Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunawasiwasi na JINSI KIGOLI alivyojifunza kuona AIBU!:-(

>> Thursday, October 07, 2010

Ndio,...
....kunaaina tofauti tofauti za aibu,....
.... na katika aina za AIBU,....

.....UTAMADUNI uutokao unamchango wake katika swala zima la NI NINI unakionea AIBU.:-(

Na kama kwenu UFISADI au tu tuseme umalaya ni LIFE STYLE aka gia mojawapo ya MAISHA na ni  kawaida,...
.... yaweza kuhitaji ujifunze KITU kama vile ni nini  watu  wengine kwenye jamii  ya kijijini kwenu wanaufikiriaje UFISADI na UMALAYA ili uanze angalau huko kijijini kwenu  kuuonea AIBU.:-(

Swali kiduchu kabla ya kuendelea kuipapasa hoja:
  •  Chakujiuliza ni je AIBUZAKO ulizaliwa nazo au ulijifunza?
  • SI unajua inasemekana hata ADAMU na EVA ambao walikuwa ni binadamu wa kwanza walijifunzia ukubwani KUONEANA AIBU kukaa bila nguo aka DUKA LA MZUNGU LI WAZI  ingawa walikuwa ndio BINADAMU  wawili tu duniani hasa ukizingatia labda hakukua na sababu ya kumficha MUNGU isemekaye ni  aonaye yote duniani au hata pia MIJUSI na WANYAMA WENGINE ambao labda hawapati bakshasha yoyote kwa kuchungulia mtu ambaye hajavaa kificha nyeti katika bustani ya EDENI?

  • Na labda SI kuna WAKULIMA wa geza ulole itakaobidi wajifunze upya kutouonea NOMA ukulima baada ya kuja mjini katika kukwepa kutambuliwa na watoto wa mjini wao ni WAKULIMA WA MBILIMBI pale MBILIMBI zitakapogeuka ni  ujanja kwa watoto wa mjini?



Ndio,....
.....wote tunajua AIBU haiui,....
... na kuna baadhi ya AIBU kuna watu wamezaliwa nazo hata ziwezacho kufanya mtu ashindwe kula vizuri msibani au tu kushindwa kumueleza AMPENDAYE  ukweli kuwa anampenda ,....
.... kitu ambacho KINAUA angalau uwezekano wa KUZALIWA baadhi ya ambalo lingekuwa penzi la kweli,.....

.... au kuachia mpendwa aishi KWA KUTOJIAMINI  bila kujua kuwa ingawa kila ajaribupo kuonyesha maringo yake ANACHOKISIKIA NI KICHEKO cha DHARAU na KEJELI bado kuna ambao WANAMPENDA na kupenda mwendo wake kama bata  kwa dhati  tu.:-(

Nikiacha utani:
  • Si unajua kuona kwako aibu  LABDA kumekukosesha mengi tukiachilia mbali kushindwa kushiba msibani labda pia kumesababisha  cheo ukitakacho usikipate, MPENZI umpendaye ushindwe kumuomba unyumba, marehemu ambaye kafariki labda afe kwa majonzi bila kujua ULIMHESHIMU au tu ujisikie vibaya kwa mambo ambayo ungeweza kujivunia?


Ila tukumbuke uwezekano kuwa,.....
...... unaweza kujifunza kuona aibu,....
.... na kwa hiyo ona aibu basi kama wewe ni FISADI kwa kuwa kitendo hicho labda kinaua watu ambao  wanakuheshimu .

Na labda tukumbuke pia,....
... kujifunza kutokuwa na AIBU kunawezekana tu pia,...
..... na kama unabisha hebu fikiria limpenzi lako lililokuwa na aibu  sikuhizi hata haya halina vile hata kwenye mibinuko  ya kiasherati .Khaaa!:-(



NAEndelea kuwaza....:-(

Unaweza kujifunza zaidi kwanini unaona HAYA ukistukia unakitovu kama kitumbua hapa kwenye http://www.shyness.com/encyclopedia.html

AU ingia tu huku kwenye wikipedia ambako sina uhakika kama ni Askofu Kakobe kaandika au Mh Shekhe Yahaya kwenye sentensi  zifuatanazo kama :

Origins of Shyness

The initial causes of shyness vary. Scientists have located some genetic data that supports the hypothesis that shyness is at least partially genetic. However, there is also evidence that the environment in which a person is raised can affect his or her shyness. This includes child abuse, particularly emotional abuse such as ridicule. Shyness can originate after a person has experienced a physical anxiety reaction; at other times, shyness seems to develop first and then later causes physical symptoms of anxiety. Shyness differs from social anxiety, which is a broader, often depression-related psychological condition including the experience of fear, apprehension or worrying about being evaluated by others in social situations to the extent of inducing panic.

... kwa kukongoli HAPA


AU HEBU tu kwa mara nyingine Esperanza Spalding safari hii akiwa White House atulize manyanga na kutekenya bezi nipendavyo bila michecheto katika kitu-Overjoyed


Na sijui kwanini lakini hebu tu tena Ritchie Spice aingilie tena shughuli kwa kurudia-More life

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDNA 11:00 am  

Mmmmmh haya mtakatifu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP