Wakati tunamkumbuka Nyerere, ....Rashid KAWAWA OYEE!
>> Thursday, October 14, 2010
Wakati tunamkumbuka NYERERE,...
.... ni muhimu pia kukumbuka yasemekana KAWAWA ndiye mmoja wa waliyekuwa KIBOKO katika kutekeleza ya NYERERE ambayo yanasaidia NYERERE anavyokumbukwa sasa.,........ na kama unabisha waweza kushauriwa angalau wakati NYERERE anaongelea VIJIJI VYA UJAMAA ni nani hasa alikuwa anatekeleza kiutekelezaji na si maneno ili viwepo vijiji vya UJAMAA.:-(
Kwa kifupi:
...Kila PAPA JOHN PAUL II kuna Kadinali Joseph Alois Ratzinger wake ambaye PAPA JOHN PAUL akisakizia mbwa a.k.a kidogi ; shikashikashika
- Ratzinger anang'ata mtu.
Swali:
- SI unajua tukichukulia kuwa DR Slaa ni RAIS WA TANZANIA anaweza akawa ni BOMBA la muongeaji na bila MTEKELEZAJI chadema itagundulika kuwa haina meno katika kung'ata?
- Si unajua kuwa HAPA najaribu TU kukumbusha kuwa MAFANIKIO ya NYERERE labda kuna umuhimu yakiwagusa na ambao walikuwa mstari wa mbele KIUTEKELEZAJI kuhakikisha PAMOJA NA MENGINE MENGI labda ni pamoja na kufanya katika kabila lenu CHIFU hana nguvu kikweli kitu kilichosaidia wewe sio mkabila sana kama Waganda?
PUMZIKA VYEMA Kingunge NYERERE na ASANTE KWA YOTE ulioufanyia UTANZANIA na TANZANIA!
Mie moja kwa moja naenda kumsikiliza Dr REMMY akitonesha kidonda kwa kuzungumzia-KIFO
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Daima tutakukumbuka Nyerere.Tanzania uliyoiacha si hii ya sasa, mambo ni shagalabagala...kiufupi mambo si shwari babu.
R.I.P
Tutakukumbuka daima na daima. Utuombee nasi kwani wote tutakuja huko.Ustarehe kwa amani!!
Post a Comment