWA HILO utapata OGAZIMU!:-(

NIMEACHA !

WIKIENDI NJEMA kwa kuwa naiunganisha kiKHERI KWAKO Ijumaa hiii kwenye hiyo kitu WIKIENDI kwako MHESHIMIWA!:-(


Tuko PAMOJA!




Hebu SHAKIRA alete -LOCA



SHAKIRA arudie pia -  HIPS dont lie


Au tu  hebu BIG YOUTH awaulize TENA wajifanyao wajanja SIKU HIZI kuwa wakati   SHUGHULI inafanyika mwanzo -Where were all dem boys

Read more...

Lile SWALA la kuwa pamoja na nguo zote ASKOFU ajivalishazo chini ya nguo kama WEWE bado yuko UCHI!:-(

Kuvaa NGUO labda PAMOJA na yote YA USTAARABU wa jamii ya yakwepayo kukabili tusi la ndani ya nguo,...

 .......ni kwamba ,....
......CHINI YA NGUO  yako au hata ya SISTA WA KIKATOLIKI  aaminiwaye  KWA KUSALI sana kama vile YESU ni MCHUMBA WAKE  ,...
..... ni kama  tu  juhudi ya WASUKUMA kukataa wali haunogi ,....
..... au katika upande huohuo KINAMNA wa kuwa WALI SIO bomba sana kama MATOKE au KUMBIKUMBI WALIOKAANGWA kwa WAHAYA katika swala la ,....
.... chini ya nguo hata kama navyojaribu kutafuta lugha ambayo itakuwa laini na unastukia kuwa sijapata ni ,...
....uko UCHI!:-(



Kuna MAMBO yasiyouchi,...
....WATU wayafikiriayo mpaka yanageuza kifikira kuwa UCHI,....
.... kwa kuwa KWA KUFIKIRIA HATA UGUMU WA MAISHA wanayapanua miguuu hata yenye chupi kwenye ENGO ya kati yenye goli,....
.... mpaka unaweza kuzani  ni kweli HAYO  ;....
....DUKA LA MZUNGU LIWAZI , lauza MCHELE NA NAZI  , kaniona mimi HALAFU eti  anafunga!.:-(


NIMEACHA na wazolilikuwa linaendelea na liendeleze MKUU!
  • AU?:-(


Hebu Sankomota adinye mdinyo- Papa



Au tu Jabu Khanyile aendeleze mtekenyo - Mbombela




Basi bwana hebu JUDY MOWATT amalizie na -BLACK WOMAN

Read more...

Jifanye MJINGA mapenzi yako yadumu na limpenzi lako KIBOGOYO!:-(

>> Thursday, October 28, 2010

Siri ya MAFANIKIO ya mengi ni TIMING a.k.a KUJULIA MUDA wa kuongelea au hata kufanya jambo,....

....kitu kifanyacho kuwa moja ya siri ya kutogombana na WAKO MPENZI kibogoyo,....
.....ni kuhakikisha kuna muda unajifanya MJINGA wakati mpenzi YUKO katika MUDI ya kujifanya kila kitu ANAJUA.:-(

Kumbuka kwa kujifanya mjinga,....
.....wewe bado sio MJINGA.:-(

Swali:
  • SI unakumbuka mara nyingi siri ya kugombana kwa watu wawili ni kwamba wote wawili hakuna anayejishusha katika lumbano lipandishalo jazba ambalo laweza kuzalisha fulu kupigana ngeu?

Ndio,....
....mara nyingine hakuna sababu ya kubishana NA MPENZI kama unajua jibu lako ndilo sahihi,....
....kwa sababu KATIKA MAPENZI kama unamjua vizuri MPENZI,....
....basi wajua kuna wakati JAMBO asilokusikiliza hata UKIBISHANA atakuwa katulia anakusikiliza kama tu UJUAVYO ni wakati gani mzuri kumchuna buzi MPENZI wakati kakaa mkao wa kukubali kila kitu na weye unataka kwenda SHOPINGI.:-(

Swali:
  • AU?
  • Si unajua kuna muda BWANA LAKO BAHIRI ni rahisi kukupa pesa kama unalijulia MATAIMINGI?
  • Na siunajua KATIKA TAIMINGI muda mzuri wa kumshushua MKE wako sio mbele za watu ?

Ndio,....
..... kama unataka kukwepa migongano isiyo na maana MAISHANI,....
..... kama unajijua sio MJINGA ,....
....ki-TAIMINGI si vibaya kujifanya MJINGA  na mwenzio naye aonyeshe maringo yake dingilidingili mpaka chini kuwa naye ANAJUA.:-(

Swali zaidi:
  • Kwani kila siku ni lazima MJUAJI awe wewe tu jamaniiiii?Loh Lione Vile!


Habari ndio HIYO na NI WAZO TU HILI LA LEO MKUU!




Hebu Tshala Mwana aingilie kati kipengele




Au tu Caiphus Semenya arudie tena jiwe-Angelina




Na Chicco aingilie ghafla na -We Miss You Manelo

Read more...

Jana ndani ya mji wa Tampere na Bloga MALKIORY MATIYA na Deo Mponda!

 Katika kuhangaika naye,...
....jana nilijikuta katika mji uitwao TAMPERE ambao Bloga MALKIORY  MATIYA na DEO MPONDA  ndiko wahangaikako naye mpaka kieleweke......


Ingawa muda  ulikuwa na kibano chake kwa kuwa mie ilibidi nidandie USAFIRI  na kuanza kivyangu tena  ,....
.... kwa mara ya kwanza nilikutana uso kwa uso na BLOGA huyu ambaye  ukimtembelea kwenye blogu yake ya ; MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI/Forward ever BACKWARD NEVER,...

.... utajua  yuko makini.


STORI kibao na kama kawaida kujifunza kitu kulikuwepo.

Baadhi ya Picha  zilizotunguliwa   katika tukio.....





Bloga Malkiory Matiya



Nguli DEO MPONDA




Ilikuwa ni furaha sana tu kukutana na ndugu hawa na NI HILO TU MKUU!

Au hebu Letta Mbulu arudie - Mahlalela




Letta Mbulu aingizie-Carry on



Au tu tena Dorothy Masuka aingilie shughuli na kumwaga -Teya TEYA

Read more...

Nachosema na UNACHOSIKIA vinaweza visiwe na uhusiano!:-(

>> Tuesday, October 26, 2010

Labda sio unachosema ndio chenye umuhimu,.....
.... kwa kuwa ni kile wanaokusikiliza wanachosikia ndicho  KASHESHE!:-(

Na kwa bahati mbaya si kila asemaye cha muhimu,....
...... husikilizwa na akisemacho kutiliwa maanani moja kwa moja na ndio maana hicho hicho CHA MAANA  kitu akikiongea Mama NTILIE adharauliwaye  chaweza kutopewa umuhimu  ingawa akikiongea hivyohivyo MANDELA kuna watu watasikiliza na kukipa umuhimu kama ubwabwa wa msibani kwa aliyezamia msibani  bila KASHESHE.:-(


Swali:
  • SI bado kunauwezekano nilichoandika na ulichotafsiri baada ya kunisoma labda havina uhusiano?

Naendelea kuwaza....:-(

Lakini unaweza tu  kujiliwaza kwa kushuhudia ulimwenguni katika SHOO BIZ ustaarabu wa watu umefikia wapi kwa kudeku hii promosheni ya Puppetry of the PENIS



Au tu cheki na Puppetry of the vagina

Read more...

Kwa wale washabiki wa Paul the Octopus!

Jamaa kaanza hivyo leo ,....
POLENI!:-(





Naamini huyu Paul the psychic Octupus (hatched January 2008 - 26 October 2010) ni moja ya ushahidi  mambo ya kishirikina au imani za ajabu ajabu  ni hai dunia nzima ukizingatia kuna watu kibao walikuwa wanamchukulia VERE SIRIASI na tabiri zake katika World CUP!


Ni HILO TU!!

Read more...

R.I .P Gregory Isaacs!

Gregory (15 July 1951 – 25 October 2010) ni miongoni mwa wanamziki wa Reggae niwapendao sana.

Asante kwa miziki lukuki Mkuu!
R..I..P!



Hebu arudie-Tune in



Aingizie- Number one



Au aachie tu pia -Sad Mood tonight

Read more...

Wakati MSAADA TUTANI unaanza kutishia kugeuza TUTA kuwa ni kituo rasmi cha BASI.

Adoado HUZOELEKA.
Na  kwa dogo kama KUSHIKWA KIBINDO labda ndio mwanzo wa kupigwa MUELEKA.
Na wakati kuombwa dogo   INAELEWEKA,...
... labda OMBI hata kwa MUNGU liwe ni wakati ombi  katika hitaji kikweli LAHITAJIKA.
Kwani azoeaye  tegemezi la MSAADA hata wa DALADALA lisimame TUTANI linaloeleweka,....
..... labda afanyacho katika OMBI ni tabia tu  kutokana na mazoea kwakuwa  kutojitegemea nako HUZOELEKA.:-(



Swali:
  • Unafikiri  wengi hata MAKANISANI wamuombacho MUNGU sio  ni kwa kuwa kumuomba MUNGU ni  jambo LILILOZOELEKA tu?

NI WAZO TU HILI BINGWA na wala usikonde!:-(

Hebu tumsikilize tena Robert Mugabe


Au ngojea tujikumbushe tena  baadhi ya mitazamo ya nguli Muammar Gaddafi



Au tu tena Simple Minds warudie tu tena - Mandela Day


Read more...

Katika kufikiria nje ya BOKSI unoko wa RAIS NYERERE ,....

>> Monday, October 25, 2010

.....................


Swali:
  • Hudhani  kunauwezekano KUBANIA ULAJI kwa RAIS NYERERE ndio  moja ya sababu  zilizozidisha  WATOTO WA MJINI waliochukua SEHEMU ZENYE ULAJI kupandwa mdadi zaidi wa  UFISADI?

Naendelea KUTAFAKARI SWALA.....:-(






Hebu FALLY IPUPA adinye-MABELE



Fally Ipupa aendelee tena na -Bakandja




J Martins ft. P Square na Timaya wa dondoshe nyundo - Good Or Bad (Owey)



Au tu Ngojea J Martins na FALLY IPUPA waanzishe...



Au tu ngojea waache nyolinyoli na kuuatu jabali -Jupa

Read more...

Uzuri wa KUMA na MBOO,....

.... labda unaongezeka bila SABABU kwa kuwa HADHARANI WAHESHIMIWA  kama wewe ambao katika jamii MNAHESHIMIKA kuliko mimi,....



..... mnageuza jina la kipengele cha MWILI CHA KAWAIDA AMBACHO labda kila MTU ANACHO  kiwe topiki kubwa na ya AJABU mpaka hata kifaa kama titi  na chuchu  inageuka pia kuwa tusi,....


....kisa  mnataka kuamini  kuwa  HESHIMA  na NENO vinauhusiano  kama muaminivyo zaidi kuwa MTU ASIPOTAMKA NENO  kama mkundu  kirahisi kama atamkavyo EMBE BOLIBO basi yeye ndio wakuheshimiwa zaidi INGAWA INAJULIKANA KWENYE AFIKIRIAYO yaitwayo  MATUSI  YAPO na  INAJULIKANA PIA kwa kuwa  YEYE ni  fisadi na UFISADI WAKE  ndio usababishao watoto wa masikini hata wakienda shule watabakia wajinga kwa kuwa hata walimu wenyewe wazuri hupenda kufundisha watoto wa matajiri ujinga ni nini,...
.... labda yeye ndio mwenye matusi  ingawa PADRE wa kiroma na WEWE labda hamoni hilo.:-(




Swali:
  • SI unajua neno mboo kama tu kisimi kwa lugha ya KIINGEREZA ipendelewayo na wasomi wa BONGO havina maana?:-(

Ni wazo tu HILI Mheshimiwa na samahani kama katika ustaarabu wako moja ya tafsiri ya nilichoandika ni MATUSI na ni RUKSA KUTONIELEWA MHESHIMIWA!!:-(



Hebu CHIWONISO arudishe TENA ustaarabu hapa kijiweni kwa jiwe-Wandirasa



Louis Armstrong aingilie kati ustaarabu kwa -Hello Dolly




Louis Armstrong aendelee kustaarabisha kwa - La vie en rose




Lois Armstrong adinye tu kistaarabu pia-What a wonderful world



Au tu hebu katika kubadili mguno  Heavy D arudie nyundo-Truthfull

Read more...

SI kila mtu ATAKUBALIANA na wewe hata katika JAMBO ZURI ufanyalo lenye MAANA kijinga!:-(

PAMOJA NA YOTE,...
.... labda  ni vizuri kukumbuka,....


..... KILA MTU anashabiki wake  hata kwa ambayo kwa MTAZAMO WAKO afanyayo  mtu na SURA YAKE MTU  ni kama usilolipenda PARACHICHI ingawa hata bila kumchunguza kikojoleo unajua kwa vyovyote  hata kisivyo kibusara bado kama wewe huyo sio PARACHICHI aka MAKATAPELA ,....


.... na haki ya nani hata pamoja na umalaika umsukumiao ukimnusa maeneo kabla hajajiswafi wajua KIUHAKIKA  pamoja na harufu kama shombo za samaki huyo ni MTU.:-(





Swali:
  • SI unakumbuka hata HITLER alikuwa na girlfriend?


Ndio,...
 .....PARACHICHI  kama tu makande sio tamu kwa kila MTU.:-(

NIMEACHA na ruksa KUTOELEWA Mkuu!:-(

Ndio huyu ni mimi Simon Kitururu wakati bado kijana na nachana nywele.:-(



Hebu jamaa alie tena...


Au tu hebu JIMI HENDRIX asawazishe tena kwa -All along the watch tower


Jimi Hendrix adinye pia -VOODOO CHILD




Au tu James Brown na Lenny Kravitz walainishe tena kwa -Papas got a brand new bag



SIjui kwanini lakini hebu Jimi HENDIX arudie kitu live


Read more...

Kuhusu MOROGORO Sekondari!:-(

Kuna kipindi tuliosoma hapoMOROSEKI  ilikuwa ni wale WALIOPASI MITIHANI ya darasa la saba vizuri na ilikuwa unaweza hata kumringia mtu kama udhaifu wako ni huo kwa kuwa ukionekana tu MOROGORO MJINI na yunifomu ya MOROSEKI wanajua weye kichwa.:-(



Nachosikitika si kwa kuwa wenye akili  MOROGORO ni MOROSEKI ni  shule ya mwisho kujaribu  kuipa shavu ni MOROGORO SEKONDARI siku hizi,....

.... ila pia tuNI SWALA ZIMA NCHI NZIMA  ilivyofikia kuwa siku hizi karibu NCHI NZIMA YA TANZANIA shule za serekali ndizo zinazokwepwa,...
....kisa ndizo ambazo  unaweza kwenda kuondoa ujinga na kubakia MJINGA,:-(


Swali:
  • SI unajua kwa aliyewahi kusoma MOROSEKI siku hizi ukisikia yanayoendelea hapo  kama una aibu ni AIBU TU?
  • SI unajua  si wanafunzi tu wakwepao shule za SERIKALI kwakuwa hata walimu nao wamestukia  kukwepa shule za serikali inalipa pia?

Hebu akina Jeff Msangi  wa BONGO CELEBRITY na wengine  ambao mpo katika ulimwengu wa kublogi ambao mnawezwa kuguswa na SWALA LA MOROGORO SEKONDARI nisaidieni  mtazamo kama mtasoma hiii ndude kwa kuwa nahisi Moroseki inawahusu pia.:-(


SAMAHANI  kama huhusiki na hii taralila MKUU!



Moja kwa moja hebu AMERIE aanzishe kwa-Gotta Work




Au labda LL Cool J na Boyz II Men katika kubadili tena zaidi kwa kulainisha zaidi warudie-Hey Lover




Au labda LL COOJ na Amerie katika kuondoa ulaini kidogo tena wadinye-Paradise



Au tu Amerie peke yake arudie mdinyo nyundo - 1 THING

Read more...

JHIKOMAN!

>> Sunday, October 24, 2010

Huyu jamaa ni  rafiki yangu   tokea zamani.



Na ndio,...
.... alinitangulia darasa moja Morogoro Sekondari.

Barikiwa na baadhi ya kazi zake....

Mapenzi



Kuagana


Au tuendelee kutatua swala la Jhikoman ni nani...



Baadhi ya picha wakati nimemtembelea BAGAMOYO kwake...














Baadhi ya picha tulipokutana mitaaani kusipokuwa Tanzania....






Read more...

WAKATI natafakari kwanini inaweza kuonekana FIDEL CASTRO kawashinda WAMAREKANI lakini ushindi HUO sio wa CUBA!

[Tahadhari: Naongea kimaandishi nikiwa naifikiria  pia TANZANIA na   kutafakari  ya Robert Mugabe]


Moja ya UDHAIFU wa  NCHI ZA MAGHARIBI ,...
.... ni siasa zake za uangalifu katika kutaka kuuza danganya toto  zionekane ni TAKATIFU zenye watu wazuri wenye kupenda amani  na hazina agenda  mbaya  kwa nchi nyingine.:-(

Na ukifikiria utastukia pia ,....
.... kama MAREKANI isingekuwa inajali DUNIA itaionaje nchi hiyo,...
....FIDEL CASTRO asingeshinda vita  na WALA nchi kama AFGHANISTAN , PAKISTAN  au hata LIBYA chini ya  Muammar Abu Minyar al-Qaddhāfī  zisingezingua kihivyo kwa kuwa  kirahisi tu kwa nguvu za mabomu zingefutiliwa mbali  ,...
....hasa kama MAREKANI ingekuwa inafuata mfumo wa KI -Al-Qaida wa  kama kuna wakumlipua ukilipua na wasiohusika MUNGU hana noma na hiyo ishu.

Na  watu kama FIDEL CASTRO  ni miongoni mwa watu wajuao sana MAADUI ZAO ,...
... na baada ya kujua udhaifu wa MAADUI zao ,...
.... hupatia kucheza na UDHAIFU wao.


Swali:
  • Hufikirii kuwa moja ya udhaifu au kiwapunguziacho nguvu  VIONGOZI wa magharibi  ni  DEMOKRASIA?


  • Kwani hujui KIONGOZI mwenye nguvu kabisa ambaye yuko juu ya mahakama zote za DUNIA sasa hivi ni Rais wa CHINA kutokana na kutokuwepo demokrasia na kutokuwepo awezaye kupamburua AMRI yake  ambayo hakuna  mahakama ya CHINA iwezayo kupingana nayo?




Ndio,...
.... pamoja na washabiki wa FIDEL CASTRO kustukia huyu MZEE kashinda na atakufa kama El Comandante,....
.... hivi tunauhakika ushindi wa FIDEL ni wa CUBA ambayo  wananchi wake kibano wanakiona?

Unafikiri  ushindi wa Robert Mugabe ni ushindi wa Zimbabwe?


Tukirudi Tanzania ,...
.... unafikiria nini  ukitafakari ushindi wa Marais wote waliowahikuchaguliwa TANZANI A, unafikiri ushindi wao ulikuwa ni ushindi wa TANZANIA,....


...hasa kwa kuwa kuanzia Rais Nyerere pamoja na kujua moyo wake ulikuwa mahali sahihi  bado unaweza kupata watakaodai alikuwa na udhaifu katika kujua udhaifu wa anaokabiliana nao ndani na nje ya nchi ya Tanzania?:-(


Naendelea kuwaza......



Tubadili  mkao kwa kuwasikiliza Jagged Edge wakibinya jipu kwa-Walked OUTTA Heaven


Craig Mack aingilie kati na kurudia-Flava In Ya Ear




Au tu nitafakari Fela Kuti angekuwa hai leo angekuwa anafikiria nini akiusikiliza wimbo wake na ROY AYERS uitwao-2000 Blacks Got To Be Free

Read more...

Siri ya MAFANIKIO ya WENGI katika KUJENGA GHOROFA, kupata KURA au tu hata KUPATA DEMU ni kucheza na UDHAIFU wa watu WENGINE!

Na siri  KUBWA ya WACHUNGAJI, mapadre, maaskofu ,MASHEKHE au tu hata wainjilisti,....
.... ni  KUJULIA tu jinsi ya kucheza na UDHAIFU wa WAUMINI wenye misingi  kwenye HOFU ZAO WAUMINI za kuogopa JEHANAMU  au tu  ule udhaifu mkubwa zaidi wa WAUMINI kutopata maana ya maisha yao BILA msaada wa yaendanayo na HALELUYAH au ASALAM ALEIKUM,....
....ambayo hudindishwa na KIDINI na hao wajanja ndani ya SWALA ZIMA ambalo ni bonge la kiosha ubongo ni DIMNI.:-(




Swali:
  • SI unajua kuna watu kuabudu NG'OMBE au tu KUKU anayetetea ndicho kifanyacho maisha yao yawe na MAANA HAPA DUNIANI hasa kama WAINJILISTI wa hizo dini wanajua kuwapukuchulia waumini wahizo dini kama tu WEWE KWENYE DINI YAKO uoanisho KIMAANA wa hizo DINI na maana ya MAISHA YA MUUMINI wa dini hizo?


Ndio,...
...labda siri ya mafanikio yako ,....
.... ni udhaifu wa MTU mwingine ambao umefanya  leo wewe UMEFANIKIWA.:-(

NI WAZO TU HILI MKUU na RUKSA kutolielewa!:-(






Hebu  A.K.A KOXX arudie-Girlfriend




Au tu A.K.A KOXX arudie pia-More Than Gold










Nimekumbuka tu filingi zilizokuwepo kwenye siku hii.....








Read more...

Nachojaribu kuongea HAPA katika BLOGU hii,....

>> Friday, October 22, 2010

....nikiitacho UjingaBUSARA,....
....kinaweza kuwa ni KWELI ni UJINGA kwa WATU fulani ,....
..... hasa wafikiriao katika UJINGA hakuna CHAKUJIFUNZA.:-(





TUNAKUMBUSHANA tu MKUU kabla sijakutakia BOMBA la IJUMAA na WIKIENDI NJEMA.









Haya basi WAKUU,...
..Ijumaa njema na BOMBA la WIKIENDI Waheshimiwa!
TUKO PAMOJA WAKUU!













Mie naanza hivyo kivyangu lakini siwezi kukuacha bila kukuachia DWELE anong'oneze kitu ambacho unaweza kumshutumu kama unaingilia mambo kwa papara bila kusikiliza na kuelewa katika -I am cheatin'


Dwele amwage tena na nyundo-Weekend LOVE



Halafu hebu tu na  MUSIQ abandike tu pia nyundo-HALFCRAZY

Read more...

Kama tukichunguza Waheshimiwa WAHAYA walikuwa wanafikiria NINI kilicholeta uvumbuzi muhimu wa KATELERO,...

....  waweza STUKIA  staili hiyo ya FIKIRA inachakuigwa.

Kama tu ukichunguza ni kwanini kila MKOA Tanzania kuna WACHAGA na biashara zao kama KENYA ilivyo kuwa na WAKIKUYU na biashara zao na kulipaumakini swala la JINSI  wahahavyo ILI  tu kuhakikisha WANAJIAJIRI hata kama ni wasomile  na  KAZI ZA KUAJIRIWA WANGEPATA na kushuka UNG'ENG'E  wanashuka kama  tu  WAZENJI washukavyo KIUNGUJA  nyororo kuliko wa  wa DAR mabishororo,.....
...... katika nchi kama TANZANNIA ambayo serikali kamwe haitaweza kutoa ajira kwa wote  LABDA basi kwao kuna la KUIGWA.:-(


Swali:
  • SI unajua nchi kama MAREKANI  ajira kubwa hutolewa na wafanyabiashara  ambao  hulka zao ni kama WACHAGA Tanzania na sera nyingi za nchi hiyo ni za kujaribu kukuza uwepo wa watu wenye silika kama za KICHAGA?

Na haki ya nani UKILICHUNGUZA KABILA lako  utagundua kuna ya KUIGWA MENGI TU ingawa KWA BAHATI MBAYA  na ya kuyatolea nje kinamna kama yale ya kutahiri KIDUDE  mabinti yapigiwayo kelele yaachwe kwa sababu zihusishwanishwazo na  utamu, AFYA au tu  kwa kuwa shughuli nzimaYA KULIPIGIA KELELE SWALA inalipa watu mishahara Ki- N.G.O  iliyostukia ulaji,.....
.. bila kusahau yale ya KAMA ya BAADHI  ya WALUGURU ya KAZOPATA ya kuona ni afadhali WAHINDI au hata WAPARE wapate kuliko apate MLUGURU mwenzao,...
.....YAPO.:-(



Swali:

  • AU?
Ndio,....
.....Ukichunguza  ubunifu wa WAHAYA katika  kitu chenye uhusiano na pekechapekecha kama KATELERO ,...

.... halafu ukawaza NJE YA BOKSI  na kustukia  karibu kila kitu ukifanyacho labda kina katelero yake,....

... basi labda kila kitu ujihusishanishacho nacho  kuna UTUNDU  ukikifanyia utamu utazidi zaidi na badala ya DARASANI kupata B utapata A,...
.... au badala ya kuwa mzibua vyoo wa kawaida waweza kujikuta unamiliki KAMPUNI ya kuzibua vyoo AFRIKA MASHARIKI,....


.. au tu badala ya kuwa FISADI udhulumuye WANANCHI wenzako ukawa bomba la FISADI udhulumuye WAWEKEZAJI WANYONYAJI  kwa manufaa ya WANANCHI WENZAKO  mpaka kieleweke ili WANACHI wako nao wawe wawekezaji katika nchi isiyoendelea ya MAREKANI  kama  hali halisi  itakavyojitokeza  hapo baadaye.:-(

Swali nje kidogo ya tundu:
  • SI unakumbuka uwezekano wa MAREKANI aka USA kuwa nchi inayoendelea  na SIO ILIYOENDELEA hapo baadaye  kama unakumbuka MONGOLIA enzi za Ginghis Khan, MISRI yakina Farao , hadi URENO zilishawahi kuwa ndio nchi tajiri na zilizoendelea kuliko zote kama isifikavyo MAREKANI sasa?
  • SI unajua ukifikiria NJE YA BOKSI   suluhisho la jirani la jinsi ya kuboresha VITUMBUA inaweza kukufanya WEWE ugundue jinsi ya kuboresha KEKI  kwa hiyo labda  kwa kudadisi  katelero unaweza kupata mwanga katika ugunduzi wa manukato ya kunako?
  • Si unajua karibu kila kifaa utumiacho  chanzo chake kilikuwa ni TATIZO na kwa hiyo kama unatatizo labda unamwanya wa kuwa wewe ndio MTATUZI?

Kabla hatujaachana na  KATELERO:
  • Je MHESHIMIWA umeshawahi kuifanyia utafiti hii kitu?

Basi BWANA  kama hujawahi kuifanyia UTAFITI  HII KITU na hujui maliwazo yake katika umadhubuti wa maliwazo  kwa ushirikiano wake na PEMBEJEO ZA KAZI NANIHINO  usitishike KAMA TARALILA HII HUIELEWI inalenga nini katika KUAMSHA hisia na TAFAKARI wala zisizo na uhusiano na KATELERO  ambayo mamasta wake ni WAHAYA by reputation Mheshimiwa.:-(











NI WAZO TU HILI  MHESHIMIWA!:-(




Update:
  • Baada ya kusoma comment ya Papaa Mubelwa ambaye ni MUHAYA naamini neno KATELERO katika taralila yangu  HII lisomeke: KATERERO .:-(



Moja kwa moja Majek FASHEK aingilie tena kati na kurudisha ustaarabu hapa kijiweni kwa kuongelea -AFRICA UNITY


Majek Fashek aendelee na -So LONG


Au tu Baaba Maal amalizie tu kwa kurudia -Yela

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP